Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Ujue ugonjwa wa Mba na tiba yake

Ndugu zangu naomba msaada kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu!
Mimi nasumbuliwa sana na mba mwili mzima na isitoshe huwa nikitoka kuoga ninawashwa mwili mzima na inachukua kama dakika 30 ndo inapungua kuwashwa na hili tatizo lina muda mrefu kama zaidi ya miaka 5.Ninaomba msaada wenu kama kuna yeyote humu ndani aliyewahi kupata hili tatizo na akapata ufumbuzi wake au anaye jua ni dawa gani zinatibu hili tatizo anisaidie! Wanasilisha kwenu wana JF!
 
Tumia mafuta y breki inasaidia

MziziMkavu kwa taarifa.
 
Last edited by a moderator:
Ndugu zangu naomba msaada kama kichwa cha habari kinavyo jieleza hapo juu!
Mimi nasumbuliwa sana na mba mwili mzima na isitoshe huwa nikitoka kuoga ninawashwa mwili mzima na inachukua kama dakika 30 ndo inapungua kuwashwa na hili tatizo lina muda mrefu kama zaidi ya miaka 5.Ninaomba msaada wenu kama kuna yeyote humu ndani aliyewahi kupata hili tatizo na akapata ufumbuzi wake au anaye jua ni dawa gani zinatibu hili tatizo anisaidie! Wanasilisha kwenu wana JF!

chukua vidonge kumi vya septrin (co-trimoxazole) uvisage viwe unga, kisha chukua mafuta madogo ya kujipaka meupe yaitwayo babycare. yapunguze yabaki nusu. changanya kwa kukoroga unga wa septrin na mafuta. tumia mchanganyiko huo kupaka mwili mzima baada ya kuoga. fanya hivyo usiku kabla ya kulala, maana hao fungus hufanya kazi na kusambaa mwili unapopumzika. nakupa wiki moja tu.
 
pole sana kiongozi, fanya hivi, nenda hospitali nzuri, kama upo dar, nenda ocean load, kwa sababu pale wanabase kwenye magonjwa ya ngozi na cancer!!!!
 
Wakuu,

Tunaomba ushauri wenu, wapi kwa Dar anapatikana Daktari ambaye ni specialist wa magonjwa ya ngozi.

Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi sana ambao wamekuwa wanatupigia simu wakitaka kujua ni wapi watapata mtaalam wa magonjwa ya ngozi na hili la MBA likiwa mojawapo.

Shukrani

========

TIBA YA MBA KWA KUTUMIA MBEGU ZA MPAPAI

Mbegu Za Papai Tiba ya Mba

Pia mapapai yaliyoiva yanatibu mapunye (ringworm), mabichi yanatibu msukumo mkuu wa damu (high blood pressure), mapapai yanatumika kama mkuyati (aphrodisiac), yanatumika kama kituliza maumivu (analgesic), mbegu za mapapai zinapunguza maumivu ya tumbo (stomachache)

Mba au mabaka mabaka kwenye ngozi ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ngozi kukosa muonekano mzuri na hata kumfanya mhusika mwenye matatizo kujikuta akijikuna kila wakati.

Kitaalamu mba ni aina mojawapo ya magonjwa yanayoambukizwa na fangasi ambao husababisha muwasho.

Wanawake wengi wanakumbana na matatizo haya ya mba, kutokana na kupaka aina ya vipodozi vinavyowaletea athari katika ngozi zao.

Unapokumbana na tatizo la namna hii ni vizuri kujipaka dawa zinazofaa badala ya kutafuta krimu ambazo ni hatari zaidi. Mbegu za papai ni tiba nzuri na ya asili ambayo haiwezi kukuletea madhara zaidi.

Jinsi ya kuondoa mba kwenye ngozi ya uso

Mbegu za papai ni dawa ya asili inayoweza kutibu ngozi yako na kukuondolea tatizo la kuwashwa au mabaka yanayokukabili.

Namna ya Kutumia kama ni Dawa Mbegu za Papai.

Unachotakiwa kufanya ni kuzipondaponda na kujipaka kwenye eneo lililoathirika na mba. Hii itasaidia kuondoa ugonjwa huo na kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye afya nzuri.

Unaweza kutumia krimu maalum za kuondoa mba hizo, zinapatikana katika maduka ya dawa, lakini unachopaswa kufanya ni kufuata masharti na kupaka kwa umakini kwenye sehemu ilioathirika.

