Ujumbe maalum wa tahadhari kwa Maaskofu na waumini wa KKKT

Ujumbe maalum wa tahadhari kwa Maaskofu na waumini wa KKKT

Its true ndio maana nimeshauri tuwe na The African church
P
Kaka P, this is 21st century hivi tangu aondoke Yesu tuseme hajaonekana jiniasi yeyote aliyegundua hiyo kitu hadi leo tuje tugundue sisi?? Nadhani, kuna kauasi ndani na uasi mbele za Mungu akheri uchawi
 
Jamani Mwananchi kuna kichwa cha habari KKKT maaskofu ..
Tuwaombee jamani
 
KWA MUDA MREFU NIMEKUWA KATIKA SHUHUDA KWA WATU, NDANI NA NJE YA NCHI KUHUSU MWENENDO WA KANISA LETU, VIONGOZI WETU KATIKA KANISA NA HATA KUHUBIRI MAMBO AMBAYO KWAYO, KKKT LIMELELEWA MIAKA MINGI ILIYOPITA.

SISHANGAI MABADILIKO NDANI YA KANISA, ILA MABADILIKO YANAPOKIUKA MISINGI YA DINI, IMANI, MAADILI NA MAFUNDISHO YAPASA KUYAKEMEA BILA KUPEPESA MACHO.

NIMEWAHI KUSEMA JUU YA MWENENDO WA MCHUNGAJI WANGU *SAMWEL PALLANGYO* AMBAYE KWA SASA ANATAKA KULICHAFUA KANISA KWA SABABU ANATAKA KUWA ‘YUDA’. AMESHAWISHI KONGAMANO LIFANYIKE TAREHE 29/12/2019 NA LITASHIRIKISHA NDUGU ZAKE WALIOMPA FEDHA.
KANISA LINAPOAMUA KUFANYA BIASHARA ZA NAMNA HII, LINAHARIBU TASWIRA YA KANISA LA KIKRISTO KWA UJUMLA.

BABA ASKOFU DKT. SHOO UPO, KWA NINI YEYE AFANYE VIKAO VYA SIRI VYA KUTAKA MAGEUZI NDANI YA KANISA NA NCHI BILA MAASKOFU WOTE KUFAHAMU JAMBO HILI? JE HARIDHISHWI NA MKUTANO MKUU WA KANISA AU HALMASHAURI KUU? TUNAPOKUTANA MAKUMIRA NA KUYAJADILI MAMBO YETU KATIKA KANISA MBONA HUWA HAYASEMI AMBAYO MOYO WAKE UNAYATAKA? URATIBU WA MAMBO KWA NJIA ZA SIRI KULIHUSISHA KANISA LENYE UONGOZI JE, SI SHAMBI HIYO?
KWA AMBAO BADO HAMJASHIRIKISHWA, JIANDAENI.

ANALITUMIKIA KANISA NA ANATUMIKIA CHAMA CHA SIASA KUPITIA KANISA. ANALIPWA FEDHA, ANASHAWISHI WAUMINI MMOJA MMOJA. MIONGONI MWETU TUNALAZIMISHWA KWA SABABU FULANI FULANI BILA KUJALI KWAMBA KANISANI WAPO WAUMINI WA VYAMA MBALIMBALI.

ANAHIMIZA KUFUATA MSIMAMO WA CHAMA CHA SIASA AMBACHO KATIBU WAKE MKUU AMEMUAGIZA AHAKIKISHE KKKT INAUNGA MKONO BAADHI YA MAMBO YAO, KAMA SIO YOTE.

KWA WALIOZALIWA KABLA YANGU, SIAMINI KATIKA MTAZAMO HUU. KAMA MUNGU ALIPANGA JAMBO KUTOKEA, LITATOKEA. BINADAMU KULAZIMISHA MAMBO NI ISHARA MBAYA HASA MBELE YA MADHABABU.

JOHN MNYIKA ANAPOANZA KUTOA MAELEKEZO NDANI YA KANISA LA KKKT TENA KUPITIA MCHUNGANI AMBAYE YUPO CHINI YA VIONGOZI WAKUU WA KANISA KATIKA NGAZI YA USHARIKA, JIMBO NA DAYOSISI NI ISHARA KWAMBA TUNA WATU AMBAO WANAWEZA KULITUMIA KANISA KUTUVURUGA.

