Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Siku hayo Madini ya copper na cobalt yakiisha au kupungua ardhini huko zambia utahamisha mataruma?
Huo mzigo uliogunduliwa Congo ni mwingi sana miaka mingi mno. Na thamani ya cobalt imepanda kwa kuwa inatumika kwenye vifaa vyote vya umeme. Pia kutengenezea betri za lithium ion za magari ya umeme. Kwa hiyo mzigo wa cobalt ulipo Katanga congo ni mwingi sana. Pia bado kuna mzigo wa Copper kama wote huko Congo miaka mingi mno.
 
Unamlaumu jamaa bure. Hayuko katika nafasi za maamuzi. Ni sawa na mimi ninavotamani SGR ingefika Dodoma na kula kona kwenda Tunduma! Mizigo ya Rwanda, Burundi na mashariki ya DRC ingechukuliwa Dodoma au MGR ingeimarishwa kutoka hapo kwenda Mwanza na Kigoma!

Nimebaki kuwa na matamanio tu na siwezi kuwa na maamuzi juu ya hilo.
Aisee yaani tumekula hasara kizembe mizigo mingi mno ipo Zambia na Congo.
 
Jiji la pili kwa ukubwa Tanzania linaitwaje?

Unajua kwa nini daraja la Kigongo busisi linajengwa?

Unajua kwa nini meli kubwa sana inajengwa ziwa victoria?

Unajua Uganda wanapitishia wapi mizigo yao?

Unaijua population ya kanda ya ziwa?

In short huna akili kabisa
Barabara na reli ya kawaida akutoka Tabora ingetosha kuhudumia mizigo ya a mwanza na uganda. Ushamba tu.
 
Kwani hii reli ya Sasa wameifanya Nini Hadi wanakazaka kuwapa waturuki pesa?
Unategemea mafisadi wenye malori zaidi ya elfu moja watakubali SGR ikamilike? Wenye malori zaidi ya 599 Ni watu wenye connection na high places.
Mimi na suggest hizo hela wangezitumie kuleta maji Dar es Salaam. Hivi tunavyoongea 29/12/2021 hakuna maji tangu Jana jioni. Umeme ndio huu wa kuunga unga vijana wa welding hawalali maana hawajui Kama kesho kutakua na pawa.
Tatueni kero za wananchi SGR sio kipaumbele kwa sisi watu wa Kimara.
 
Zambia ndio wameuza nchi yao kwa wachina. Kumbuka mambo huenda yakibadilika. Rwanda na Burundi utaziona mzigo wake reli itakapokamilika.

Hii tabia ya kulalamika haitufikishi popote, zaidi ya kujionyesha namna gani tusivyo na ubunifu vichwani.
Mzigo wa Rwanda, Congo DRC, na Zambia unaoingia kupitia bandari kwa mwaka ni tani ngapi kwa kila mmoja?
 
Huo mzigo uliogunduliwa Congo ni mwingi sana miaka mingi mno. Na thamani ya cobalt imepanda kwa kuwa inatumika kwenye vifaa vyote vya umeme. Pia kutengenezea betri za lithium ion za magari ya umeme. Kwa hiyo mzigo wa cobalt ulipo Katanga congo ni mwingi sana. Pia bado kuna mzigo wa Copper kama wote huko Congo miaka mingi mno.
Nchi husika zitajenga Barabara na reli zao kutoka migodi ni Kuja mpakani na tz na tz itajenga Barabara Kuja Tabora iliko bandari
 
Kwa nini? Inatakiwa tuwe na treni kila mahali, hili kuzuia uaribifu wa barabara zetu. Kuna vitu vingine vya kuzuia. Bwawa la Nyerere, Daraja lq busisi. Madaraja ya kupishania magari nk..
Kila mjinga leo anatoa ushauri wa kichekesho.
 
