Ujenzi wa Reli ya SGR uishie Tabora

Siku hayo Madini ya copper na cobalt yakiisha au kupungua ardhini huko zambia utahamisha mataruma?
Huo mzigo uliogunduliwa Congo ni mwingi sana miaka mingi mno. Na thamani ya cobalt imepanda kwa kuwa inatumika kwenye vifaa vyote vya umeme. Pia kutengenezea betri za lithium ion za magari ya umeme. Kwa hiyo mzigo wa cobalt ulipo Katanga congo ni mwingi sana. Pia bado kuna mzigo wa Copper kama wote huko Congo miaka mingi mno.
 
Aisee yaani tumekula hasara kizembe mizigo mingi mno ipo Zambia na Congo.
 
Barabara na reli ya kawaida akutoka Tabora ingetosha kuhudumia mizigo ya a mwanza na uganda. Ushamba tu.
 
Kwani hii reli ya Sasa wameifanya Nini Hadi wanakazaka kuwapa waturuki pesa?
Unategemea mafisadi wenye malori zaidi ya elfu moja watakubali SGR ikamilike? Wenye malori zaidi ya 599 Ni watu wenye connection na high places.
Mimi na suggest hizo hela wangezitumie kuleta maji Dar es Salaam. Hivi tunavyoongea 29/12/2021 hakuna maji tangu Jana jioni. Umeme ndio huu wa kuunga unga vijana wa welding hawalali maana hawajui Kama kesho kutakua na pawa.
Tatueni kero za wananchi SGR sio kipaumbele kwa sisi watu wa Kimara.
 
Zambia ndio wameuza nchi yao kwa wachina. Kumbuka mambo huenda yakibadilika. Rwanda na Burundi utaziona mzigo wake reli itakapokamilika.

Hii tabia ya kulalamika haitufikishi popote, zaidi ya kujionyesha namna gani tusivyo na ubunifu vichwani.
Mzigo wa Rwanda, Congo DRC, na Zambia unaoingia kupitia bandari kwa mwaka ni tani ngapi kwa kila mmoja?
 
Nchi husika zitajenga Barabara na reli zao kutoka migodi ni Kuja mpakani na tz na tz itajenga Barabara Kuja Tabora iliko bandari
 
Kwa nini? Inatakiwa tuwe na treni kila mahali, hili kuzuia uaribifu wa barabara zetu. Kuna vitu vingine vya kuzuia. Bwawa la Nyerere, Daraja lq busisi. Madaraja ya kupishania magari nk..
Kila mjinga leo anatoa ushauri wa kichekesho.
 
Nchi husika zitajenga Barabara na reli zao kutoka migodi ni Kuja mpakani na tz na tz itajenga Barabara Kuja Tabora iliko bandari







Soma hapo. Yaani Madini yanatoka Drc mpaka afrika ya kusini chanzo ni changamoto ya bandari
 

..lakini reli ya Tazara imefika mpaka Kapiri Mposhi Zambia.

..Na hapo Kapiri Mposhi Tazara inaungana na reli inayotoa Copper Belt ambayo inafika ktk mpaka wa Zambia na DRC.

..jambo la msingi ni kuwa na reli, masuala ya GAUGE ni secondary.

NB:

..Standard Gauge Rail / SGR ni 1435 mm.

..Cape Gauge Rail / Tazara ni 1067 mm.

..Meter Gauge Rail / reli ya kati ni 1000 mm.
 
Utekelezaji wa huu mradi umekuwa wa kisiasa. Ndio maana wameenda kujenga kipande cha mwisho kinachoenda mwanza kabla ya kujenga cha katikati.
#KatibaMpya
 
Mizigo mingi inapita Africa kusini kutokana na efficiency ya Bandari zao. Pia Angola wanataka kujenga reli kutoka Katanga Congo kupitia Zambia copper belt kuelekea bandari ya Angola(port Lobito) kwa hiyo bado kuna ushindani toka Angola unakuja.
 

Akili ndogo inajadili mambo makubwa. Rubbish
 
Hivi Hizi chuki na watu wa Kanda zinawanufaisha nn enyi nyie kizazi cha Nyoka, mnahisi kabisa Chadema Kuna siku itashika dola anyway labda Corona iue watanzania wote abaki Mbowe na genge lake.
 
Mizigo mingi inapita Africa kusini kutokana na efficiency ya Bandari zao. Pia Angola wanataka kujenga reli kutoka Katanga Congo kupitia Zambia copper belt kuelekea bandari ya Angola(port Lobito) kwa hiyo bado kuna ushindani toka Angola unakuja.

..Thank you!!

..Nashukuru umeitaja Angola na ushindani inaouleta.
 
Well said
 

Wangejenga bandari kavu afu ikapigwa high way moja kutoka dar to maeneo potential. Nafikiri leo tungekua tushamalizana na gharama zingekua kubwa kiasi hiki
 
SGR inakwenda kuwasaidia Wapiga Kura Mwanza. Full stop!
 
Tungekuja na wazo la ujenzi wa reli fupi ya kutoa makontena toka bandari hadi depot nyingine mfano chalinze. Tunajenga high ways njia zote potential zinazo pitisha mizigo mingi kutoka eneo la depot.

Leo tusingekua tunakolomeana kuhusu madeni mengi mengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…