Jana usiku kulikuwa na Tamasha pale Nairobi ambalo moja ya Wasanii walioalikwa kutumbuiza ni Wasanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz akisindikizwa na Zuchu huku Msanii mwingine akiwa Rayvanny.
Vurugu zilianza baada ya muda wa Diamond Platinumz kupanda stejini kufika ambapo Msanii wa Kenya Willy Paul Msafi kulazimisha kupanda stejini eti kwa kuwa yeye ni msanii wa Kenya hivyo anapaswa kupanda mwanzo kabla ya Diamond Platnumz, na akadai yeye kuwekwa wa mwisho baada ya Diamond Platnumz ni kuwadharau Wasanii wa Kenya. Willy Paul anadai kuwa kwa mujibu wa ratiba yeye alipaswa kumtangulia Diamond, na pia anadai ratiba ilibadilishwa na yeye kupangwa baada ya Diamond Platnumz jambo ambalo hakulitaka na kupelekea kuleta vurugu ya kugombania kupanda stejini.
Baada ya vurugu hizi vyanzo vinasema Meneja wa Diamond ambae ni Sallam SK alipiga simu na kutaka Msanii wake "Diamond" ahairishe show hiyo. Diamond na timu yake waliondoka eneo hilo mara moja na kwenda kuendelea na ratiba nyingine pale jijini Nairobi.
Willy Paul alipanda stejini, lakini hakuishia hapo alizua taharuki baada ya Dj kupiga wimbo wake wa "Mmh" ambao alimshirikisha Rayvanny. Baada ya wimbo huo kupigwa Willy Paul akamwambia DJ kwa ukali "Naomba uondoe hiyo Takataka" akimaanisha aache kipiga wimbo huo. Hii kauli ilionesha ni dharau kiasi gani Willy Paul alikuwa nayo kwa wasanii wa Tanzania.
Bado Willy Paul aliongea na media na kudai wasanii wa kenya wanadharauliwa hawapewi kipaumbele na pia amelalamika kuwa jina lake na picha yake kwenye bango la matangazo vimewekwa kwa udogo ukilinganisha na jina na picha ya Diamond, huku wasanii wengine kama Eric Omondi wakikazia kupitia machapisho yao ya Instagram kuwa wasanii wa Kenya wamekuwa wakidharaulika.
Tamasha la Furaha City Festival lilibadilika na kuwa tukio lenye drama nyingi, likitoa sio tu burudani za kuvutia bali pia ushindani mkali. Wakati mgongano kati ya Willy Paul na Diamond Platnumz ulikuwa tayari umeweka hali mbaya, msanii wa rap wa Kenya, Khaligraph Jones, alichukua mambo hadi kiwango kingine kwa matamshi yake ya kibaguzi.
Akiwa jukwaani, Khaligraph alitangaza sio tu kwamba yeye ndiye msanii bora wa rap barani Afrika, bali pia alijitawaza kuwa msanii bora nchini Tanzania—mbele ya Diamond Platnumz, ambaye kwa muda mrefu amehesabiwa kuwa mfalme wa muziki wa Tanzania. Kauli hiyo ya kishujaa iliwashangaza mashabiki, huku minong’ono ya kutokuamini ikitawala umati.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Khaligraph aliendeleza hali hiyo kwa kuimba wimbo wake wa diss unaojulikana kama "Bongo Flavour" dhidi ya marapa wa Tanzania, wimbo ambao alitoa miezi kadhaa iliyopita akiwatuhumu kwa “kusinzia kazini.”
MY TAKE:
Katika ukumbi huo wa burudani hapo jijini Nairobi wanekuwa wakiharikwa wasanii wengi kutoka Jamaica na Nigeria lakini hakujawahi kutokea vurugu ya namna hii, lakini baada ya wasanii wa Tanzania kutokea jana zikatokea vurugu hizo, na mpaka sasa mitandaoni wakenya wamesapoti kwa ukubwa kitendo cha vurugu alichokileta Willy Pau.
Huwezi kusikia hata kwa bahati mbaya Msanii au Mtanzania yoyote yule kutoa lugha za kibaguzi kama hizi kwa Majirani zetu Wakenya.
Wenzetu ile dhana ya kubaguana ipo kwenye damu zao,
Wao Kwa wao kutwa kubaguana kwa misingi ya Ukabila na mahali unapotoka.
Sasa baadhi yao kama huyu Mpuuzi anachochea hasira za Wakenya waone sisi ni Maadui zao!!
Huku kwetu Tanzania always tunawaona nyinyi ni ndugu zetu na tunawapenda sana.
Wanasiasa wetu wa Afrika Mashar
iki siku zote wanafikiria kuunganisha Mataifa yetu,
Lakini kijana mmoja wa hovyo kwa chuki zake binafsi anatoa lugha za kishamba shamba.
View attachment 3172093
View attachment 3172097