Ujue kwa ufupi: Mkataba wa Songas na TANESCO unaotarajiwa kufika tamati Julai 2024

Sasa sielewi unaelezea kitu gani hapa ambacho ni tofauti na mradi wa Dege City, sijui Village; ambao nao una mwekezaji kama huyo unayemjadili kwenye maelezo yako hapa. Mwekezaji hakuwa hata na hela za kuwekeza, akitegemea mkopo toka kwa mfuko wa pension, na wakati huo huo.sehemu kubwa ya Ardhi ikiwa ni ya Mfuko wa pension.

Unajaribu kuelezea jambo rahisi kueleweka kwa kuweka madoido to ya 'jargon' kama ulivyo anza kullamika toka kwenye bandiko lako la mwanzo kumsuta mleta mada. Hizi 'jargon' hazibadilishi chochote katika kuelezea ubovu wa mikataba yenyewe.
 
Mada nzuri, lakini badala ya kusoma mimi nabaki kuigeuza geuza avatar yako kuiangalia hapo shavuni, ni ka nini kamechorwa bwa shee?
 
Mkataba utaongezwa!
Wale wapigaji bado wapo na mwingine mpigaji sana ni yule mwenye "romote control"
Ni mambo ya aibu kabisa haya sijui mapesa yote ya DHULUMA wanapeleka wapi
 
Hii nchi ya vibonde kwelikweli, kitachotokea wachonga deal watashauriana na jamaa kufungua kesi ya fidia tunapigwa tena hela.
 
Umeme wenyewe ndio huu unaokatika kila dakika? Kama vile kuna kitoto cha mwaka mmoja kimeshikilia switch kinaona raha kufyatuafyatua.

Mkombozi wa wengi kwenye inshu ya umeme atabaki kuwa yuleyule tu siyo mwingine bali ni SOLAR PANEL

Hapa ninampango wa kununua solar panel 3 kubwa kwaajili ya nyumba yangu. FULL STOP
 
Mkataba mkubwa huu. Umeanza kuigharagaza serikali katika lugha ya kimieleka kutoka kule Mara Musoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…