Pre GE2025 Ujio wa Rais Samia Suluhu Hassan: Hadi sasa sijaona dalili yoyote ya utashi wa kuwepo kwa maridhiano ya kisiasa nchini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tunalilia Watanzania wenzetu na haswa Watoto walioachwa wakafe kwa sababu tu ionekane Magufuli anapendwa

Watoto wadogo wameikosea nini Serikali ya kidhalimu ya CCM?
Kila mtu ana muda wake, njia yake na sababu yake kutoweka hapa duniani.
 
Kwani ww ndo unatoa madaraka au wananchi kupitia sanduku la kura?

Unafikiri mtaweza kuiba kura miaka yote?!!!
Kwakua katiba mpya si kipaumbele cha serikali ya CCM, swala la upinzani kutawala litabaki kuwa ndoto.[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Maridhiano ya nini mzee? Kwani tulikua na Vita. Rais Samia endeleza moto ule ule hakuna kumkaribisha mtu Ikulu kunywa Juice
Ujinga wa kuwaita hawa nyumbu Ikulu hakuna tena...kazi kazi...tu!
2414618_24gvpqh.jpg
 
Mungu kafanya yake tayari. Haangalii cha CCM, Chadema, CUF wala ACT.

Na Mungu ataendelea kuwapatiliza wengine ambao hawatajifunza kutokana na hili lililotokea. Mungu ni fundi!
Hakuna chochote utakachofanya hapa duniani kitakachokufanya ukwepe kifo. Wewe sio kama Magufuli, haya Jiulize kama utakufa ua hautakufa. Kama jibu ni kwamba utakufa, Jiulize tena kuna faida gani ya kuishi unavyoishi?
 
Chini ya JPM, tumeshuhudia jamii ya Watanzania ikiwa imegawanyika pasu-pasu kwa misingi ya itikadi kinzani za vyama vya siasa. Mgawanyiko wa jinsi hii haujawahi kutokea kwenye awamu yoyote ya urais huko miaka ya nyuma - ulikuwa mgawanyiko uliosheheni kuhasimiana kiasi cha kufikia watu kutamani kutoana roho, kupotezana, kutekana, kubambikiana kesi za uonevu, nk.

Katika kipindi hicho hicho tumeshuhudia sheria nyingi kandamizi zikitungwa zikiwa zimelenga kuudhoofisha upinzani wa aina yoyote dhidi ya serekali ya JPM.

Nchi imejikuta katika mtanziko huu mkubwa kufuatia mtazamo wa JPM alipokuwa anaingia madarakani mwaka 2015 alipoweka azma yake bayana kuwa lazima vyama vya upinzani viwe vimeshakufa kabisa ifikapo mwaka 2020. Katika kuhakikisha azma hii chini ya utawala wake inafikiwa, tulishuhudia kati ya 2015 hadi 2020 jinsi ambavyo vyama vya upinzani vilivyokumbwa na sulba ya kiama. Hakuna haja ya kurudia yaliyojiri kwani wote humu tunayajua.

Dhamira hiyo ovu hata hivyo haikufanikiwa kwani vyama vya upinzani vikaimarika zaidi ilipofikia mwaka 2020 kuliko hata vilivyokuwa mwaka 2015. Hivyo chama tawala kikabakiwa na silaha moja pekee - kufanya uovu mkubwa wa karne dhidi ya demokrasia October 2020!

Sisi tunaoamini tunajua Mungu ni Mungu wa haki, huwapatiliza wale wote wawafanyiao udhalimu waja wake. Mungu ni fundi. Hutenda kwa majira yake.

Sasa amekuja mama Samia. Wengi tukimtegemea kuwa ni a new hope of fresh air. Watanzania wanamuangalia yeye kama tumaini jipya pekee la kuleta matengenezo katika nchi yetu.

Hata hivyo, kwa maoni yangu naona hajaanza vizuri. Niliyoyaona na kuyasikia so far si dalili za mwisho mzuri kabisa.

