Ujumbe: Taifa hujengwa kwa watu kufanya kazi kwa bidii, nguvu na akili nyingi na sio mizahamizaha na kuendekeza ujinga

Ujumbe: Taifa hujengwa kwa watu kufanya kazi kwa bidii, nguvu na akili nyingi na sio mizahamizaha na kuendekeza ujinga

Mfumo ndio umewafanya wawe masikini, kwa maana ya umasikini unaletwa na watawala Ili iwe rahisi kuwatawala watu, huwezi mtawala mwenye shibe.

kwahiyo unamaanisha tusubiri siku wenyewe wakiamua kuongoza vizuri au kuondoka madarakani.
 
Nakukatalia pale unaposema vijana wanapambana au watanzania wanapambana, SI KWELI, ni wachache sana katika nchi hii ni productive kwa maana ya productive, tuliowengi tumerelax na wengine ni wavivu huko makazini.
Kua productive sio poa, mtu lazima uwe na discipline ya juu.. upende kusoma, uwe self aware, maono ya mbali, mahesabu makali, connection, meditation, alliegences e.t.c

Sasa chimbuko yote haya ni tunavolea watoto, tuwekeze muda kwa vijana wetu zaidi.. ni mifumo ya ku set profusely!

WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

Nahusisha huu msemo 👆 maarifa ni malezi ambayo ilitakiwa vijana wapewe au walipewa wakakiuka maadili matokeo yake ndo haya productive wachache sana!
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
"Asiye fanya kazi na asile" hii aya ipo kwenye kitabu cha Biblia na ni maneno ya Mwenyezi Mungu kupitia nabii wake Yesu kama sijakosea.

Waislamu kuna mahala wanaambiwa wakishafanya ibada watawanyike wakatafute ridhki.
Hata dini zinaamini kwenye kufanya kazi.

Watanzania na Waafrica tunaumiza vichwa sana juu ya mkwamo tulionao na kujikosesha majibu kwa makusudi kwa kuukwepa ukweli asiyefanya kazi na asile.

JE WATANZANIA TUNAFANYA KAZI? ILI MWISHO WASIKU TULE?, JIBU: HAPANA.
idadi ya wazarishaji ni wachache na waliowengi ni walaji na hapa nini tufanye wengi wazarishe na wachache wale kwa sababu maalumu TUMEKWAMA HATUNA JIBU.

Hakuna mahala unaweza kujenga taifa kwa kutegemea watu legelege na wamizahamizaha kama jamii ya Kitanzania, Tuna watu wengi wazembe na legelege ambao hawazarishi na hata wanaozarisha wanazarisha kidogo na muda mwingi wanautumia kwenye mizaha na ujingaujinga.

Mataifa yaliendelea duniani kwa watu kufanya kazi kwa bidii na kuwa serious na maendeleo ya mataifa yao, vizazi hivi vilivyojitolea vimeacha urithi thabiti kwa watu wake kuanzia nguvu, akili, uelewa, ustaarabu nk, urithi huu ndio hutumika mpaka leo kutawala wajinga wajinga WaAfrica wanaolialia na kuendekeza upumbavu.

KILA MMOJA ABADILIKE ALIPO YEYE NA KIZAZI CHAKE KAMA KWELI TUNATAKA KULETA MAENDELEO NA KUACHA ALAMA KWENYE HII ARDHI, HAKUNA MAHALA WATU LEGELEGE NA WAMIZAHAMIZAHA WALIWEZA KULETA MAENDELEO.
Hatuwezi kutoka hapa tulipo bila mfumo madhubuti na imara, mizaha inaanzia juu inashuka chini, uliwahi kusikia /ona nchi zilizoendelea wanafunga mifumo na kubadirisha mara kwa mara kama huku? Kila kiongozi akiingia anafunga uliokuwepo anaanzisha wake,ukifunga maana yake unaathili shughuli za uzalisha kwa ujumla wake, Ungeshauri waliopo juu wajenge kwanza taasisi imara,itakayosimama bila kuyumba , halafu hayo mambo mengine ndio yafuate sasa mbona mambo yataenda mchaka mchaka,hata hao wavivu wataamshwa tu
 
Back
Top Bottom