Ujumbe: Taifa hujengwa kwa watu kufanya kazi kwa bidii, nguvu na akili nyingi na sio mizahamizaha na kuendekeza ujinga

Mfumo ndio umewafanya wawe masikini, kwa maana ya umasikini unaletwa na watawala Ili iwe rahisi kuwatawala watu, huwezi mtawala mwenye shibe.

kwahiyo unamaanisha tusubiri siku wenyewe wakiamua kuongoza vizuri au kuondoka madarakani.
 
Nakukatalia pale unaposema vijana wanapambana au watanzania wanapambana, SI KWELI, ni wachache sana katika nchi hii ni productive kwa maana ya productive, tuliowengi tumerelax na wengine ni wavivu huko makazini.
Kua productive sio poa, mtu lazima uwe na discipline ya juu.. upende kusoma, uwe self aware, maono ya mbali, mahesabu makali, connection, meditation, alliegences e.t.c

Sasa chimbuko yote haya ni tunavolea watoto, tuwekeze muda kwa vijana wetu zaidi.. ni mifumo ya ku set profusely!

WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA

Nahusisha huu msemo 👆 maarifa ni malezi ambayo ilitakiwa vijana wapewe au walipewa wakakiuka maadili matokeo yake ndo haya productive wachache sana!
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Hatuwezi kutoka hapa tulipo bila mfumo madhubuti na imara, mizaha inaanzia juu inashuka chini, uliwahi kusikia /ona nchi zilizoendelea wanafunga mifumo na kubadirisha mara kwa mara kama huku? Kila kiongozi akiingia anafunga uliokuwepo anaanzisha wake,ukifunga maana yake unaathili shughuli za uzalisha kwa ujumla wake, Ungeshauri waliopo juu wajenge kwanza taasisi imara,itakayosimama bila kuyumba , halafu hayo mambo mengine ndio yafuate sasa mbona mambo yataenda mchaka mchaka,hata hao wavivu wataamshwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…