Nchi husika zitajenga Barabara na reli zao kutoka migodi ni Kuja mpakani na tz na tz itajenga Barabara Kuja Tabora iliko bandari

Soma hapo. Yaani Madini yanatoka Drc mpaka afrika ya kusini chanzo ni changamoto ya bandari
 
Ni hujuma tu na usimamizi mbovu. Hiyo reli ya Tazara mchina aliijenga ili achukue copper ya zambia apeleke kwenye viwanda vya china. Na ndio maana wachina wanaviwanda vya vifaa vya umeme. Ni hujuma tu. Ila tukiwa na SGR inayopita karibu na migodi ya Copper na Cobalt ya Zambia na DRC congo halafu hiyo reli ikasimamiwa vizuri mizigo mingi mno itapita kwenye reli na pesa itarudi.

..lakini reli ya Tazara imefika mpaka Kapiri Mposhi Zambia.

..Na hapo Kapiri Mposhi Tazara inaungana na reli inayotoa Copper Belt ambayo inafika ktk mpaka wa Zambia na DRC.

..jambo la msingi ni kuwa na reli, masuala ya GAUGE ni secondary.

NB:

..Standard Gauge Rail / SGR ni 1435 mm.

..Cape Gauge Rail / Tazara ni 1067 mm.

..Meter Gauge Rail / reli ya kati ni 1000 mm.
 
Hela hatuna, tusikope sana ili kupunguza kutumia na madeni.

Tabora ni karibu sana na Burundi, Rwanda, DRC, Mwanza na Uganda. Tujenge bandari kavu kuubwa pale Tabora ili watu wa Mwanza, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na Kigoma wachukulie Tabora mizigo yao itakayoletwa na SGR hapo.

Tukipata faida hapo tutaendelea na ujenzi hadi Mwanza, Burundi Rwanda na DRC kama tulivyokuwa tumepanga.

Hii itasaidia kuepuka uharibifu wa barabara kutoka dar hadi Tabora lakini na kupunguza umbali na gharama kwa watu wa DRC, Rwanda, Burundi kufuata bidhaa zao Dsm.
Utekelezaji wa huu mradi umekuwa wa kisiasa. Ndio maana wameenda kujenga kipande cha mwisho kinachoenda mwanza kabla ya kujenga cha katikati.
#KatibaMpya
 
..lakini reli ya Tazara imefika mpaka Kapiri Mposhi Zambia.

..Na hapo Kapiri Mposhi Tazara inaungana na reli inayotoa Copper Belt ambayo inafika ktk mpaka wa Zambia na DRC.

..jambo la msingi ni kuwa na reli, masuala ya GAUGE ni secondary.

NB:

..Standard Gauge Rail / SGR ni 1435 mm.

..Cape Gauge Rail / Tazara ni 1067 mm.

..Meter Gauge Rail / reli ya kati ni 1000 mm.
Mizigo mingi inapita Africa kusini kutokana na efficiency ya Bandari zao. Pia Angola wanataka kujenga reli kutoka Katanga Congo kupitia Zambia copper belt kuelekea bandari ya Angola(port Lobito) kwa hiyo bado kuna ushindani toka Angola unakuja.
 
Hela hatuna, tusikope sana ili kupunguza kutumia na madeni.

Tabora ni karibu sana na Burundi, Rwanda, DRC, Mwanza na Uganda. Tujenge bandari kavu kuubwa pale Tabora ili watu wa Mwanza, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na Kigoma wachukulie Tabora mizigo yao itakayoletwa na SGR hapo.

Tukipata faida hapo tutaendelea na ujenzi hadi Mwanza, Burundi Rwanda na DRC kama tulivyokuwa tumepanga.

Hii itasaidia kuepuka uharibifu wa barabara kutoka dar hadi Tabora lakini na kupunguza umbali na gharama kwa watu wa DRC, Rwanda, Burundi kufuata bidhaa zao Dsm.

Akili ndogo inajadili mambo makubwa. Rubbish
 
Hivi Hizi chuki na watu wa Kanda zinawanufaisha nn enyi nyie kizazi cha Nyoka, mnahisi kabisa Chadema Kuna siku itashika dola anyway labda Corona iue watanzania wote abaki Mbowe na genge lake.
 
