Uchaguzi 2020 Ujue Tundu Lissu unakera, unakera, unakera!

Uchaguzi 2020 Ujue Tundu Lissu unakera, unakera, unakera!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Maumivu yanayotupatapa wanaccm kutokana na huyu bwana ni kuusema ukweli unaouma. Huyu jamaa hasahau na wala hapindishi kitu. Yaani mkuki moyoni inaumiza sana ndio maana hatumpendi.

Ni kweli anapowaambia wananchi ukuaji wa uchumi wetu hauendani na maisha halisi ya wananchi, kweli wananchi wanakubali kwa sababu maisha ni magumu sana wao wananchi wanaijua hali hiyo. Sisi viongozi tunaifanya hatujui maisha kua ni magumu tunapindisha ukweli, sasa Lissu anachoma katikati.

Lissu anaposema vifaa vya ujenzi vimepepanda maradufu, sukari imepanda maradufu ndio ujue anachomaka kati kati. Polepole juzi nadanganya eti vitu havijapanda bei muongo mkubwa, nenda kaulize bei ya nguo ya 2014 kwa sasa usikie bei yake.

Ukweli mchungu, Lissu anawaambia watumishi wa umma wengi hawajalipwa stahili zao na wala hawajaongezewa mishahara miaka mitano, wengi hawajalipwa stahili zao baada ya kuachishwa kazi, kwani uongo?

Huyu Polepole kwakua hajui uchungu wa chama na ameingia juzi tu eti anasema watumishi wamepunguziwa kodi, kwani kupunguziwa kodi ndiyo kuongeza mshahara na ndiyo makubaliano ya kimkataba? Aache kudanganya watu kwanza yeye siyo Mwanaccm ameazimwa kwa muda tu.

Lissu huyu anakera,anakera hadi anachukia.
 
Lissu ni mgonjwa, serkali imwache ajitibu kwa kuropoka kila neno baya mpaka October atakuwa amepata nafuu

Baada ya hapo awahi ubeligiji akatibiwe
Swali langu jee anayosema lisu ni yaungoo kwani? Kama niyauongo mbona hamuya jibu kwa hoja ? Jee tangu mwaka 2015 mpaka leo ni mwalimu gani aliyeongezewa mshahara.
 
Kibushuti mmoja wa watesi wa Lissu anena haya:
"Huyu Lissu nilimfukuza Bungeni kwa sababu ni mtoro alikua anazurura Ulaya anaisema vibaya nchi anasema nchi haina Uhuru amerudi hakuna aliyemkamata, anasema tunataka uhuru wakati Nyerere alishauleta anataka uhuru upi?"~Spika Job Ndugai
1599976985278.png
 
Lissu ni mgonjwa, serkali imwache ajitibu kwa kuropoka kila neno baya mpaka October atakuwa amepata nafuu

Baada ya hapo awahi ubeligiji akatibiwe

Wakati mwingine kama huna cha maana cha kuandika ni vyema ukatulia ili wenye hoja waandike hii tabia ya kipumbavu ya kudandia vitu siku moja itakuingiza matatizoni..

Usiharibu thread za watu...anzisha zako....then uone kama kuna mtu timamu atashughulika na wewe.
 
Ccm waliingia na matokeo mfukoni wakizani waliowafungia wasifanye mazoezi hawawezi kucheza na wao lakini 35'' tayari tundu lissu anaongoza 2-0
Unajua hata kichaa akiwa uchi huwa anaona kavaa nguo na anaona yupo sawa na wengine salio wazima, sasa ndo ninyi bavicha, mkijaza ka mkutano kamoja tayari mmeshinda.
Huko morogoro subilini babalao siku akitua huko ndo vibatari vyenu vitazimika.
 
Ccm waliingia na matokeo mfukoni wakizani waliowafungia wasifanye mazoezi hawawezi kucheza na wao lakini 35'' tayari tundu lissu anaongoza 2-0
Unaota mchana Lissu hata kura 600,000 za mbowe hana, tukutane october
 
Back
Top Bottom