Ujio wa SGR tishio kwa mabasi? Inabeba abiria 4000 sawa na trip 70 za mabasi

Kipya kinyemi serikali hii imejaa uswahili,local people na mundane politicians ambao ndiyo wafanya biashara, train Hilo litahujumiwa ovyo ovyo utaona,hii nchi ya ovyo Sana ,self aggrandization ndo zinatawala,hivi Leo mabasi ya mwendo Kasi yako mangapi barabarani
 
Uswahiba,uswahiba! Nepotism, Nepotism, Nepotism, self aggrandization is going to kill the so called TRC public parastatals
 
Ndio maana nimeweka wahanga wakuu mkuu, Shabiby na Abood.. Ni njia yao kuu ya mapato. Though wengine wataathirika, basi zitazokosa wateja Dar-Moro-Dom zitaenda kubanana kwenye njia mpya..
Wahamie kusafirisha wilayani na mikoa mingine, Tanzania ni kubwa sana
 
Nadhani itabidi wabafilishe business model zao wahudumie maeneo ambayo hayana reli na ni mengi tu
 
Kwa hiyo machungwa ya kutoka muheza tanga yaende Dodoma ili yasafirishwe na SGR?

Uchawa ukizidi unakua uenda-wazimu
 
Mbona tayari mambo yameishaanza mdogo mdogo.
Baada ya kuona watu wengi wanaotumia treni ya asubuhi na jioni kiwepo mimi mwenyewe kutoka Dar to Moro , na kuona inawasaidia sana watu tayari wameamua kuibadirisha nauli zake kuwa 20,000/= na kudai hiyo ni tran ya Express.
Na ile ambayo haina abiria wa kutosha ndio inaondoka saa tatu.
Na kuna tetesu kuwa hizo bei zitabadilika muda si mrefu na kuongezwa.
 
Kagame angekuwa Raisi wa Tanzania SGR na mwendokasi vingedumu
 
All that is immaterial Swali la maana zaidi je ni affordable ? Na kabla haujajibu kumbuka kwamba hii ni huduma na necessarily sio luxury
 
Kwa nauli niliyoisikia leo, Hilo Treni sasa ni kwa wenyenazo. Turudi tu kwenye mabasi kwani kilio chao ndo kimesikiwa.
 
Yametimia!
 
Upande wa pili itafinya sekta binafsi ya usafirishaji kwa wamiliki na wote wanaofaidika na mzunguko huo kama wakata tiketi, wahudumu, madalali, madereva na wamiliki wake wa malori na mabasi.
Mbona imeanza kulalamikiwa ikiwa bado mbichi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…