1. Kwenye speech yake ya leo pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, hajatambua uwepo wa vyama vya upinzani. Kama kuna mtu kasikia, nisahihisheni!

2. Sambamba na # 1 hapo juu, hakuna mwakilishi yoyote kutoka kambi ya upinzani aliyepewa nafasi ya kutoa salaam.

3. Kuna watu walikamatwa eti kwa kusema tu kuwa JPM ni mgonjwa. Mara tu baada ya kuapishwa, ilitarajiwa atoe decree ya kuachiliwa huru kwao mara moja lakini kimya hadi sasa.

4. Kuna watu wamekamatwa kwa vile eti hawaonyeshi kusikitika kifo cha JPM. Kama rais, alitarajiwa alikemee hili mara moja!

5. Kuna watu kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha kwenye stampede iliyotokea jana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Rais ni mfariji wa taifa, kupitia speech yake ya leo Dodoma alipaswa atamke neno la faraja kwa familia zilizokumbwa na msiba kutokana na tukio hilo.

Zipo dalili nyingine kadhaa lakini nimeorodhesha hizo hapo juu kwa uchache.

Rai na ombi langu kwa rais wetu mpya (mama Samia). Mama tutoe kwenye mtanziko huu ili maendeleo ya nchi yetu yawe jumuishi na wananchi wote tuyafurahie.

JK yupo hapo, nakushauri usisite kuomba ushauri kutoka kwake - mathalani ni jinsi gani aliweza ku co-exist na wapinzani in harmony.

Wakatabahu
Mwalimu M-Mbabe
22 March 2021
Bado mapema
 
Maridhiano ya nini mzee? Kwani tulikua na Vita. Rais Samia endeleza moto ule ule hakuna kumkaribisha mtu Ikulu kunywa Juice
Rais mpya Mama Samia hapendi upuuzi huu
Ndio maana alisema tufute machozi, tuanze upya
 
Hakuna chochote utakachofanya hapa duniani kitakachokufanya ukwepe kifo. Wewe sio kama Magufuli, haya Jiulize kama utakufa ua hautakufa. Kama jibu ni kwamba utakufa, Jiulize tena kuna faida gani ya kuishi unavyoishi?
Kuishi ni Kristo.
Kufa ni faida (lakini kama tu huna damu za watu zinazokulilia!)
 
Maridhiano ya nini mzee? Kwani tulikua na Vita. Rais Samia endeleza moto ule ule hakuna kumkaribisha mtu Ikulu kunywa Juice
Mama Samia hawezi kuhadaiwa na waganga njaa na watu wenye roho mbaya wenye tamaa ya kumwaga damu za watu.

Chapter ya Magufuli tushaifunga. Sasa tuko na mama. Atawanyoosha tu MATAGA!
 
Kaka yawezekana Unaicheza Ngoma husioijua. Magufuli hakua Mjinga kwa Yote aliyoyafanya.

Rais Anajua Mambo mengi kuliko MTU yeyote yule katika nchi hii.

Anajua nia ya kila tahasisi iliyopo katika Jamhuri ya Tanzania kwamba ni njema au ni Mbaya.

Jamaa zako wa chadema wamejificha kwenye koti la kudai democracy lakini nyuma yao wapo wale jamaa zetu wanaotaka Kunyonya rathilimali zetu kwa kivuli cha Democracy.

Fatilia Misimamo yao tangu Awamu ya Mzee Jakaya utagundua hawa jamaa mnaowashabikia ni vibaraka wa Mabeberu. Na kamwe hakuta kua na Maridhiano na watu wa sampuli hii.
Ni mtazamo wako pia
 
Chini ya JPM, tumeshuhudia jamii ya Watanzania ikiwa imegawanyika pasu-pasu kwa misingi ya itikadi kinzani za vyama vya siasa. Mgawanyiko wa jinsi hii haujawahi kutokea kwenye awamu yoyote ya urais huko miaka ya nyuma - ulikuwa mgawanyiko uliosheheni kuhasimiana kiasi cha kufikia watu kutamani kutoana roho, kupotezana, kutekana, kubambikiana kesi za uonevu, nk.

