Ujenzi wa Uwanja wa Mpira Dodoma kwa msaada wa Mfalme wa Morocco umeishia wapi?

Mkuu kwani pale Dodoma tulitaka kujenga kwa pesa zetu?
Unaweza kumpangia cha kufanya yule anayekuja kukusaidia?
Mfalme mwenyewe (baada ya kufurahi) aliaahidi kutujengea buree uwanja mkubwa wa kisasa pale Dodoma.
Waswahili na msemo wetu
Ahadi ni Deni ila naona alitoa ila waizi wakaweka mifukoni
Au walimpiga Mfalme na ile miradi hewa wakasema leta asilimia kadhaa tuanze nazo wakauchuna na hataki kutusikia kabisa

Yaani ukweli utakuja kujulikana siku moja
 
Vipi maulid, ulikuwa upande gani katika munaqasha wa Mombasa, wanaoipinga au wanaoiunga mkono?
Sina upande, mimi ni Muislam. Wote wale wanajitahidi kwa namna yao na sina tatizo na wote.

Unafahamu walichokuwa wanabishana ni kipi? Maana naona umeitaja "Maulid" mimi nimeuona huo mnakasha, sikuona kuwa pale walikuwa wanapingana kuhusu Maulid. Rudia kuutazama.
 
karibu kwenye Uislam, siku ya kwanza utayoingia kwenye Uislam utaanza kuihisi raha yake.
Nijibu kwanza sababu za kitabu chenu kuandika kuwa jua unazama kwenye matope.


Sura ya Al-Kahf (Sura ya 18) verse 86


"حَتَّىٰ إِذَا بَلَغَ مَغْرِبَ الشَّمْسِ وَجَدَهَا تَغْرُبُ فِي عَيْنٍ حَمِئَةٍ وَوَجَدَ عِندَهَا قَوْمًا ۗ قُلْنَا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِمَّا أَن تُعَذِّبَ وَإِمَّا أَن تَتَّخِذَ فِيهِمْ حُسْنًا"

Nipe jibu
 
Tanzania haijali vipaumbele vya kwanza ambacho ni kuondoa Umasikini kwanza, ukiondoa umasikini wananchi wanajenga wenyewe hivyo viwanja.
Mfalme aliahidi kujenga kiwanja, sio pesa za serikali.
 
Wahuni Tu
Wahuni waliokula advance
Maana palitayarishwa kijengwe sehemu Inaitwa Nala njia kuelekea Singida mara puu Nzuguni kuelekea Moro

Mfadhili machale yakamcheza

Hapo nani Muhuni?!!

Bongo Nyoso hamfai kuanzia juu mpakabalozi wa mtaa na wananzego wote vicheche

Kilamtu anakula Kwa Urefu wa kamba yake
 
Mfalme wa Morocco hawezi tena kujenga kiwanja cha mpira maana nchi yake imekumbwa na tetemeko lililosababisha vifo vya maelefu ya wananchi na miundo mbinu kuharibiwa vibaya sana.

Walioko madarakani sasa hivi wanaelekeza nguvu nyingi Dar Es Salaam badala ya kuhakikisha kwanza Dodoma umekaa swa katika kila mahitaji ya miundo mbinu ya viwanja vya mpira, ndege, barabara, mashule, hospitali, na huduma zingine za kijamii zikidhi mahitaji na kushawishi mabalozi kuhamia huko ambako JPM aliwapa vinja vilivyopimwa bure.
 
Ilikuwa ahadi wakati wa vita ya kiuchumi,kwasasa vita hamna tena so ile ahadi imekufa
 
Wakati wa utawala wa magufuli nakumbuka tulitangaziwa kuwa mfalme wa morrocco atatujengea uwanja mkubwa wa mpira mkoa wa dodoma sijui ile ishu iliishia wapi...
Huenda ahadi ilitimizwa ila kuna wahuni waligawana mapato ya ahadi baada ya Magufuli kupumzika kwa amani.

Kwa sasa wapigaji wapo mstari wa mbele kula kwa urefu wa kamba zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…