Ujio wa SGR tishio kwa mabasi? Inabeba abiria 4000 sawa na trip 70 za mabasi

Aliijenga Kwa tabu sababu hakuwa anapewa hela za bwelelee kama bi. tozo! Imagine wazungu wangekuwa wanamjazia matrillion kila mwezi kama wafanyavyo Kwa Samia hali ingekuwaje.
Hata hiyo 702km alijenga kwa pesa za mkopo,Ila baada ya kuwa na utawala wa hovyo ndiyo mabeberu wakaanza kumbania mikopo
 
Wafanyabiashara washahujumu reli huko nyuma bila hata thread.. Hata ile ya Moshi inasemekana inasua sua kutokana na wafanyabiashara..
 
Nadhani aboud aliliona hilo mapema, na ndio maana akaamua kutafuta routes nyingine mapema... Na si kutegemea Dar - Moro pekee
 
Nauli ndio itafanya mabasi yaendelee kuwepo. Badala ya kuwa cheap ni expensive kuliko basi hivyo watu watakomaa na basi tu maana kuna mtu hata 10,000 ni nyingi kwake plus hupandi na sandarusi.
 
Maendeleo ya Nchi ni kuwa na huduma tofauti tofauti kwenye mazingira hayo hayo na wala usitegemee sijui bus au wasafirishaji wengine watakosa watu hicho kitu hakipo Nchi zilizoendelea na zinazoendelea hivyo vitu vyote vinakuwepo na wote wanafanya kazi kwa kupata watu .
 
Ndio maana nimeweka wahanga wakuu mkuu, Shabiby na Abood.. Ni njia yao kuu ya mapato. Though wengine wataathirika, basi zitazokosa wateja Dar-Moro-Dom zitaenda kubanana kwenye njia mpya..
soma komenti yako miezi 12 ijayo utaona maajabu.
 
Badala ya kuwaza kuhujumu treni wafanyabiashara wa mabasi wawaze kuboresha huduma zao ili kuvutia wateja wao.

Utahujumu mpaka lini, kila jambo lina mwanzo na mwisho wake.

Itafika mahali hujuma zitakoma ila biashara lazima iendelee, treni pekee haitotosha kubeba watu wote na sio kila abiria ataopt kupanda treni, wapo watao opt mabasi hivyo wenye mabasi wajipange tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…