Mimi ni raia wa kawaida wa nchi hii. Nachukuwa fursa hii kutoa ujumbe wangu kwa wasaidizi wa Mh Rais wetu wote kwenye Serikali na Chama (CCM)
Historia ya nchi yetu imepata doa ndani ya miaka 4 ya utawala wa JPM hilo halina ubishi. Ama iwe ni kwa bahati mbaya, makusudi au kwa kutojuwa ni DHAHIRI Utawala huu umeshindwa kuendana na kungamua mbinu za KIDIPLOMASIA na nguvu za mataifa ya ulimwengu. Tukubali tumeshindwa kubalance mambo ili Tanzania iendelee mbele smoothly.
Niwakumbushe kwamba ni CCM hii hii imetawala awamu zilizopita na sera hizi hizi zilizokuwepo na hatukuwahi kupata doa hili. Lazima kuna tatizo mahali.
Sasa nitoe ujumbe wangu.
Mkumbuke kwamba Tanzania inaendeshwa kwa misingi ya KATIBA na Sheria, wajibu wa kufuata matakwa ya Sheria zetu hayategemei hisani ya Raisi AKISHAKUTEUWA. TENDENI kwa mujibu wa sheria.
Tambuiweni kwamba JINAI haizeeki. na Tambuweni kwamba wateule hawana KINGA. Kuna baadhi wamefanya makosa ya wazi na yameingia kwenye kumbukumbu tayari, wajibu ni kujisahihisha leo kabla ya kesho.
Tambuweni kwamba Tanzania sasa inamwilikwa kwa macho yote. Tulionya tokea Mwanzo, Jihakiki matendo yako na uchukuwe tahadhari za matendo na maneno kuepuka kuvunja sheria na katiba kwa wadhifa wowote ulionao.
Historia imeshauingiza utawala wa Rais Magufuli kwenye alama fulani, ikiwa ni nzuri nanyi mtahusishwa ma mazuri na ikiwa ni mbaya mtabeba mabaya hayo vile vile. Jipambanue sasa kwa Maslahi ya Taifa. Jipime mwenyewe kwa kiasi gani utaepuka ANGUKO LA DIPLOMASIA kwa Tanzania kwenye awamu ya tano?
Viongozi wote wa serikali na CCM mna wajibu wa kuisaidia Tanzania kama Taifa na watanzania wote, Nyinyi ndio mmeipeleka Tanzania hapa ilipo na nyinyi ndio muikwamue hapa ilipo. Mshaurini Rais achukue hatua stahiki. Wasaidizi wote na wenye dhamana ya nchi hii hasa kwenye Ulinzi na Usalama, mwambieni Rais afanye nini ili tutoke na aibu hii ya Anguko la Diplomasia ambalo halina mwisho Mwema.
Tambueni Kwamba Dunia ni kijiji na wenye Dunia yao wapo. Rejesheni hali ya kawaida.
MAMBO YA KUZINGATIWA.
Fanyeni ubunifu wa kuziba mianya ya ndani kwanza kwa kuwaweka watu wenye tofauti pamoja mkitaka anzeni na vyama vya SIASA, viongozi wa dini na wadau wa maendeleo.
Fikirieni Ajenda ya Kitaifa kwa mnasaba wa hali ilivyo na fikirieni Uzalendo shirikishi wa Kitaifa na sio Uzalendo wa Ki- CCM. Tunahitaji kutoka sasa.
CCM na Wasaidizi wa Rais mna wajibu wa kumsaidia Rais, hatutarajii mumpe mapambio ya kumvimbisha hapana, angalieni leo na kesho na angalieni makosa ya wengine hapa hapa Afrika ili liwe funzo.
Tulionya mwanzo na leo tunakumbushia, Wadau wa Tanzania ni muhimu kwenda nao sambamba. Kuanzia ndani na nje tatizo ni kujiona mko sawa kwa kila jambo.
Tafuteni tatizo mlitatue ili watanzania wawakumbuke.
Msisahau KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI
Tafadhali CCM chukueni Hatua.
Kishada.