Ujerumani yaipa Tanzania msaada wa Tsh. Bilioni 56.3 kuboresha Haki za Binadamu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, imetia saini ya Mkataba huo kupitia Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Fedha zitakazotumika kwaajili ya kugharamia maeneo Manne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Tsh. Bilioni 8.15 zitafadhili Programu ya Haki za Binadamu na Usawa wa Kijinsia, Tsh. Bilioni 8.15 zitaimarisha Upatikanaji wa Maji na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi Zanzibar katika maeneo ya Mijini.

Kiasi kingine cha Tsh. Bilioni Bilioni 10.8 kitatumika katika Usimamizi Bora wa Fedha za Umma na Tsh. Bilioni 32. 6 zitaenda kwenye Programu ya uboreshaji wa huduma za Afya.
 
Misaada hii ingetumika kujenga viwanda au kumaliza SGR au kulipa madeni ya walimu au kuboresha vyuo vya Amali mambo yangekuwa mazuri sana
 
Haki za binadam tuishe hapo wangefunguja tu dhumuni LA huo mkwanjaaa ......sis wengine ilo fungu halituhusu......walengwa
Haki .za...magasho...
Hak...za wakoboaji....
 
Serikali kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, imetia saini ya Mkataba huo kupitia Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Fedha zitakazotumika kwaajili ya kugharamia maeneo Manne.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Tsh. Bilioni 8.15 zitafadhili Programu ya Haki za Binadamu na Usawa wa Kijinsia, Tsh. Bilioni 8.15 zitaimarisha Upatikanaji wa Maji na Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi Zanzibar katika maeneo ya Mijini.

Kiasi kingine cha Tsh. Bilioni Bilioni 10.8 kitatumika katika Usimamizi Bora wa Fedha za Umma na Tsh. Bilioni 32. 6 zitaenda kwenye Programu ya uboreshaji wa huduma za Afya.
Kuna Afya,haki za binadamu na ufuatiliaji
 
Hapo kwenye haki za binadamu hapo.....binadamu wenyewe ndio kina aggrey sasa
 
Ndio maana ya kuomarisha mifumo hivyo unawaimarika hao rasilimali watu.

Wewe inakuuma nini wakati ni Kodi za Wajerumani?
Asubiri kodi yake iwalipe wake wa viongozi wa nchi yake ambao wamekula kodi za Wajerumani [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom