Ujenzi wa Nyumba: Je, ninaweza kujenga kanyumba kadogo kazuri kwa bajeti ya Mil. 6!?

Kwa gharama hizi ni bora kuhamia mkoani
 
ukiongelea nyumba manake unaongelea
-msingi (matofali, kifusi, mchanga, cement,kokoto)
-lintel/beams (mchanga, kokoto, cement)
-boma (tofali, cement, mchanga)
-plaster (mchanga, cement)
-rangi (gypsum powder, rangi nk)
-upauaji (mbao, bati, misumari nk)
-umeme (mfumo wa umeme, switch, sockets etc)
-maji (mfumo wa maji, fittings)
-floor (floor ya kawaida, tiles mbal etc)
-ceiling (blundering, gypsum/plywood)
-madirisha (grilles, aluminium/mbao)
-milango (frame, milango, vitasa, bawaba, grille doors)
-tanesco (kuunganisha umeme)
-mfumo wa maji taka (chamber, mabomba, septic/soak away pit)
-kuna swala mambo mengine kama usafiri (materials), maji, ulinzi, hifadhi/store, umeme wa kuazima, usimamizi nk.


kwa 6m unajenga nyumba ila labda hatua za mwanzoni.
kama huna haraka unaweza anza itakupunguzia ukiwa unaendelea.
 
Inategemea uko wapi kama ni dar kwa pesa hiyo labda ujenge kwa awamu, weka msingi kwanza
 

Unaamini kabisa kwa milioni sita atachimba msingi,utanunua tofali,cementi,mchanga,nondo,bati,na kisha umlipe fundi? Anyway tunaishi katika ulimwengu wa adventure,inawezekana!
 
Japokuwa mada si yangu nilikuwa ninapenda kuuliza mfano una kajumba ka vyumba viwili(kimoja master), sebule, choo cha public na jiko. Eneo la ujenzi ni 10X10m. Ili uezeke bati ya m-south, umalizie finishing na kuvuta umeme walau mtu atenge kiasi gani?
 
Weka 18000000
 
Kwny iyo 6M kata 18% VAT ya Magufuli kinachobaki ndo upangie hesabu!
 
Unaamini kabisa kwa milioni sita atachimba msingi,utanunua tofali,cementi,mchanga,nondo,bati,na kisha umlipe fundi? Anyway tunaishi katika ulimwengu wa adventure,inawezekana!
mkuu milioni sita atanunua tofali tu na mchanga. apo haja anza kujenga. kujenga ajipange atleast na 10 to 15 kwa kuanzia.
 
Eneo ulilopo linaweza kueleza zaidi. Nyumba ya milioni kumi dar kule kijijini kwangu yaweza kuwa 3.5M. Tueleze mahali ulipo kwanza ndo tutajua.
 
Shida ipo ktk Raman yako hatuijui. Kwa maelezo yako inaleta picha kuwa ndogo ila ukubwa wa master, jiko, sebule, choo hatujui. Tupe vipimo tukupe tathmini halis ya bati.
Kuhusu umeme kuna nguzo jirani? Au hakuna?
 
Kiwanja anacho tayari. Kwa 6m anajenga kanyumba kadogo msimuogopeshe. Sikia rafiki, unaweza jenga. Tumia bati za kawaida ila ziwe grade 28 bundle@240k, silingboard si lazima kuweka, madirisha weka ya kawaida(mbao)@120k, milango ni 4@180k, ujenzi wote msingi had paa 1.3m. Tofali 1800@1000 zinatosha hadi karo la maji taka.
 
mchanganuo wako unatoa mwanga mahali pa kuanzia, hiyo pesa inatosha kabisa lakini itabidi finishing iwe ya Kawaida sana, kuna vitu anaweza ku save mfano madirisha usinunue yaliyotengenezwa badala yake nunua material tafuta fundi akutengenezee utaokoa almost laki tatu hapo, pia fundi ujenzi agiza mkoani tsh million mmoja watajenga kuanzia msingi hadi kupaua, kwa kifupi INATOSHA tofari tumia zile za interlock utaokoa gharama ya ripu, cement pia gharama za ufundi
 
kaka asante kwa ushauri, ninaufanyia kazi nimeamua kujenga hivyo hivyo ingawa bajeti inabana
 
acha kumpotosha. kuna kumpa mtu moyo kwenye kitu ila sio kwenye uongo. unasema tofali 1800@1000, manake hiyo ni 1.8m afu unasema tena ujenzi wote msingi hadi paa 1.3m inakuaje apo.
milango 4 @ 180,000. uo mlango una frame, door panel, kitasa, bawaba? au labda aweke frame na mlango wa bati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…