Waweza pia kutumia sabuni maalum ya maji, shampoo, poda na hata baadhi ya losheni zote hizi zinaweza kuisafisha ngozi yako na kuifanya iondokane na muwasho unaokukera na wakati huo kuiacha ngozi yako ikiwa safi na yenye kuvutia.

Kwa wale wote mnaosumbuliwa na tatizo la mba iwe kichwani au sehem zingine za mwili natoa ushauri msichoke kutumia dawa tofauti tofauti kwasababu unaweza kutumia dawa fulani isikusaidie hivyo usikate tamaa jaribu nyingine tena na tena mpaka upate inayoendana na tatizo lako unaweza sikia mwingine ametumia dawa fulan akapona na ukajaribu hiyo dawa usipone usikate tamaa jaribu nyingine tena.
 
Ushauri mzuri,muendelee hivohivo

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
jaman mwenye dawa ya mba wa kichwan na mafuta ya kutumia maana dah kwangu imeshakua kero sa hvi
 
Wakuu kwanza naomba ufafanuzi hivi kweli kuna mba wa kurithi? maana unaweza kukuta mtu msafi lakini mba unajitokeza
Pili ipi dawa ya mba inayotibu kiuhakika maana nshatumia hizi whte field tubes lakin wapi
Kwa anayejua anijuze tafadhali
 
pole sana, cjawahi sikia kwakweli mba wa kurithi? may be, ebu jaribu na mafuta ya break nasikia wanasema ni dawa pia.

subiri wajuzi waje kwa ufafanuzi zaidi
 
kama ni mwilini nenda phamacy nunua dawa ipo ktk kichupa cha rangi ya kijani inaitwa DAWA YA MBA wiki tu mba kwisha
 
waungwana habari zq majukumu naombeni msaada juu ya huu ugonjwa wa ngozi umenitokea mgongoni tokea nijigundue saivi ni wiki 2 tokea uanze sijui ni lini kiukweli nimepoteza amani plz mwenye kujua tiba ya ugonjwa huu msaada waungwana nazidi kulika mgongo mwenzuni
 
Attachments

  • 1430288049585.jpg
    1430288049585.jpg
    29.7 KB · Views: 433
Wakuu,

Tunaomba ushauri wenu, wapi kwa Dar anapatikana Daktari ambaye ni specialist wa magonjwa ya ngozi.

Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi sana ambao wamekuwa wanatupigia simu wakitaka kujua ni wapi watapata mtaalam wa magonjwa ya ngozi na hili la MBA likiwa mojawapo.

Shukrani

========

Dont hestitate kumtafuta dermatologist just for MBA. Fahamu tu mba ni fungus, jua tabia kuu za fangasi, jua namna gani waweza pambana nae fungus hata kutafuna kamwe.

Fungus ni vimelea kama vimelea wengine ambao wapo common juu ya ngozi zetu tunaishi nao siku zote ila mara nyingi hawakui kutokana na kukosa nafasi nzuri kufanya hivyo. Fangasi huhitaji chakula kumea hivyo anapopata nafasi ndio humea. Mba ni fangasi anaemea juu ya ngozi hivyo matibabu yake huwa juu ya ngozi. Fangasi alie mea kwa muda mrefu na kujiwekeza vilivyo ni vigumu kumtibia kirahis hivyo huhitaji matibabu ya muda mrefu. Fangasi hapendi maeneno yenye hali ya asidi ktk ukuaji wake hivyo kwa kuliweka tu eneo husika ktk hiyo hali huweza kuwapukutisha kirahisi. Lakini kuna dawa maalum hutumika mara nyingi huwa katika mfumo wa kama mafuta ya kupaka. Na kwa jinsi walivyo wabishi waweza paka mafuta hayo kwa muda mrefu zaidi huwa tunashauri pengine wiki mbili zaidi baada ya kupotea kwenye ngozi hii husaidia kuwa fanya wasirudi haraka.

Sababu kuu ya kuwafanya fangasi wakue ni kupungua kinga ya kuwazuia hivyo dalili ya fungus wengi juu ya ngozi ni kumaanisha ngozi hiyo haina afya nzuri pia mi kavu ili kujikinga hasa na kupona haraka na fungus huna budi kula vyakula vya kujenga afya kunywa maji ya kutosha na mazoezi ya afya. Labda kama kuna swali zaidi
 
Back
Top Bottom