Kama una amini ipo siku ya mwisho (siku ambayo wanadamu watahukumiwa kwa matendo yao ya hapa duniani) Angalia sana haya......
1. Acha kujichukulia mali za masikini (zisizo halali) na kujilimbikizia, utapata tabu sana siku ya mwisho
2. Acha kupunja watu kwenye Mizani, adhabu yake ni kali sana siku ya mwisho
3. Acha kunyima watu haki yao (sheria) kwa sababu ya janja janja yako, utajutia sana
4. Acha ushirikina/uchawi/Kwenda kwa waganga kudhuru watu wasio na hatia – utapata tabu sana siku ya mwisho
5. Mali ya mayatima (watoto waliofiwa na mzazi/wazazi wao) ogopa sana hii kitu kama moto; unatakiwa uwasaidie kusimamia hadi watoto wakisha kua (miaka 18+) uwakabidhi mali ya mzazi/wazazi wao.
6. Ardhi, Mungu huangalia kwa karibu sana hii kitu; usichukue Ardhi isiyoya kwako hutabaki salama
Siku ukifa raha zote ulizopata hapa duniani utaona kama ni raha za siku moja na hazitakusaidia chochote...
Ulio waacha huku duniani watachezea mali ulizo limbikiza, huku wewe ukipata cha moto huko kwa Mungu, ni suala la muda tu
Saidia masikini kwa hela zako za halali, sio uibe milioni 100 za masikini, halafu utoe milioni 10 sadaka ufikiri umetoa sadaka; jua tu kuwa, Mungu hapokei mali ya wizi!
Saidia watu wenye mahitaji (masikini) kwa kadri ya uwezo wako na nafasi yako uliyobarikiwa. Wengine wanakuhitaji tu utamke