Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Heshima mbele wakuu,

Tafadhali nimepatwa na huu ugonjwa mgongoni kwa mabegani hivi na ndo unaanza
  1. Nini chanzo chake?
  2. Nawezaje kupona? Nitumie dawa gani?
Hauwashi ila nikitokwa jasho unakuwa kama unanichoma hivi.
Watu8 MziziMkavu tafadhali katika hili
 
Last edited by a moderator:
Heshima mbele wakuu,

Tafadhali nimepatwa na huu ugonjwa mgongoni kwa mabegani hivi na ndo unaanza
  1. Nini chanzo chake?
  2. Nawezaje kupona? Nitumie dawa gani?
Hauwashi ila nikitokwa jasho unakuwa kama unanichoma hivi.
Watu8 MziziMkavu tafadhali katika hili

UGONJWA WA UTANGOTANGO MWILINI

  • Kwa kawaida, maradhi haya hushambulia zaidi vijana walio katika umri wa balehe na watoto.

Katika mwendelezo wa makala yetu ya maradhi ya ngozi tunaendelea kuangalia maradhi ya ngozi yatokanayo na fangasi, leo tukiangalia hamira (yeast) yanavyoshambulia sehemu mbalimbali za mwili. Maradhi haya kitaalamu huitwa tinea versicolor.

Utango tango (mba)

scabies-1.JPG
tinea_versicolor.jpg

Mba ni maradhi maarufu zaidi kati ya magonjwa mengi yanayosambazwa na fangasi wanaoitwaMalassezia furfur ambao kwa kawaida huishi kwenye ngozi ya watu wazima bila kusababisha matatizo yoyote ya kiafya.

Vimelea hivi husababisha ngozi kwenye sehemu ndogo ya mwili kubadilika rangi ukilinganisha na rangi ya ngozi ya sehemu ya mwili iliyoizunguka.

Mba hushambulia nani?

Kwa kawaida, maradhi haya hushambulia zaidi vijana walio katika umri wa balehe na watoto.

Mwonekano wake

Maradhi haya hutambulika kwa namna mbalimbali, lakini ya muhimu zaidi ni mwonekano wake. Hutambulika kitaalamu kama ‘versicolor., neno la Kigiriki linalomaanisha kubadilika kwa rangi ya ngozi na hii humaanisha kuwa sehemu ya ngozi inayopata maambukizi ya maradhi haya hubadilika rangi yake kutoka ile ya asili.

Mfano rahisi ni mabadiliko ya rangi ya ngozi kutoka maji ya kunde na kuwa nyeusi zaidi au nyeupe zaidi ukilinganisha na sehemu za ngozi zilizozunguka eneo lenye maambukizi ya fangasi hao.

Ni sehemu gani hushambuliwa?

Maeneo ya ngozi yanayoathiriwa zaidi katika mwili ni mabega, shingo, mgongo na kifua.

Mara nyingine maradhi haya hushambulia maeneo ngozi inapojikunja kama vile maungo ya mikono, ngozi ya chini ya matiti, maeneo ya siri hasa pale miguu inapoanzia. Uso mara nyingi hauathiriki, ingawa kwa watoto wanaweza kupata maambukizi ya kwenye kidevu, pua, mashavu na hata paji la uso.
Mara nyingi, fangasi hawa wanaposhambulia uso hushambulia kwa wingi kiasi kwamba ukimtazama mgonjwa kwa haraka haraka unaweza kudhani kuwa hiyo ndiyo rangi yake halisi ya ngozi na kuwa maeneo ambayo hayajaathirika ndiyo yaliyoathirika.

Sababu za kutokea kwake

Sababu za maradhi haya bado zinafanyiwa uchunguzi, lakini kama nilivyosema kwenye makala za nyuma kuhusu namna fangasi wanavyosambaa, na kwamba, sababu hizi pia ni muhimu, nazo ni;

-Hali ya majimaji kwenye ngozi (inaweza kuwa hata jasho)

-Hali ya hewa ya joto (fangasi wanakua vizuri kwenye hali ya joto)

-Kinga ya mwili ikiwa chini

-Mabadiliko ya homoni

Inawezekana pia maradhi haya kupata watu ambao wamekosa sababu zilizotajwa hapo juu.

