Ujinga wa Hamza usizalishe ujinga wa medani; yaliyotokea yasitufanye tukose weledi. Polisi imepoteza wapiganaji, familia ya Hamza imepoteza mtoto

Ujinga wa Hamza usizalishe ujinga wa medani; yaliyotokea yasitufanye tukose weledi. Polisi imepoteza wapiganaji, familia ya Hamza imepoteza mtoto

Uzi murua sana usiobagua upande.
Yapo makosa ya UWAJIBIKAJI na namna ya Kudai HAKI yako.
Kama namna ya kudai haki itakuwa kama ambavyo imetumiwa kama ipo basi
Law of the jungle ndio itatawala sisi sio wanyama.
Assume hakuwa na bastola , assume hana pesa wala uwezo wa kununua haki ingekuwaje?

Wapo wanaodhani kuwa majukumu waliopewa na wananchi ni kwa ajili ya kujinufaisha na kuyatumia madaraka yao vibaya. Hawa wanastahili KUWAJIBISHWA kma sio leo ni Kesho.

Mwisho tusishangilie mabaya, taifa limepoteza raia wake kwa kutowajibika kwao na wengine kwa kuonewa kabisa hawakuwa na hatia
 
Shida ya yote haya ni HAKI NA WAJIBU!

Tukilichambua tukio la mauaji ya HAMZA Linatupa taswira ya HAKI NA WAJIBU!

Hamza alikuwa ni mtu nzima mwenye familia yake( Huenda alikuwa level ya kutegemewa na si mtoto)

Kila mtu ana HAKI

Hamza kama kuna jambo lolote baya Aliona linamnyima HAKI yake hakutakiwa KUPANIKI! Angefikisha malalamiko yake ngazi husika ili atendewe HAKI! (Huo ndio uungwana)

Ukiporwa HAKI yako na watumishi wasio waaminifu haina maana ndiyo ufanye JINAI!

Makosa ya kunyimwa HAKI yapo kila mahali katika ofisi za Umma, Je, ni sawa kila mtu adai HAKI yake kwa nguvu ya mauaji?

Yaani mtu iwe busara mtu akifika TRA akiombwa Rushwa asipolizika basi achomoe bastola Apige afisa wa TRA

Au Mtu afike Tanesco akinyimwa umeme achomoe bastola apige!!!

Tukio la HAMZA lisitufanye tulaumiane! Lakini ni vyema likatukumbusha HAKI NA WAJIBU pande zote!

Weledi wa polisi ni kulichunguza tukio na kutoa report ya kitaalam wala hakuna haja ya kutoa vijembe na kashfa kwenye familia ya Hamza!

Mwili wa Hamza uheshimiwe kama miili mingine, wakabidhiwe familia kwa heshima ile ile ya ubinadamu!

Familia ya Hamza kwa upande wao, wanaona wamepoteza kijana shupavu, mtaftaji, Mme, baba wa watoto na mlezi wa familia iliyokuwa ina mtegemea!

Kosa la ndugu au mtoto lisiwe kashfa ya familia!
Isifikie mahali tukaaminishana kwamba Mtoto wa KAMANDA X akibaka huko mtaani basi tumulaumu baba yake KAMANDA!

Hata kama HAMZA alimtaja SIRRO Kwenye shambulio, IGP anatakiwa asipaniki!
Wachunguze kwanza kwa makini chanzo na ukweli wa tukio lile Hata kama litatia DOA baadhi ya watumishi kwa kutokutenda HAKI!
Ningekuona wa maana km ungekuja hapa na Ripoti inayoonyesha kuwa Hamza alikurupuka ktk maamuzi yake, tofauti na hapo wewe ni walewale wenye mawazo finyu ya akina Sirro.
 
Kuna wakati chuma cha mzungu ndo suluhisho sahihi.SASA HV WATAANZA KUOGOPA.
 
Back
Top Bottom