Ujirani mwingine ni kero tupu

Kiukweli ni tabia mbaya sana kwa mtu kutokuwa na vipaumbele kwenye items muhimu sana kama panga, fyekeo, nyundo, plaiz nk
Nadhani ni tabia mbaya tu sio kwamba hawana uwezo. Kuna jirani yangu ana uwezo kuliko mimi lakini kutwa kuazima mpira wa maji, chepe na jembe kwangu.
 
hujui kua kuna watu na viatu humu duniani?
Huenda huyo ni kiatu...
 
Kwenye huu uzi kila mtu ni mtendwa, hakuna hata mmoja ambaye ni muazimaji. Kila mtu analalamika alimuazimisha mtu.

Au hao wanaoomba vitu hawapo humu na hawana smartphone? Kweli ubinadamu kazi
 
Namnyima.

Kwanza ni uzembe wako mwenyewe mtu kukuzoea kiasi hicho cha kuvuka mipaka.
 
Kiukweli ni tabia mbaya sana kwa mtu kutokuwa na vipaumbele kwenye items muhimu sana kama panga, fyekeo, nyundo, plaiz nk
Bora hata panga na nyundo utasema vinatumika mara chache chache.
Yaani mtu anaazima jag la kuchemshia maji?
Unayekubali kumpa ndo mwenye matatizo.
 
Siku nyingine akija kukuazima jagi, mpe hilo bovu...

Akija kukuazima kiberiti, mpe chenye njiti zilizotumika...

Akikuazima mwamvuli, mpe ulio mbovu...

N.k
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Khaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…