Uji mzuri wa watoto wanaotakiwa kuanza kula, mchanganyiko mzuri ni upi?

Uji mzuri wa watoto wanaotakiwa kuanza kula, mchanganyiko mzuri ni upi?

Na kama sina microwave wala strainer, unanishauri nifanyeje.

Mdau35
Kama huna microwave chemsha maji kisha itumbukize kwenye maji kwa few minutes -lengo ni kuilainisha vizuri sio kuipika! Kama huna strainer iponde kwa kijiko, mwiko etc cha muhimu ilainike kabisa kumbuka ndio anaanza, tumbo lake halitamudu particles anaweza kupata shida ya choo.

Shukran
Annina
 
Mlo wa aina hii mtoto anatakiwa apatiwe mara ngapi kwa siku?
1,2,3 ???

FL
Kama ndio anaanza, mpatie mara 2.
Angalizo: jaribu kumpa chakula cha aina moja kwa angalau 3 -7 days ili uone kama kina reaction yeyote.

Tuendelee kubadilishana mawazo.

Annina
 
Mdau35
Kama huna microwave chemsha maji kisha itumbukize kwenye maji kwa few minutes -lengo ni kuilainisha vizuri sio kuipika! Kama huna strainer iponde kwa kijiko, mwiko etc cha muhimu ilainike kabisa kumbuka ndio anaanza, tumbo lake halitamudu particles anaweza kupata shida ya choo.

Shukran
Annina

Asante sana kwa maelezo na uahauri mzuri
 
FL
Kama ndio anaanza, mpatie mara 2.
Angalizo: jaribu kumpa chakula cha aina moja kwa angalau 3 -7 days ili uone kama kina reaction yeyote.

Tuendelee kubadilishana mawazo.

Annina

thanks Dear
Nimemwanzishia ya ndizi na maziwa naona anakula vizuri
 
dada Karucee mi nimepigwa butwaa kwenye hiyo ratio ya lishe halafu kupikwa kwa dakika 10?

Hata me nimeshtuka kwanza kitaalam wanashauri kutomchanganyia mtoto vitu vingi at once...sababu hujui ana allerge na nini...wanaanzaga na dona,then unadd karanga ,akiendelea kukua una add vingine taratibu huku ukiwa unamcheck mtoto...wengine wana allerge na vyakula vya protein kama maharage na allerge zipo za design nyingi kama acute resp attack unaweza mkosa mtoto ndani ya masaa...so ukipewa ushauri unachanganya na akili yako but muhimu zingatia balance diet at least mtoto apate protein,carb,fat,minerals na water kwa siku na si lazima vyote viwe kwenye uji...
 
Last edited by a moderator:
jaman hata mie nna twins wangu wako na 5 months hapa naumiza kichwa vyakula vya kuwapa,ntajaribu kuwaanzishia ya ndizi na avocado. mda gani ni mzuri kuwapa huo mchanaganyiko?
 
Huu mchanganyiko unakua na ladha gani?? Unalika??
Dagaa kwenye uji?? Lazima iwe na ladha isiyopita kooni..

Teh teh hizi lishe za kimasai hizi!! Wanaweka na maharage hahahaha!!
 
Mtizamo wangu mnawachosha watoto matumbo. Miezi 5 achanganyiwe mahindi, mtama, karanga, dagaa, ulezi, kunde, choroko?

Hilo tumbo changa linalojifunza kubeba vyakula vizito baada ya kuzoea maziwa tu litaweza?

No wonder watoto wanakataa kula, uji uwe na harufu ya dagaa?Ukute siku hiyo na haraka haraka hata hazijaiva.

Unga wa mahindi wa dona unatosha kabisa, ongeza maziwa, blue band, na sukari kidogo.

Hivyo vyakula vingine, mpe separately, unaweza kujifunza kutengeneza veg soups nyepesi, na apewe kwa ratiba ama siku tofauti tofauti.

Anyway, hii ni traditional way, mie hata uji wa ulezi tu simpi mtoto. Ya nini ahangaike kutaga?
 