Mizigo mingi inapita Africa kusini kutokana na efficiency ya Bandari zao. Pia Angola wanataka kujenga reli kutoka Katanga Congo kupitia Zambia copper belt kuelekea bandari ya Angola(port Lobito) kwa hiyo bado kuna ushindani toka Angola unakuja.

..Thank you!!

..Nashukuru umeitaja Angola na ushindani inaouleta.
 
Mradi wa sgr umetutia madeni. Halafu mradi ukikamilika utatutia madeni zaidi. Pia ramani ya mradi imekosewa. Reli ya sgr inatakiwa iende sehemu ya mizigo mingi. Na mizigo mingi ni shaba ya Zambia, na madini ya cobalt na shaba yaliyopo Lubumbashi/kolwezi/katanga DR Congo.

Sasa hii reli naona imepotea uelekeo wa mizigo mingi mno kwa hiyo haitarudisha hela. Kwa hiyo ni madeni juu ya madeni halafu riba. Mizigo mingi ipo kusini kwa Congo na Zambia. Halafu reli inaelekea mashariki mwa Congo

Hao Rwanda na Burundi hawana mzigo wa maana kuzidi Zambia na Cobalt na Copper ya Drc congo. Ilitakiwa SGR iende kwenye mizigo ya maana huko kwenye migodi ya zambia na Congo.

Hii sgr inayojengwa imekosewa kabisa. SGR ilitakiwa iwe Dar-Kapirimposhi-Lubumbashi(ikiwezekana ipite kwenye migodi ya Copper na Cobalt iliyopo Kolwezi, Mutanda huko Drc ndanindani)
Well said
 
Zambia Wana options za kutumia bandari za msumbiji Na South Africa. Hii Reli ilitakiwa iende kigoma kabla ya mwanza, nadhani imepelekwa Mwanza kimakosa. Hii SGR hata ingeishia morogoro na kujenga bandari kubwa sana ya nchi kavu pale morogoro bado tungewapunguzia safari wateja wetu Kuja hadi Dsm.

Wangejenga bandari kavu afu ikapigwa high way moja kutoka dar to maeneo potential. Nafikiri leo tungekua tushamalizana na gharama zingekua kubwa kiasi hiki
 
Mradi wa sgr umetutia madeni. Halafu mradi ukikamilika utatutia madeni zaidi. Pia ramani ya mradi imekosewa. Reli ya sgr inatakiwa iende sehemu ya mizigo mingi. Na mizigo mingi ni shaba ya Zambia, na madini ya cobalt na shaba yaliyopo Lubumbashi/kolwezi/katanga DR Congo.

Sasa hii reli naona imepotea uelekeo wa mizigo mingi mno kwa hiyo haitarudisha hela. Kwa hiyo ni madeni juu ya madeni halafu riba. Mizigo mingi ipo kusini kwa Congo na Zambia. Halafu reli inaelekea mashariki mwa Congo

Hao Rwanda na Burundi hawana mzigo wa maana kuzidi Zambia na Cobalt na Copper ya Drc congo. Ilitakiwa SGR iende kwenye mizigo ya maana huko kwenye migodi ya zambia na Congo.

Hii sgr inayojengwa imekosewa kabisa. SGR ilitakiwa iwe Dar-Kapirimposhi-Lubumbashi(ikiwezekana ipite kwenye migodi ya Copper na Cobalt iliyopo Kolwezi, Mutanda huko Drc ndanindani)
SGR inakwenda kuwasaidia Wapiga Kura Mwanza. Full stop!
 
Tungekuja na wazo la ujenzi wa reli fupi ya kutoa makontena toka bandari hadi depot nyingine mfano chalinze. Tunajenga high ways njia zote potential zinazo pitisha mizigo mingi kutoka eneo la depot.

Leo tusingekua tunakolomeana kuhusu madeni mengi mengi
 
Back
Top Bottom