Ujumbe wa Eid ni Amani, Amani, Amani Mbona hawazungumzii HAKI?

Bra-joe

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,888
Reaction score
1,570
Habari Wananchi?

Hivi Hawa watu wanaohubiri kuitunza amani yetu hawaoni kwamba ni Serikali na ccm ndiyo wanaohatarisha Amani yetu kwa kung'ang'ania kukumbatia mifumo mibovu ya chagizi zetu?

Ujumbe huu wa amani Kila Kona kwa siku ya Leo nadhani ni mpango maalumu ili watu watakapokuwa wanadai haki Yao kwa nguvu waonekane wanavunja amani. Amani Haina maana kama hakuna haki.

Ni swala la muda tu, tutaelewana!
 
Watanzana walio wengi hawajui kutofautisha Kati ya AMANI NA HAKI
Mufti wa TANZANIA Ni kada mtiifu wa chama cha CCM, Chawa na mbumbu asiyejua lolote
 
Amani ni jambo jema,leo wamelichagua hilo,siku nyingine watalizungumzia hilo ulilolisema wakipenda,maana nalo ni jema pia.wala hawajakosea!
 
Hawawezi kuhubiri haki maana hawaitekelezi, ila amani kwao iko mdomoni kwani kwao amani ni uoga.
 
Mashehe ubwabwa hao.Wamevimbiwa futari.
 
Hakuna amani bila haki. Vyote viende sambamba.
 
Amani amani ili waendeleze wizi na ufisadi wao..
 
Hakuna amani bila haki. Vyote viende sambamba.
Amani ni zao la Haki, na Amani inatunzwa na Haki. Sasa tukiondoa Haki Amani itatoweka. Huko ndipo ccm wanataka kutupeleka.
 
KWA AKILI YANGU, NILIDHANI PENYE AMANI, PANA HAKI, PANA, UPENDO, PANA USHIRIKIANO, PANA FURAHA NA MENGINE MENGI MEMA HIVYO HAKI IKO NDANI YAKE.
 
Amani ni zao la Haki, na Amani inatunzwa na Haki. Sasa tukiondoa Haki Amani itatoweka. Huko ndipo ccm wanataka kutupeleka.
Upo sahihi. Wameshatupeleka huko maana wanahubiri amani pasipo haki kutendeka. Watu wanapotea, ufisadi, rushwa, kodi za wananchi zinatumika visivyo halafu mtu anakwambia tutunze amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…