Ujenzi wa nyumba kwa bajeti ya milion 5

Ujenzi wa nyumba kwa bajeti ya milion 5

Nina kiwanja cha 20m kwa 20m, nataka kujenga 11m kwa 11m room Tatu sebule Choo na bafu za kawaida milioni kumi na tano, nitaweza kuanza kuishi kama haijakamik
Akili zetu watanzania ni kujenga tu.. Tumejiwekea imani kuwa bila kujenga maisha hayaendi... Anzisha biashara, zalisha hayo mamilioni, utajenga tu
mjini ukiwa na pakulala hela ya kula haikusumbui kwahiyo kujenga muhimu
 
Tuliza kichwa halafu fundi asijue kiasi ulicho nacho halafu kingine peleleza mafundi maana unaweza kutana na makanjanja kila kitu ununue mwenyewe yaani mtu asilambe hela yako bila kusota
 
Ujenzi kwanza

Mkuu jenga,mambo mengine utayajua mbele kwa mbele,hiyo hela ukiingiza kwenye biashara sasa hivi huna bahati. Uzuri kutokana na hali ilivyo sasa ufundi na materials nyingine unaweza kuzungumza. Ila usije kubargain sana ukampata fundi feki au materials zisizo na viwango.
 
Najua ubahili ni hasara
 
Watu wanajidanganya sana kwa hidden roof ,gharama za kuaandaa ili iitwe hidden ni mara mbili ya kununua mbao na bati ingawa at the end utatumia mbao na bati chache.
Sio kweli. Nimejenga hidden roof nyumba kubwa na roof ya kawaida nyumba ndogo. Nyumba ndogo ni gharama kuliko kubwa yenye hidden roof.
Na ninajenga nyingine nitatumia hidden roof style tena. Changamoto ni kudhibiti leakage ambayo ukipata fundi mzuri sio issue.
 
Nina kiwanja cha 20m kwa 20m, nataka kujenga 11m kwa 11m room Tatu sebule Choo na bafu za kawaida milioni kumi na tano, nitaweza kuanza kuishi kama haijakamilika?
Mkuu wasiliana na UVIMO watakusaidia mengi.

0753927572 -Wasap
0629361896 -Kupiga
 
Unaweza ila muhimu uwe na muda wa kusimamia ujenzi na upate fundi mzuri.

Hivi ni vitu muhimu kujua bei yake kabla hujaanza.
_ Mchanga
_ Cement
_Mawe
_ Kokoto
_ Tofali

Msingi usizidi ml 3, hapa hakikisha umemwaga na jamvi
Boma liende 4 ml
Kuezeka mil 4
Shimo la choo laki 8
Grill 1.2
Mlango wa mbele na nyuma laki 5 na flem zake
Plaster nje ndani mil 1.3
Laki 2 dharula

Ujenzi unawezekana chief, muhimu ni kuwa na roho ngumu na kuziba masikio,maana wakatisha tamaa ni wengi.

All the best.
Shikamoo Mkuu,,
 
Nina kiwanja cha 20m kwa 20m, nataka kujenga 11m kwa 11m room Tatu sebule Choo na bafu za kawaida milioni kumi na tano, nitaweza kuanza kuishi kama haijakamilika?
Fanya 9M by 9M utaweza kumaliza kwa asilimia 75 then umalizie taratibu.Boma Utatumia Milioni 6,Kupaua Milioni 6,Unaweza kuamia huku ukiendelea kuimalizia taratibu.NB.Bei inategemea na eneo unalojenga kwani gharama zinaweza ongezeka kutokana na eneo.Kama unayo ramani tayari tuwasiliana PM kwa ushauri na connection zaidi
 
Akili zetu watanzania ni kujenga tu.. Tumejiwekea imani kuwa bila kujenga maisha hayaendi... Anzisha biashara, zalisha hayo mamilioni, utajenga tu
Biashara kipaji mkuu, wala msimtamanishe mtu.

Hujawahi kuuchuuza hata njiti za viberiti ukajifanye mfanyi Biashara mashuhuri, hiyo Pesa yote inapotea.

Ibaki tu wengine tujenge mungu akijaalia tuitwe Baba mwenyenyumba kisha nyie watu wa Biashara mje muwe Wapangaji wetu basi.
 
Back
Top Bottom