Ujerumani yaiomba msamaha Namibia kwa mauaji ya kimbari

Ujerumani mapema Ijumaa imefikia makubaliano na Namibia kwamba inatambua rasmi mauaji yaliyotokea wakati wa ukoloni yalikuwa ya kimbari.

Kauli hiyo imetolewa wakati taifa hilo likitangaza kutumia dola bilioni 1.3 moja kwenye miradi ya maendeleo nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, makubaliano hayo yamefikiwa baada ya mashauriano yaliochukua zaidi ya miaka 5 kati ya Namibia na Ujerumani.

Mashauriano hayo yalijikita katika ukatili uliyofanyika kati ya mwaka wa 1904 - 1908 wakati taifa hilo likiwa chini ya ukoloni wa Ujerumani.

Wanahistoria wanasema Jenerali Lothar von Trotha alitumwa na Ujerumani kwenye taifa hilo lililojulakana kama German West Afrika ili kuzima uasi kutoka kwa watu wa kabila la Herero mwaka 1904.

Badala yake Trotha inasemekana kuamuru kutokomezwa kwa kabila hilo lote.

Inasemekana kuwa takriban watu 65,000 kutoka kabila la Herero waliuawa pamoja na wengine 10,000 kutoka kabila la Nama.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema kuwa wameomba msamaha kwa Namibia pamoja na watu wake.

Chanzo:
VOA Habari (28, Mei 2021)
 

Na Tanganyika iiombe msamaha Zanzibar kwa iliyoyafanya Tokea 1964 mpaka leo
 
Wakitoka waje na Tanganyika, huku Afrika Mashariki ndiko walipoharibu na kufanya mauaji zaidi kupitia German East Africa Company (GEAC)

Kwanza wawalipe vitukuu na vilembwe vya familia ya Mkwawa na Kinjekitile Ngwale kabla sijamtajia familia zingine.
 
Duh niliskia bwana mmoja anasema kule Zanzibar kuna watu wameamua kumtoa mwarabu kwenye uovu wa uuaji na utumwa alioufanya, Leo wanamsafisha Ni msafi Hana doa. Eti mwarabu alikuja kueneza uislamu tu. La hasha. Mungu awahurumie na dhambi hii. Kinyume chake wanajaribu kumfanya mwingereza , mreno, na mfaransa kuwa katili wa kutupwa. Ajabu!
Sibishi kuwa wazungu pia Ni wakatili Sana lakini hili halifichi uhalisia wa kilichofanywa na waarabu kwa Karne nyingi. Wao ndio waliowafanya wapwani na wabara watumwa. Wale waliofika arabuni wakahasiwa kutoleta uchotara ndani ya uarabu. Huku Afrika wakaoa, wakabaka hakuna aliyeongea.
Baba angu alinambia siku moja namna baba yake alivyoshurutishwa kwenda Tanga kwa miguu . Akapigwa Sana akafa akiwa kiziwi kwa kipigo. Kipindi hicho utumwa ulipoa kidogo lakini waliathirika.
Nb.
Utumwa ulifika kote kuanzia Zanzibar. Dodoma, Tabora bagamoyo mpaka Tanga nk.
 
Na waarabu ni watakatifu sio. Wale waliokuwa wanafungwa minyororo visiwani Unguja na Pemba yalifanywa na waswahili?
Umewaona wapi au umeona yale masanamu, kama masanamu yamejengwa na nani? Je yale masanamu yalikueko kabla ya mapinduzi, acheni undezi na history yenu potofu
 
Usisikitike ndugu,Mbuzi ukimpigia gitaa usitegemee acheze utapoteza mda na Nguvu zako buree.imenenwa Waache wafu wazike wafu wao.
 
Kmmk sasa wanamuachaje Namibia ili afute machozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…