Mradi wowote ili ufanikiwe inabidi uwashirikishe wanufaika ambapo katika huu uwanja ni wakazi wa Dodoma kwa upana zaidi na wengineo ambao sio permanent residents wa hapo. Ukiangalia madi huu Dodoma ni kama wanapelekewa 'maendeleo' ambao walipaswa kuyajadili wenyewe na kuyaomba au kuyatekeleza. Matokeo yake huenda yakawa si mazuri, mfano kama uwanja wa Tabora ambao pamoja na kujengwa zamani lakini hadi leo haujakamilika na matumizi yake sio kama viwanja vingine.
Kufanya maamuzi kisiasa ni vizuri lakini inakuwa mbaya pale vision inaposhia miaka mitano ya uchaguzi, ingelikuwa kuna mwenye vision nje ya ccm, cuf, cdm nk hivyo kuiona Dodoma ya miaka 50 au 100 ijayo angapendekeza uwanja simple tu wenye capacity ya 20,000-30,000 ya watazamaji. Kumbuka idadi ya watu dodoma ni chini ya 500,000 na mwenye ndoto kwamba mji utakua na kuwa na wakazi 3,000,000 basi wakati huo nchi ya Tanzania kwa ujumla itakuwa na watu milioni 500! Sijui itakuwaje wakati huo maana hawa 50 milioni wa sasa nusu yetu tunaishi chi ya $1 na hatujui kusoma na kuandika!!!
Nasikiaga wanaofikiri kwa umakini wakiita miradi kama hii 'white elephants' japo sielewagi maana yake.