Usambaaji wake

Kwa vile vimelea vya fangasi vinavyosambaza maradhi haya kwa hali ya kawaida huishi kwenye ngozi si lazima mtu aambukizwe, bali kwa kawaida maradhi haya hutokea tu.

Ukitaka dawa ya kutibu huo Ugonjwa wa Utangotango mwilini ( Mba) Wasiliana na mimi kwa kubonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Tatizo la mba kichwani linasababishwa na

a) Ngozi iliyokufa katika kichwa yaani dead cell

b) Fangas za kichwani iliyodumu kwa muda mrefu (tinea capitis), unapata maambukizi ya fangas za kichwani kwa kushirikiana kwa mfano chanuo, au taulo na mtu ambaye tayari ana maambukizo na pia inaweza kusababishwa na uchafu wa muda mrefu katika nywele.

Kwa maelezo zaidi/maswali ambapo hujaelewa ni SMS namba 0719 252523
 
kama kweli una fangas basi meza dawa inayoitwa griseofulvin kwa siku 30/31 kila siku kidonge kimoja. ila kama sio fangas ila ni deadcells wanapukutika kichwani kama mba na kukusababishia kuwashwa kila leo basi nitafute kwa iyo namba hapo juu
 
Nimekua nikihangaika sana wakuu kwa kutafuta ni dawa gani itanisaidia lakini nimefikia kuambulia matokeo mabovu..nimeshatumia vidonge mwezi mzima lkn ni kma nachochea..unaanzia kichwani mpaka usoni kote mpaka kifuani na mgongoni.. msaada wenu tafadhali wataalamu Wa ngozi.
 
Vidonge vina Feli sana ni Kutumia Tiba za Asili mfano jani la Aloe Vera ule ute wake ukijpaka unasaidia sana
 
Nimekua nikihangaika sana wakuu kwa kutafuta ni dawa gani itanisaidia lakini nimefikia kuambulia matokeo mabovu..nimeshatumia vidonge mwezi mzima lkn ni kma nachochea..unaanzia kichwani mpaka usoni kote mpaka kifuani na mgongoni.. msaada wenu tafadhali wataalamu Wa ngozi.
Chukua maganda ya ndizi mbichi yakaushe then takishskauka chukua na yachome,baada ya kuyachoma yaloweke kwenye maji chuja vema then yachemshe na yabaki maji kidogo.then ipua na hapo tayari kwa matumizi.tumia kujipaka asbh,mchana na jioni.nakuhakikishia wiki moja mba zote kwishaa kabisa.kama hujaelewa uliza ndg nikusaidie.
 
jaribu mafuta ya brake au dawa fulan ya kupaka inaitwa gentalene C
 
Chukua maganda ya ndizi mbichi yakaushe then takishskauka chukua na yachome,baada ya kuyachoma yaloweke kwenye maji chuja vema then yachemshe na yabaki maji kidogo.then ipua na hapo tayari kwa matumizi.tumia kujipaka asbh,mchana na jioni.nakuhakikishia wiki moja mba zote kwishaa kabisa.kama hujaelewa uliza ndg nikusaidie.
Nimekuelewa mkuu Santee sana
 
Usivae nguo mbichi, oga maji vuguvugu siyo baridi , piga Pasi nguo zako usichangie nguo kuepusha secondary infection! Ni PM
 
Chukua maganda ya ndizi mbichi yakaushe then takishskauka chukua na yachome,baada ya kuyachoma yaloweke kwenye maji chuja vema then yachemshe na yabaki maji kidogo.then ipua na hapo tayari kwa matumizi.tumia kujipaka asbh,mchana na jioni.nakuhakikishia wiki moja mba zote kwishaa kabisa.kama hujaelewa uliza ndg nikusaidie.
Je kuna Tiba ya ziada mkuu?
 
Je kuna Tiba ya ziada mkuu?
Hii dawa ya maganda ya ndizi na mafuta ya breki ni mujarabu.
Jaribu kuanza leo then ndan ya wiki moja uje utupe kienda shanda shamba!!!!
 
Nakuongezea, tumia magadi, loweka katika maji, alafu yale maji jipake
 
Back
Top Bottom