Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Dodoma(Dodoma Stadium) kuanza hivi karibuni

Naona sawa wangeupeleka kule Nala tu Bs nilisikia stand Stand ya bus za mwanza nayo inaenda kule..
Mzee kule watu walishaweka mitegesho. Jamaa walinunua mashamba ili serikali iwalipe pesa nyingi.
 
Dom patakuwa patamu sana baada ya muda mfupi.....nahitaji kiwanja low density nala kilichopimwa
 
Hii habari naitilia shaka sana, hiki kiwanja ni cha olympic ujerumani, jaribu ku google "olympic stadium german"
 
Ramani za uwanja wenyewe zipo wapi, maana hiyo picha sio ya huo uwanja unaotarajiwa kujengwa
 
Binafsi naukaribisha kwa mikono miwili huo uwanja! Lakini kama suala ni kuomba, hivi hatukua na cha maana zaidi cha kuomba badala ya uwanja wa mpira?! Unless kama Mfalme mwenyewe alitaka kutoa msaada kwenye uwanja wa michezo kinyume chake, natamani hizo takribani 200 billion zingeenda kwenye changamoto zinazoathiri maisha ya mwananchi wa kawaida moja kwa moja!!

Nasikia Dodoma kuna changamoto ya maji kweli kweli... na hili taifa linalohamia huko hiyo changamoto si itakuwa maradufu?! Dodoma wana shule za kutosha kukabiliana na migration ya watu kutoka Dar na maeneo mengine ya nchi?!

Wakati Uwanja wa Taifa unafunguliwa tulikuwa tunadanganyana soka letu litapanda lakini ndo kwanza Mnyama ambae mpira ushamshinda ndo kwanza anakimbilia FIFA kuomba pointi za mezani baada ya kuomba zingine za mezani mwaka 2011 dhidi ya TP Mazembe 😀😀😀😀😀😀!!!!
 
Rais atasimamia mwenyewe!! What a shame... Hiyo ni kazi za rais.. Mbona huyu bwana hajitambui.. Kila kitu ufanye wewe..???
 
ACHENI UPOTOSHAJI UWANJA WA UJERUMANI HUU WA OLYMPIC... Weka picha halisi za mchoro wa uwanja kaka.

 

Wabunge pingeni kujengwa kwa Daraja la Juu ya Bahari kutoka Coco Beach-Agakhan
figganigga kuna siku unaamka vizuri sana na mawazo murua
ulipinga sana Daraja la Coco beach hasi Agha Khan linalojengwa na mkorea Kusini na hapa unasupport kiwanja chenye nakala ya Mjerumani kujengwa na mMorocco kwa kasi

Vyote ni misaada na je? tunaangalia manufaa
  • Coco Beach - Agha Khan barabara utapitika kila siku na itapunguza msongamano kwa magari yote kukatika katikati ya Juju la Dar
  • Kiwanja cha Nzuguni, hakitatumika kwa Mechi zozote kwani Dodoma hakuna Timu iliyo daraja la kwanza, Ligi Kuu au Kombe la FA
    • Shereha za Muungano, Mei mosi na Uhuru ndizo zinaweza kufanyika tu
    • Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu si riadha wala mpira ambao leo wanashtakiana moaka ngazi za juu kwa ajili ya kadi ya njano
    • Uwanja mkubwa kama huo wa Ujerumani kwa idadi ya leo ya wakazi wa Dodoma ni asante kubwa sana tutaingia labda waje Simba na Yanga
figganigga kwa kutafakari hii misaada mingine mm naona kubali kwanza Daraja halafu Kiwanja tutaenda sawa
 
Ha ha magufuli si alisema nchi tajiri sana why.tunaombaomba viwanja tena kwa waarabu wa Morocco sizonje ana maigizo ila. Sio mbaya aisee
Kwahiyo wewe kilichokuwasha ni kusikia kua huo msaada unatolewa na waarabu wa Morocco?

Ingekua mzungu ndio anatoa huo msaada wewe ungeona ni sawa sio?

Acha kua na mawazo mgando wewe kutwa kuwaza ubaguzi tu.
 
Achebi uongo nyinyi huo uwanja mbn ni wa ujeruman
 
Ni hali halisi ya utindio wa kizalendo kutotambua mahitaji halisi ya wananchi chini ya uongozi husika ambayo yanahitaji suluhisho litakalodumu hata miaka 20 tu kuwafanya wawe wenye neema milele!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…