Katika kipindi hicho hicho tumeshuhudia sheria nyingi kandamizi zikitungwa zikiwa zimelenga kuudhoofisha upinzani wa aina yoyote dhidi ya serekali ya JPM.

Nchi imejikuta katika mtanziko huu mkubwa kufuatia mtazamo wa JPM alipokuwa anaingia madarakani mwaka 2015 alipoweka azma yake bayana kuwa lazima vyama vya upinzani viwe vimeshakufa kabisa ifikapo mwaka 2020. Katika kuhakikisha azma hii chini ya utawala wake inafikiwa, tulishuhudia kati ya 2015 hadi 2020 jinsi ambavyo vyama vya upinzani vilivyokumbwa na sulba ya kiama. Hakuna haja ya kurudia yaliyojiri kwani wote humu tunayajua.

Dhamira hiyo ovu hata hivyo haikufanikiwa kwani vyama vya upinzani vikaimarika zaidi ilipofikia mwaka 2020 kuliko hata vilivyokuwa mwaka 2015. Hivyo chama tawala kikabakiwa na silaha moja pekee - kufanya uovu mkubwa wa karne dhidi ya demokrasia October 2020!

Sisi tunaoamini tunajua Mungu ni Mungu wa haki, huwapatiliza wale wote wawafanyiao udhalimu waja wake. Mungu ni fundi. Hutenda kwa majira yake.

Sasa amekuja mama Samia. Wengi tukimtegemea kuwa ni a new hope of fresh air. Watanzania wanamuangalia yeye kama tumaini jipya pekee la kuleta matengenezo katika nchi yetu.

Hata hivyo, kwa maoni yangu naona hajaanza vizuri. Niliyoyaona na kuyasikia so far si dalili za mwisho mzuri kabisa.

1. Kwenye speech yake ya leo pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, hajatambua uwepo wa vyama vya upinzani. Kama kuna mtu kasikia, nisahihisheni!

2. Sambamba na # 1 hapo juu, hakuna mwakilishi yoyote kutoka kambi ya upinzani aliyepewa nafasi ya kutoa salaam.

3. Kuna watu walikamatwa eti kwa kusema tu kuwa JPM ni mgonjwa. Mara tu baada ya kuapishwa, ilitarajiwa atoe decree ya kuachiliwa huru kwao mara moja lakini kimya hadi sasa.

4. Kuna watu wamekamatwa kwa vile eti hawaonyeshi kusikitika kifo cha JPM. Kama rais, alitarajiwa alikemee hili mara moja!

5. Kuna watu kadhaa wameripotiwa kupoteza maisha kwenye stampede iliyotokea jana kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Rais ni mfariji wa taifa, kupitia speech yake ya leo Dodoma alipaswa atamke neno la faraja kwa familia zilizokumbwa na msiba kutokana na tukio hilo.

Zipo dalili nyingine kadhaa lakini nimeorodhesha hizo hapo juu kwa uchache.

Rai na ombi langu kwa rais wetu mpya (mama Samia). Mama tutoe kwenye mtanziko huu ili maendeleo ya nchi yetu yawe jumuishi na wananchi wote tuyafurahie.

JK yupo hapo, nakushauri usisite kuomba ushauri kutoka kwake - mathalani ni jinsi gani aliweza ku co-exist na wapinzani in harmony.

Wakatabahu
Mwalimu M-Mbabe
22 March 2021
We mwl sidhani kama wanafunzi wako huwa wanafaulu masomo yako! Sibonhwa kabisa wewe!
 
Yaani hata week bado hajamaliza unamletea siredi? Tumezidi mno ujuaji sisi watz

Mijitu ya CHADEMA ni kuikazia hapo hapo tu na ikiwezekana zaidi. Hatuwezi achia hii nchi vibaraka wa mabeberu na mabwana zao waje kuifanya watakavyo.
Kama wanashida ya vilainishi visambazwe kwa wanachama wao
 
Back
Top Bottom