Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024

Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024

Pension aina mmbia inamilikiwa 100% na serikali. Ili pension iweze kulipa michango inahitaji kukuza hizo financial resources ndio maana wanafanya investments za aina mbali-mbali.

Songas kutoa gas chini ya ardhi ilihitajika uwekezaji, kuna mmbia ambae kaweka hela yake na anamkataba wa either consession agreement or PSA na hiyo biashara scope and limitations za activities zake zinajulikana.

Kwa hivyo Songa na Pension funds ni vitu viwili tofauti on sources of funding, ownership structure and scope of their activities, the only similarity ni serikali mmiliki wa hizo entities zote.
Sasa sielewi unaelezea kitu gani hapa ambacho ni tofauti na mradi wa Dege City, sijui Village; ambao nao una mwekezaji kama huyo unayemjadili kwenye maelezo yako hapa. Mwekezaji hakuwa hata na hela za kuwekeza, akitegemea mkopo toka kwa mfuko wa pension, na wakati huo huo.sehemu kubwa ya Ardhi ikiwa ni ya Mfuko wa pension.

Unajaribu kuelezea jambo rahisi kueleweka kwa kuweka madoido to ya 'jargon' kama ulivyo anza kullamika toka kwenye bandiko lako la mwanzo kumsuta mleta mada. Hizi 'jargon' hazibadilishi chochote katika kuelezea ubovu wa mikataba yenyewe.
 
1. Songas kampuni binafsi iliyoingia mkataba wa kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO mwaka 2004 kwa kutumia mitambo ya gesi. Songas iko Ubungo mataa kama unaatokea Mwenge kwenda Riverside ama Buguruni.

2. Songas ilianzishwa kwa mtaji wa Dola milioni 306, yaani 75% ( Serikali ya Tanzania kupitia mkopo) na 25% mtaji. Kwa maana serikali ya Tanzania ilichangia 75% ya mtaji ama Dola 234M kuanzisha kampuni ya Songas na Globeleq kampuni inayomilikiwa na Uingireza na Norway kuchangia 25% sawa na Dola 72M kwenye uanzishwaji wa Songas.

3. Serikali ya Tanzania ilichukua mkopo wa Dolar 234m ili kuchangia kuanzia kampuni ya Songas kutoka Benki ya Dunia (Dola183m) na Benki ya Umoja wa Ulaya (Dola 51m).

4. Serikali ya Tanzania inaimiliki hisa 40% ya kampuni ya songas pamoja na kwamba ndio ilichangia sehemu kubwa ya kuanzisha Songas. 75/25 lakini sasa inamiliki 40% tu.

5. Pamoja na serikali ya Tanzania kuchangia 75% ya kuanzishwa kwa Songas, bado mitambo inabaki kua mali ya Songas baada ya mkataba kuisha mwaka 2024.

6. Mkataba wa Songas ulipaswa uwe ni build, operate and transfer lakini uko build, own and operate.

7. Tanzania tayari imelipa mkopo wote wa dola 234 lakini Songas bado sio mali yake. Hii ni kama Pride Tanzania. Serikali ilitoa mtaji 100% kuanzisha Pride Tanzania lakini baadae ikaja kuonekana Pride Tanzania ni mali ya Iddi Simba😂.

8. Pamoja na kwamba serikali ya Tanzania ilichukua mkopo kutoka WB na EIB lakini riba ilikua kubwa kuliko hata mikopo ya kibiashara ama Commercial loans.

9. Mkataba wa Songas ulikua wa miaka 20 ambao unaisha muda wake July 2024.

Je serikali itaongeza mkataba wa Songas, je isipoongeza na imelipa mkopo wote na bado mitambo sio yake itakuaje?

Soma pia:

1) Songas: Tuko tayari mkataba kupitiwa upya

2) TANESCO yashitukia mkataba wa Songas

3) Serikali yaagiza TANESCO na Songas waanze kugawana mapato kwa usaw

4) Mkataba wa Songas na TANESCO bora uvunjwe, hauna maslahi kwa Taifa!
Mada nzuri, lakini badala ya kusoma mimi nabaki kuigeuza geuza avatar yako kuiangalia hapo shavuni, ni ka nini kamechorwa bwa shee?
 
Mkataba utaongezwa!
Wale wapigaji bado wapo na mwingine mpigaji sana ni yule mwenye "romote control"
Ni mambo ya aibu kabisa haya sijui mapesa yote ya DHULUMA wanapeleka wapi
 
Hii nchi ya vibonde kwelikweli, kitachotokea wachonga deal watashauriana na jamaa kufungua kesi ya fidia tunapigwa tena hela.
 
Umeme wenyewe ndio huu unaokatika kila dakika? Kama vile kuna kitoto cha mwaka mmoja kimeshikilia switch kinaona raha kufyatuafyatua.

Mkombozi wa wengi kwenye inshu ya umeme atabaki kuwa yuleyule tu siyo mwingine bali ni SOLAR PANEL

Hapa ninampango wa kununua solar panel 3 kubwa kwaajili ya nyumba yangu. FULL STOP
 
Mkataba mkubwa huu. Umeanza kuigharagaza serikali katika lugha ya kimieleka kutoka kule Mara Musoma.
 
Back
Top Bottom