HEBU TUKUMBUKE KIKAO CHETU CHA MWISHO PALE MAKUMIRA, BABA ASKOFU UTANISAIDIA, MAENEO AMBAYO WENGI WALIYAPIGIA KELELE NI MIGOGORO NDANI YA KANISA.

BILA KUJADILI ATHARI ZAKE, SAMWELI ANAINGIA NADHIRI YA KUYATUMIA MADHABAHU KWA AJILI YA KUTAKASA FEDHA AMBAZO ZITALETWA KANSANI KWA KAZI ZA KAISARI. MUNGU TUMPE YAKE NA KAISARI TUMPE YAKE.

SISI TULIO KATIKA KANISA TUNA WAJIBU WA KUOMBA AMANI, UTULIVU NA MSHIKAMANO WAKATI WOTE. MIGAWANYIKO SI JADI YETU, ONENI KAZI TUNAYOPATA KATIKA MAENEO YENYE MIGOGORO KATIKA KANISA LETU LA KKKT. HATA MUNGU AKISHUKA LEO, ANAWEZA KUTUHUKUMU KWELI KWELI.

MADAI YA KISIASA YAKIANZA KUINGIA KANISANI TUTAWAGAWA WATU. HUWEZI KUINGIA KATIKA IBADA YA TAREHE 1/1/2020 NA KUSEMA “SASA TUNATANGAZA RASMI KUWA TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI”.

KANISA LINA VIPAUMBELE VYAKE, NA VYAMA VYA KISIASA VINA VIPAUMBELE VYAKE. TUJIKITE KATIKA DHAMIRA ZA KIROHO KULIKO DHAMIRA ZA KIMWILI.

HATA WARAKA TUNAOSHIRIKI KUUANDAA KAMA KANISA,TUNAWEZA JITIA DOA JEKUNDU KATIKA VAZI LA THELUJI. TAREHE 1/1/2020 UWE MWANZO MWEMA WA MWAKA 2020 LAKINI ENDAPO TUTAKUBALI KUTUMIKA, TUTAHARIBU KANISA.

NAWASIHI SANA VIONGOZI WETU WOTE KATIKA NGAZI MBALIMBALI: WAKUU SHARIKA ZETU, MAJIMBO, DAYOSISI, MKUTANO MKUU NA HALMASHAURI KUU HEBU MWAKA 2020 UWE MWAKA WA MAPATANO NDANI YA KANISA NA SIO MIGAWANYIKO.

TUTUNZE NADHIRI KATIKA KAZI YETU YA KANISA ILI NEEMA ZA MWENYEZI MUNGU ZISHUKE KWETU NA VIZAZI VYETU, SASA NA HATA MILELE.

MUNGU AWABARIKI!

_MSHARIKA MWENZENU, KKKT - USHARIKA WA ARUSHA MJINI_
Weka jina lako hapa wacha umbeya mpuuzi mkubwa.Usharikani kwetu hatuna mbumbumbu kama wewe.Wewe ni mamluki umejichomeka usharikani kwetu kutuchafua.Hiyo barua ya maagizoAliyopewa kama kweli iweke hapa.Mmbeya mkubwa wee.
Unamchafua Mchungaji wetu bila kuwa na haya.Utashangaa yatakayokufuata.Huyo ni mpakwa mafuta achana naye.
 
Ukisoma Bible Yote, Kulikuwa na Intergration Kubwa Mno kati ya Dini na Serikali(Siasa), Kuanzia Kina Musa, Samweli, Daudi, Yoshua wote walikuwa wanafanya Intergration na Siasa, wakiwa na Lengo la Kuwaunga Watu kwa Mungu;
Kuwaeleza watu habari ya MUNGU.
Changamoto ya Viongozi wengi wa Dini Africa , wanafikiri kwamba wao wapo kwa ajili ya Dini zao tu, Au watu wa Imani yao tu, Lakini Sheria ya MUNGU inatutaka kufanya UPENDO, of which utaona hapo ili kuonyesha Upendo ni lazima kwa namna Flani usiwe na Ubaguzi wa Dini yako, watu wako etc.

Anyway haya ni mambo ya zama hizi tu, yatabadilika hata kama hatutakuwepo, naona vugu vugu kwa mbaali, la mabadiliko ya waamini, sasa wachache wanaanza kuelewa Vitabu vyao vya Kiimani; Wenzetu wa huku Ughaibuni walishatoka siku mingi sana kwenye masuala ya Imani mfu.
 
Back
Top Bottom