Hii PRECEDENT mbaya kabisa ya kutafuta nafasi ya urais miaka mitano kabla ilianzishwa na wanamtandao kwabahati mbaya ndoimeshakuwa njia inayotumika na wahuni wote sasa hivi hata katika ubunge na udiwani, na mbaya zaidi wanatumia njia ovu.
Hivi mtu anajipanga kutafuta urais miaka mitano kabla kwa kutumia kila aina ya mbinu, huyu mtu ni kweli anauchungu na nchi ? Ndomana wakiingia madarakani wanafanya ufisadi mkubwa kuiba mali za umma na kutumia nafasi zao kujineemesha kwasababu ndilo lilikuwa dhumuni kuu.
Hivi sasa mafisadi wamechukua open space karibu zote Dar es Salaam wanaweka miradi yao, mabandari ya nchi kavu imekuwa kero kwa raia kuharibu miundo mbinu katika wilaya ya Temeke. Hizi bandari kwanini zimeshamiri baada ya JPM kufariki? Kuna sehemu wamechukua eneo la TAZARA katikati ya reli na mapejengwa kwakusimamiwa na askari baada ya wananchi kukataa eneo lisichukuliwe. Hayo yalitokea miezi mitatu tu baada ya JPM kufariki.
Hawa wanamtandao wanapotupeleka sio sehemu salama kwaajili ya tamaa zao zisizo na msingi. Hivi inaingiaje akilini unachukua eneo la serikali alafu serikali inakuja kupangisha kwako wewe unalipwa, as if eneo lilikuwa la Baba yako? Kama kweli Bandari hawana eneo la kutosha la kuhifadhia makasha kwanini eneo hilo la tazara wasipewe Bandari?
Sasa hivi tunapoongea wameshachukua eneo la wizara ya kilimo hapo vetenali wameweka bandari zao. Magufuli alijua hizi bandari ni za mafisadi ndomana alizipiga chini zoote, bandari wakawa na maeneo yao. Baada ya kufariki wakarudi kwa kasi ya ajabu, mtu ukiwa na akili hili jambo linauma na linaleta hasira sana yaani mpaka presha inapanda, kwanini wanatufanyia hivi lakini????
Hakuna kitu kinanizidishia hasira sasahivi kuhusu hizi bandari zao huku temeke kama foleni ya malori na uharibifu wa barabara. Fanyeni ufisadi wenu wekeni mazingira sawa sasa watu tupite kwaamani kuliko hivi mnavyotufanyia, yaani ukitaka kumia gari sasa hivi barabara ya mandera haipitiki imejaa maroli. Siku nyingine mpaka huku uswahilini kwenye bandari zao. Dahh Mungu tusaidie kutuondolea hawa watu wasiojali maisha yetu wanajali ya kwao tu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.