Ujinga wa Watanzania unavyofanya wanatapelewa mitandaoni Kila siku !!

Kama watu wanauziwa maji ya kilimanjaro na mafuta na udongo wanaambiwa ni vya baraka na huyo anaewauzia hazitaki hizo baraka zaodi ya sadaka zaka zako, hii ni hatua ya juu kabisa ya uzwazwa. Wabongo hawataki kuumizq kichwa kutafuta majibu ya maisha yao wao wameamua kuwaachia watu wafikirie kwa niaba yao. Waache wapigwe sana.
 
WABONGO MATAPELI, na vile tuna TCRA ya kudeal na Siasa tu, kunafanya MATAPELI haya, yanazi download video hizo mbalimbali.
 
Huyo mdada ulistahili kuchapa makofi aliporudi kwako baada ya kutapeliwa.
Ni mpumbavu Sana yule.
 
Ikiwa kama mpaka zama hizi watu wanauziwaeneo la bahati maji yakihama, watu wanauzuwa ahafi hewa hadharani na wanasiasa na wanazisubiria.
Dah! Nimekumbuka ule mradi wa Vanilla Village kule Njombe
 
Ikiwa kama mpaka zama hizi watu wanauziwaeneo la bahati maji yakihama, watu wanauzuwa ahafi hewa hadharani na wanasiasa na wanazisubiria.
Dah! Nimekumbuka ule mradi wa Vanilla Village kule Njombe
Uliishia wapi vile?
 
Mimi hua naagiza vitu China, kwa ajili yangu na rafiki zangu. Na hizo story za kutapeliwa nakutaka nazo Kila siku. Kuna wanaotapeliwa na watanzania na wanaotapeliwa na wakenya na wanaijeria. Changamoto ya kwanza ni bei nafuu sana, lazima uwe reasonable yaan iphone 15 uuziwe kwa laki 2 hata kama ni China hapana. Lakini wengine hawasomi hizi taarifa vizuri, hawaangalii location ya muuzaji, hizi platforms zinavutia mazungumzo ya pembeni nje ya platform lakini pia zinazuia malipo ya moja kwa moja kwenda kwa muuzaji kama Wire Transfer, M pesa au namba yoyote Ile ambayo muuzaji atapata Hela moja kwa moja. Lakini yote kwa yote, matapeli ndio watu wa kwanza kuifahamu biashara ya mtandaoni. Hivyo usinunue kwa mtu ambayr huna taarifa zake za kutosha, usilipie Hela ya mzigo ikiwa hujui gharama za usafiri za mzigo husika na utachukua muda Gani. Mwisho wewe mwenyewe unaweza kuagiza chochote unachotaka bila kumtumia mtu kati, Dunia inabadilika jifunze tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…