Ujio wa kocha mpya Simba SC hauna tofauti na kupika mchele wenye chuya

Ujio wa kocha mpya Simba SC hauna tofauti na kupika mchele wenye chuya

UONGOZI wa Simba unachapia nyufa badala ya KUJENGA ukuta, na hakika safari hii NYUMBA yenyewe imegoma na mafuriko ni mazito kiasi kwamba wakiendelea kukaza SHINGO basi tujiandae na mfuatano wa majanga...

Kufanikiwa kunahitaji kijikana kwakweli, hili linalotokea leo lilikuwa lazima lifike kwasababu klabu zetu zipo kwa ajili ya leo... Simba iko na uwanja Bunju miaka 10 inaenda lakini mpaka muda hakuna hata mtoto mmoja anayetokea pembeni ya uwanja hata wa kujua kudaka na tunaoyeshana Ndoto za mafanikio Afrika...

Haya kutengeneza cha kwetu tumeshindwa, sasa huko kununua nako tunabebana na sagula sagula za mwisho maana hata mtumba nao una grade zake, halafu tukishakusanyana na hayo magalasa tunayapamba kwenye magazeti ili kuhalalisha udhalimu wetu, halafu bila aibu TAJIRI tunamdanganya kuwa tumetumia Bilioni 3 kusajili [emoji1787][emoji1787][emoji1787], lakini ukichukua kalkuleta na peni Kila ukipiga hesabu huziona hizo Bil 3 zimeishia kwa nani?? [emoji23][emoji23][emoji23] Hapo MHINDI tushampiga kwa kumuuzia JUMBA LA UDONGO LILOCHAPWA PLASTA ambalo soon litavimba tu...

Na Sasa ndo limeanza kuvimba [emoji1787][emoji1787][emoji1787] maana wakati tunamwongezea MHINDI sifuri kwenye hesabu tunasahau kuwa mwisho wa siku yooote yanaishia uwanjani,,,, hapo ndo tunabaki na mazoea kuwa kwa "MKAPA HATOKI MTU" [emoji23][emoji23][emoji23].... huku chini ya VITI tunacheka tu [emoji23][emoji23][emoji23] tunasubiria dirisha dogo....
Wamechapia Nyufa Kama tunavyoona mkuu
 
Kiungwana kabisaa na kimichezo kuna Viongozi(wale walio mleta Manzoki wakati wa uchaguzi) wangetakiwa hadi muda huu wawe wamekabidhi ofisi kwa faida ya Simba.
Lakini ajabu bado wanashupaza shingo.
Kwanini nasema viongozi kwasababu ndiyo wahusika katika usajili kwa wachezaji na makocha
HATARI SANA SIMBA INATITIA KWENYE SHIMO LA HEWA
 
Tukumbushane.
 

Attachments

  • downloadfile-76.jpg
    downloadfile-76.jpg
    98.5 KB · Views: 3
KWANI ROBERTINHO ALIIHARIBU TIMU?!
FUKUZA FUKUZA YA MAKOCHA HUWA NI KUWAZUGA MASHABIKI TU
Simba Wana mpira wao ndio maana Robertino alikuwa akilalamikiwa sema timu ilikuwa inapata matokeo na viongozi walikuwa wakiwasapoti.
Mtu yeyote. Mwenye jicho la mpira alikuwa anajua Simba itakuja kipigo cha aibu, bahati mbaya ikawa na mtani.
 
Simba Wana mpira wao ndio maana Robertino alikuwa akilalamikiwa sema timu ilikuwa inapata matokeo na viongozi walikuwa wakiwasapoti.
Mtu yeyote. Mwenye jicho la mpira alikuwa anajua Simba itakuja kipigo cha aibu, bahati mbaya ikawa na mtani.
Sasa kwa menendo huu mbovu wa Simba sc analalamikiwa nani kocha au wachezaji?!
 
Back
Top Bottom