Ujumbe wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa unaosababisha 'Changamoto ya Upumuaji'

Ujumbe wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kuhusiana na mwenendo wa ugonjwa unaosababisha 'Changamoto ya Upumuaji'

Hata hawaeleweki yaani. Full kujichanganya
Ukweli hapo Ni kuwa corona ipo na inazidi kusambaa na kuua watu, ila imetumika lugha ya kisiasa zaidi tujikinge na kumuomba mungu maana kwa hili si kwa ujanja wetu Wala watawala, Ni Allah pekee
 
Madaktari wa ovyo kama hawa, wasio na ujasiri wa kusimama katika taaluma, hawawezi kulisaidia Taifa wala kulinda wanachama wao.

Wanachama wa hiki chama wanastahili na wanayo haki ya kufukuza uonhozi wote. Viongozi kama hawa wanaweza kuua wanachama wao kwa unafiki wao.

Mara changamoto ya kuoumua siyo ugonjwa, mara ili kupambana na changamoto ya kupumua - ujinga mtupu.
 
Ukweli hapo Ni kuwa corona ipo na inazidi kusambaa na kuua watu, ila imetumika lugha ya kisiasa zaidi tujikinge na kumuomba mungu maana kwa hili si kwa ujanja wetu Wala watawala, Ni Allah pekee
Ndiyo maana tunasema tuna madaktari uchwara. Chama cha Madaktari ni cha kitaaluma, siyo chama cha siasa. Walistahili kutoa tamko lililosimama kitaaluma. Lakini hawa wajinga kwenye tamko lao wamejaza siasa badala ya taaluma.
 
Ndiyo maana tunasema tuna madaktari uchwara. Chama cha Madaktari ni cha kitaaluma, siyo chama cha siasa. Walistahili kutoa tamko lililosimama kitaaluma. Lakini hawa wajinga kwenye tamko lao wamejaza siasa badala ya taaluma.
Hichi si chama cha madaktari bali ni kikundi fulani cha wapuuzi wasakatonge.
Ni bora wangekaa kimya kuliko huu uozo.
 
Hawa wanashindwa kutamka moja kwa moja COVID-19 Wanazunguuka zunguuka tu mpaka message yao inakuwa too general badala ya kuwa Specific.

Ni aibu chama cha madaktari kutoa tamko kwa kutaja ugonjwa kwa kutumia alama za nukuu badala ya kutaja jina la ugonjwa husika.

Nimefedheheshwa sana na hawa wanaojiita madaktari wanaozunguuka mbuyu kupeleka message yao.

Wanasema eti ugonjwa unaosababisha "changomoto ya upumuaji" Hawasemi ni upi, Je ni Kansa ya mapafu?, Ni pumu? au upi?.

Bora wangekaa kimya tu ni hopeless kabisa hawa madaktari kanjanja
 
Covid-19 ni tatizo litakalotesa sana legacy ya utawala wa Magufuli. Wakati Ummy analishghulikia kwa nguvu, yeye alimzuia na kudai kuwa "Tanzania hakuna covid." Ingawa ni kweli kuwa lockdown haikuwa solution, kutokukukubali kuwa tatizo hilo lipo ilikuwa ni kosa kubwa sana.

Mfichaficha maradhi, kilio kitamuumbua!! ..,......... JKNyerere
 
Dr anatakiwa kusimama kwenye ukweli Siku zote na muda wote,kujielimisha kwa kadiri ya upeo wao kuhakikisha huduma bora zinamfikia Kila mhitaji bila ubaguzi wowote.Katika kujielimisha ni pamoja na tafiti za kisayansi zilizothibitishwa bila shaka yoyote.
Tunapozingatia hoja hapo juu tujiulize,Dunia yote imekumbwa na COVID na dalili zake ni pamoja na kushindwa kupumua.Hapa kwetu dalili hiyo tunaihusisha na mgonjwa ambayo ni Differential Diagnosis kama Pumu,Pneumonia, mgonjwa ya moyo nk.Lakini kwa nini Dr haututahadharishi kuwa Provision Diagnosis ni Corona Disease? Unatambua kwamba katika vituo vya kutolea huduma wanachama wenu wapo endangered kwa kiwango kikubwa kwa ukosefu wa PPE,Dawa na vifàa tiba nchi nzima?
Safety First for Front Line Fighters!
 
Asante sana madaktari wetu,tunawaombea kwa Mungu katika kutimiza majukumu yenu.
Magonjwa ya mlipuko ni vita kama vita nyingine,katika vita hii wanajeshi wa kwenda mstari
wa mbele ni ninyi madaktari na manesi,tunatambua na nyini ni binadamu mna damu na nyama kama sisi
lakini mtusaidie na sisi tunawaombea kwa Mungu ili katika kutimiza majukumu yenu muwe salama.

Idd Amini alipovamia mkoa wa kagera wanajeshi(majeshi ya ulinzi na usalama) walienda mstari wa mbele kutuokoa
Tuliendelea kuwaombea,wapo waliokufa lakini wapo waliorudi salama.Waliokufa walikufa kishujaa kwa ajili
ya taifa lao,na waliorudi walirudi kishujaa kwa ajili ya kuendelea kuilinda nchi yao,na kazi yetu sisi raia ni kutoa ushirikiano kwao inapobidi
na kuendelea kuwaombea kwa Mungu na ili Mungu atuepushe na majanga,

Viongozi wa dini,kwenye vita hii msibaki nyuma,iwe kufa au kupona,maana sisi waumini wenu
tumeiamini imani na Mungu mnayemtangaza.Hivyo tunapoumwa tukiwahitaji mje mtuombee
msisite kuja kutuhudumia,japokuwa msiache kuchukua tahadhari za kuvaa vifaa kinga n.k
Hii inatuongezea imani sisi waumini wenu,kwamba hakika Mungu tunayehubiriwa anatulinda wakati
wa shida na raha,Hivyo watumishi wa Mungu msisite kutupatia huduma za kiroho
tukiwa hai hata ikitokea tukafariki katika vita hii maana kiimani ni kwamba kuna maisha baada ya kufa.

Mungu wabariki wahudumu wa afya,Mungu wabariki viongozi wetu wa imani,Mungu tubariki watanzania wote
na ktuvusha katika vita hii,macho yetu yanakutazama wewe ili utuvushe salama.
AMINA
Zaburi.123:1-4
 
Back
Top Bottom