Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 182,097
- 1,099,383
Mkuu. Hoja yangu haijajikita huko unakotaka kunipeleka.Huu ujumbe wa kwamba hakuna mtu awezae kufika mbinguni bila kumfuata yesu uko sawa lkn jiulize ni kwa wakati gani.kuna vitu inabid kabla ya kubishana tujiulize wenyew katika akili zetu mfano hapa Tz kila baada ya miaka 10 anateuliwa Rais mpyaa na kila Rais anakuja na mifumo baadh mpyaa na haijawah tokea mtu akasema Rais wa sasa simtambui na hata dini ni hivo kama tunajua Mungu alimtuma Ibrahim akamtuma Daud Musa na kisha yesu kwanini mkatae ujio wa Muhammad?
Hoja yangu kuu ni hii: Kama mwislamu anaweza kusema kuwa hakuna atakayekwenda mbinguni bila kuwa mwislamu; na akatoa na ushahidi kutoka katika kitabu chake anachokiamini (ambacho wengine wasio waislamu wanaweza wasikiamini); ni nini kinachompinga Mkristo (au dini nyingine yo yote) kusema kwamba bila kupitia dini yake hakuna kwenda mbinguni; na akatoa na ushahidi kutoka katika vitabu vyake vya dini anavyoviamini?
Kwa maneno mengine; ni kwa nini unaamini kuwa Uislamu ndiyo njia sahihi ya kwenda Akhera? Ni kwa vile Quran (ambayo wengine wasio waislamu hawaiamini) imesema hivyo ama?
Kwa nini Mkristo asiamini kuwa bila Yesu hakuna kwenda mbinguni; wakati Biblia anayoiamini inasema hivyo?
Umenielewa?