Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amezitaka nchi za NATO kuipa silaha Ukraine ili ishambulie ndani ya mipaka ya Russia hasa military targets.
Mpango huu umekuja baada ya Ukraine kutembezewa kichapo cha kutosha kutoka kwa Russia na majeshi ya Russia kuzidi kusonga mbele kuelekea mji muhimu wa Kharkiv.
Ila baadhi ya washirika wa NATO kama Ujerumani na Italy hawajaunga mkono wazo hilo.
Chancellor wa Ujerumani Olaf Scholz, Waziri wa Mambo ya nje wa Italy, Antonio Tajani na makamu wa waziri mkuu wa Italy, Matteo Salvini wameonyesha msimamo wa nchi zao kwa kukutaa.
Scholz: "Hatupaswi kupiga ndani ya Urusi ili kuepusha vita kubwa."
Tajani: "Hatutatuma mwanajeshi hata mmoja wa Kiitaliano nchini Ukraine, na vifaa vya kijeshi ambavyo Italia hutuma vinapaswa kutumika katika eneo la Ukraine."
Salvini: "Tunatafuta amani, sio utangulizi wa Vita vya Kidunia vya Tatu."
Nini kinaendelea katika mataifa ya Ulaya?
Kuhusu Netanyahu mataifa ya Ujerumani na Ufaransa yalikubaliana na waraka wa ICC kuhusu kukamatwa kwa Netanyahu.
Norway, Spain na Ireland zimeitambua Palestine as a state.
Acha tuupe muda nafasi.