Ujumbe kutoka kwa wanachama minority wa CHADEMA kwenda kwa mwenyekiti mpya Tundu Lissu

Swali ni dogo tu. Unajua maana ya legitimacy. Kama hujui subiri dunia itakufundisha. Nasaha zangu ni za nia nzuri na muda bado tunao ikiwa tunataka kushika dola.

Legitimacy ndio roadmap ya kushika dola.
ACT au CUF haikuwahi kuwa legitimacy? Au uliwahi kuwashauri wateue na wakristo wapate hiyo legitimacy?

Hii ni democratic society, na tunafuata democratic processes, na hatujatoka kwenye vurugu zitokanazo na racse au dini. Ingueni kwenye siasa tafuteni nafasi za uongozi kwa merits siyo kubebwa.

Wakati Bob Makani muislamu alipokuwa katibu mkuu wa kwanza na baadae mwenyekiti wa CHADEMA ilikuwa ni kwa sababu ya uislamu wake? Au profesa Safari makamu mwenyekiti ilikuwa ni sababu ya uislamu wake?

Kama minority mnaijiita kuwa ni waislamu, wenye muelekeo wa kiisalamu hamtaki au hamna qualification au ushawishi wa kuweza kugombea mkachaguliwa kwa sifa za uongozi mnataka kupewa nafasi ili CHADEMA ipate legitimacy kwa waislamu tafuteni chama kitakachowapa legitimacy ya udini. ACT au CCM kutawafaa sana, acheni wanaotaka kujenga secular state ambayo dini siyo kigezo cha kupata uongozi waendelee.

Tatizo hili lipo ndani ya mioyo yenu isiyokuwa na dhamira nzuri
 
Akili ndogo. Dini si udini. Dini ni jukwaa. Ndio maana hata Lissu na Mbowe walisuluhishwa na viongozi wa dini. Hivyo kuweka legitimacy yao.
Akili ndogo kufikiria dini kuwa jukwaa, secular states hawafikiri dini kuwa jukwaa labda nchi za kidini mostly za kiarabu.

Unataka kupotosha maana ya legitimacy, ilikuwa ni vigumu kupata usuluhishi mwingine ndio maana walikwenda kusuluhishwa na viongozi wa kidini. Kama walipata legitimacy kwa viongozi wa dini walifanikiwa kusuluhishwa? Mbona walitoka vile vile hadi kwenye sanduku la kura ndio ukawa mwisho na wanachama wakaamua?

Pendekeza waislamu wako wakagombee washawishi wajumbe kwa vichwa vyao siyo dini yao wachaguliwe. Kwenye uchaguzi wa CHADEMA sikusikia yeyote akija na manifesto ya udini, huo ni wa kwako na wenzio nendeni ACT. Je wasio waislamu au wakristo mnawafanyaje?
 
Mtu yupi wa pwani aliyejitokeza kugombea nafasi ya uongozi? Au mnataka kuteuliwa tu? Yupi aliyekuwa kwenye harakati za kukijenga au kukipigania chama cha CHADEMA kiasi unaona ateuliwe tu kwa misingi ya udini?
 
simple nendeni mkapigie CCM na ACT, kabla ya ujinga wa Magufuli kwenye uchaguzi CHADEMA ilikuwa inapogiwa kura na watanzania regardless ya imani zao. Huo upuuzi wa udini hauna nafasi Tanzania
 
Wewe ni shetani haswa, ulichukua form ukanyimwa? mbona Zanzibar CCM/ACT ni waislamu watupu lakini hujawahi kulalamika au Zanzibar hakuna wakristo?
 
Nazungumzia legitimacy na sio authority.

Kama hamuelewi kuhusu uongozi (leadership) na ushawishi subirini October.
Ungekuwa na akili ungejiunga na wale wanaotaka tume huru na mabadiliko ya sheria za uchaguzi na katiba mpya ili tunapoenda kwenye uchaguzi uwe wa haki. Kumbe wewe mabadiliko yako ya kuwapa ushindi wapinzani ni kuwateua waislamu? Aisee sijaona jamii yenye watu wajinga kama hii.
 
1.Hapa Kuna harufu ya udini.

2.Ndio kwanza watu wamekabidhiwa ofisi jana ila una rap kama wana mwaka ofisini.

