Mtanga90
JF-Expert Member
- Nov 18, 2022
- 238
- 460
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Anna Baerbock amesema "hatoizuia " Poland ikiwa itatuma vifaru vya Leopard 2 nchini Ukraine.
Ukraine imetoa wito kwa nchi za Magharibi kutoa vilivyotengezwa na Ujerumani ambavyo wanasema ivtawasaidia kuishinda Urusi.
Lakini Ujerumani bado haijatoa magari ya kivita, na sheria zake za usafirishaji wa silaha zinazuia nchi zingine kutuma zao.
Siku ya Jumapili, Bi Baerbock alisema Poland ilikuwa bado haijaomba ruhusa ya kuuza silaha hiyo nje.
"Kwa sasa swali halijaulizwa, lakini ikiwa tungeulizwa hatatuzuia ," aliiambia LCI TV ya Ufaransa Jumapili.
Wiki iliyopita, waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alisema nchi hiyo iko tayari kutoa vifaru 14 ya Leopard 2 kwa Kyiv ikiwa Berlin itawaruhusu kufanya hivyo.
"Uwezo wa kutetea uhuru nchini Ukraine unaweza kutegemea hilo," alisema.
Vifaru vya Leopard 2 viliundwa mahsusi kushindana na vifaru vya Urusi T-90, ambavyo vinatumika katika uvamizi.
Inaaminika kuna zaidi ya 2,000 duniani kote na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema takriban 300 kati yavyo vitasaidia kuhakikisha kushindwa kwa Urusi.
Nchi nyingi washirika zimechanganyikiwa na Ujerumani kwa kusita kwake kutuma vifaru vyake vya Leopard 2.
Chini ya kanuni za sasa, Ujerumani lazima pia iidhinishe usafirishaji wowote wa vifaru vyake na nchi zingine, kama vile Poland.
Kufuatia mkutano wa zaidi ya nchi washirika 50 siku ya Ijumaa, Ujerumani ilikuwa bado haijajitolea kusambaza vifaru hivyo wala kutoa leseni ya kuuza nje. Lakini ilikanusha kuzuia usafirishaji wa vifaru hivyo kwa upande mmoja.
Katika taarifa ya pamoja siku ya Jumamosi mawaziri wa mambo ya nje wa Estonia, Latvia na Lithuania waliiambia Ujerumani "kutoa vifaru vya Leopard kwa Ukraine sasa".
Kwa nini vifaru Leopard inahitajika sana?
Kifaru cha Leopard 2 ni silaha ya kiwango cha kimataifa inayotumiwa na zaidi ya nchi kumi na mbili.
Ukraine inaona kifaru hicho kama sehemu nyingine muhimu ya ulinzi wake dhidi ya vikosi vya Urusi na Leopards zimetumiwa kivita nchini Afghanistan na Syria.
Kinachowafanya zivutie zaidi Kyiv ni kwamba karibu theluthi mbili ya Leopards zote zinazozalishwa bado ziko Ulaya. Kwa hivyo kupata Leopards kwenye mapambano ni jambo la moja kwa moja. Hilo pia hurahisisha matengenezo na ukarabati - vipengele muhimu vya mfumo wowote wa silaha.
Inafaa kukumbukwa katika haya yote kwamba Ujerumani inaipa Ukraine mifumo muhimu ya ulinzi wa anga, kama vile IRIS-T na makombora ya kutoka ardhini hadi angani ya Patriot, pamoja na magari ya kubeba wanajeshi
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz hapo awali amekuwa na mashaka juu ya ushiriki wa Ujerumani katika mizozo ya kijeshi, na ana wasiwasi juu ya kuchochea mzozo huo na kuihamakisha Urusi .
Kansela huyo alikutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwishoni mwa juma kusisitiza muungano wa nchi hizo mbili baada ya vita.
Ufaransa tayari imejitolea kupeleka mizinga mepesi kwa Ukraine, na Bw Macron alipendekeza kuwa inawezekana kwamba mizinga mikubwa ya Leclerc iliyotengenezwa na Ufaransa inaweza pia kuwasilishwa Ukraine.
Nchi nyingine zimejitolea kutuma mizinga, ikiwa ni pamoja na Uingereza, ambayo itatuma Challenger 2 14.