Habari zenu wadau ni masiku mengi sijatia mguu ndani hapa ila leo naomba msaada ,
Ni mchanganyiko upi wa vyakula unaomfaa mtoto wa kuanzia miezi mitano.....
maana wengine wanasema
Dagaa,mahindi ,maharage ,karanga nk ni
mahindi ,soya ,karanga ,ulezi ,mtama nk nk
Mahindi ya bisi,uwele,ngano,karanga,soya nk nk
Kwa anayejua ni vitu vziuri vikichanganywa msaada tafadhari
wenu Mtiifu
FL1

Ningekushauri uanze na uji wa dona mwepesi mwepesi hadi akifika miezi kama 7 unaanza wa kuchanganya na nafaka nyingine, na uangalie usichanganye vitu vingi sana maana anaweza kupata allergy mtoto usijue ni kitu nafaka ipi haimfai.
Pia jaribu kuangalia unapo introduce new food kwa mtoto unampa for like 3 days huku unaangalia kama kinamletea madhara maana watoto wako so sensitive na vyakula vipya.
Visit wholesome baby food ( http://wholesomebabyfood.momtastic.com) upate kujua zaidi wakati wa kumuanzisha mtoto mboga mboga na vyakula vingine.
Enjoy your bundle of joy.
 
Yes, hiyo ndo lishe nampa mtoto wangu, na its the best kwani pia inamjengea imune system nzuri.

Ngano kg 5, (kaanga- Korosho 1/2kg, Kunde 1/2kg, Mbaazi1/2kg, Njugumawe 1/2) Ufuta1/2kg, Unga wa ubuyu1kg,) karafuu ya 1000/=, Iliki ya1000, . Usage alafu kupika ni dk10
Mamii ulipoanza kumpa huu mchanganyiko alikua ana umri gani?

Mwanangu hivi sasa ana umri wa mwaka mmoja karibu na mwezi. je huo mchanganyiko wamfaa maana hiyo karafuu naona kama ni kali sana.
 
Unabadilisha flavor kidogo ila usiweke vitu vingi kwa wakati waweza weka :
Mahindi, soya na ufuta.... Next time badala ya ufuta unaweka karanga
Mahindi, ngano na ulezi.... Ulezi unaweka kidogo make unaleta constipation
 
Mhh! Mbona hii lishe ndiyo naisikia leo. Karanga ni sawa na korosho.kunde,mbaazi,njugu ni jamii moja.
Ngano kg 5, (kaanga- Korosho 1/2kg, Kunde 1/2kg, Mbaazi1/2kg, Njugumawe 1/2) Ufuta1/2kg, Unga wa ubuyu1kg,) karafuu ya 1000/=, Iliki ya1000, . Usage alafu kupika ni dk10
 
Habari zenu wadau ni masiku mengi sijatia mguu ndani hapa ila leo naomba msaada.

Ni mchanganyiko upi wa vyakula unaomfaa mtoto wa kuanzia miezi mitano...

Maana wengine wanasema Dagaa, mahindi, maharage, karanga nk ni
mahindi, soya, karanga, ulezi, mtama n.k.
Mahindi ya bisi, uwele, ngano, karanga, soya n.k.

Kwa anayejua ni vitu vizuri vikichanganywa msaada tafadhari..

Wenu Mtiifu,
FL1.
saga mahindi na brown rice! huwa nawapa watoto wangu ivo! hali ikiwa ngumu kidogo maana brown rice ipo ghali kidogo...bas wanakunywa uji wa dona unachemka vizuri natia na maziwa! wanaupenda
 
Je ni sawa kuweka karanga,mchele,mhogo,ufuta,ulezi,mahindi ya lishe,soya,ngano katika uji wa lishe? Kuna mtoto wa mwaka mmoja alishaanza kunywa uji muda mrefu kidogo
 
Ngano kg 5, (kaanga- Korosho 1/2kg, Kunde 1/2kg, Mbaazi1, Njugumawe 1/2) Ufuta1/2kg, Unga wa ubuyu1kg,) karafuu ya 1000/=, Iliki ya1000, . Usage alafu kupika ni dk10
Ufuta na korosho hivyo vina mafuta, vikichanganywa na nafaka halafu vikae kwa muda mrefu vinatengeneza toxins. Usalama ni kutengenexa nafaka pekee, hivyo vyenye mafuta mf. Karanga, ufuta, au korosho weka unapochemsha huo uji tena viwekwe mwishoni, siyo unapoanza tu kukoroga uji. Haishauriwi mchanganyiko mwingi kwenye chakula cha mtoto.
 
Back
Top Bottom