3.Mahalimu kwenda ACT ni CHADEMA hawakuwa active ili kuinasa sahihi yake.

4.Kila mtu alikuwa na haki ya kugombea kama alikidhi vigezo,kama unaushahidi hebu tuambie ni Akina nani walienguliwe baada ya kuomba nafasi kwa kigezo cha udini.

5.kuhusu ukanda bado unazidi kupotosha,Lisu,Heche,Nshala,Mnyika,Lema ,BOB NK,Hawa ni wa kanda moja na kabila moja?

6.Punguza hisia za mapema subiri watu waingie kazini rasmi.
 
Unatatizo kubwa sana la UDINI
Nadhani infiriority complex inakusumbua
 
Competency based ni muhimu kuliko huo udini wako.
 
Hakuna siasa zinazoweza kufanyika Tanzania zikasimama bila kushirikisha jiji la dar. Na dar ina wenyeji, sasa utawezaje kumobileze wenyeji wa dar wewe ukiwa wakuja. Utawezaje bila ya kutanguliza wenyeji.

Nywrere alifanikiwa kwa kutambua hili.

Niwaambie tu yawezekana huu ni mkakati wa watu wakuja kuiteka dar.

Wenyeji wa dar wanajulikana kama wajumbe.

Kama mnadhani wenyeji wanataka vyeo kwa njia ya huruma, yawezekana hujui siasa na ktk hali hiyo hebu tuache muda uongee.
 
Haya ndio mambo yanayofanya waislamu waonekane kituko, kumbe ni mjinga mmoja tu
Ahsante mpiganaji wa Keyboard. Mwaka mmoja NCCCR Mageuzi iliamua kwenda pemba na kushiriki uchaguzi. Matokeo yalivyotoka hawakuamini.

Naona chadema inajiandaa na matokeo makubwa wakiamini wao wanaweza kuwapatia waislam nini cha kufanya.

Tuache muda utaongea
 
Unatatizo kubwa sana la UDINI
Nadhani infiriority complex inakusumbua
We are oppressed society by the ccm. Tulidhani chadema tungeweza kupata hifadhi.

Pamoja na hali hiyo tuna kura ya Maamuzi. Lkn hatuwezi ipiga hadi tuwe na wawakilishi wanaweza kutosema maslahi yetu ktk taifa hili

Tofauti na chadema walipitia mateso kwa miaka 7 Watu wa pwani wamedhibitiwa kwa miaka 60.

Anyway binafsi mwelekeo wangu ni CHAUMMA
 
Umeanza kunialewa baada ya kuona umejenga hoja ingawa ni finyu.

Waislam wengi wako ACT. Wengi ni wenzangu tuliotoka CUF Ngangari. Nilipowauliza kwann mmeamua kwenda ACT wengi walijibu tunafata Sief, mimi sifati mtu, dini wala kabila. Ninafata falsafa cha taasisi. Na nimeridhika na ile ya Serikali ya majimbo (Federal States). Lkn kuna hawa wenzangu wa kufata upepo, kufata mtu, mtu wao. Ndio lengo la kumzingua Lissu ktk Uzi huu.

Sisi minority hatuna njia ya kuendelea kuwashawishi kundi kubwa ambalo kufata watu, hufata upepo.

Sasa kama wawakilishi wao hawako chadema tunafanyaje mabadiliko kwa kuondoa dola
 
Ondoa adha ya udini
 
Kwa ufupi nilimshari mwenyekiti achague katibu mkuu Muoslam na ingewezekana naibu katibu mkuu wake. Na nilipendekeza Sheikh Ponda angekuwa katibu mkuu wa chadema.
Duh hii mpya, sheikh Ponda katibu mkuu wakati hana kadi ya chadema!! Watu wanachagua mabadiliko sio dini, mbona Lissu alipata kura nyingi kuliko Membe huko zanzibar licha ya ACT kuwa ndio kinawavutia zaidi wazanzibari kuliko chadema?
 
Waislam wengi wako ACT.
Acheni ujinga, mbona huwa wanapata kura laki 1? Ina maana nchi hii kuna waislam wapo laki 1? Embu jiulize ilikuwaje chadema iwazidi kura ACT hapa dar wakati ni Muslim majority?

Tuache udini, tufocus kwenye chama Imara maana umaskini na ufisadi wa CCM hauathiri dini moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…