nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,801
23/08/2013
JWTZ litatoa taarifa kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo, taarifa hizo zitatolewa Agosti 24.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.
Kwa Mawasiliano zaidi 0715-270136 au 0754-270136
JWTZ litatoa taarifa kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Makao Makuu ya Jeshi hilo, taarifa hizo zitatolewa Agosti 24.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi.
Dar es Salaam.
Kwa Mawasiliano zaidi 0715-270136 au 0754-270136
Tanzania Daima Jumapili limekariri msemaji wa JWTZ akikiri kuwa ni kweli mwanajeshi ametoroka lakini tayari alikuwa chini ya uchunguzi na alikuwa amekabidhi vitu vyote muhimu.
JWTZ yakanusha ofisa wake kutoroka na nyaraka
na Abdallah Khamis
JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limetoa ufafanuzi juu ya kutoroka kwa ofisa wa jeshi hilo, Luteni Kanali Colestine Serombe na kusema kuwa ofisa huyo hakufanikiwa kuondoka na nyaraka yoyote muhimu ya jeshi hilo.
Mbali na kusema Luteni Kanali Serombe hajaondoka na nyaraka muhimu za jeshi hilo, pia wamesema ofisa huyo aliyetoroka ni Mtanzania na kwamba kabla ya kuroroka alikuwa akikabiliwa na tuhuma dhidi ya makosa ya kijeshi.
Jeshi limelazimika kutoa kauli hiyo baada ya baadhi ya vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kusema kuwa ofisa huyo aliyetoroka ni miongoni mwa maofisa wachache walio na asili ya Rwanda ndani ya jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa jeshi hilo, Meja Erick Komba, alisema Luteni Kanali Serombe alizaliwa katika Kijiji cha Rukira kilichopo mkoani Kagera na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Rukira kabla ya kwenda sekondari za Rulenge na baadaye Minaki alikosoma kidato cha tano na sita.
"Ametoroka usiku wa Desemba 17 kuamkia 18 mwaka jana baada ya kuwa na makosa ya kijeshi …tulimuweka chini ya uchunguzi kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, sasa labda hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya kutoroka kwake, kwa kuwa suala la utoro ni uamuzi wa mtu kama ambavyo wengine wanaamua kujiua wakiwa na sababu zao," alisema Meja Komba.
Kuhusu madai kuwa ofisa aliyetoroka alikuwa mkuu wa kitengo cha teknolojia ya habari na mawasiliano, Meja Komba alisema hilo si la kweli na kwamba Luteni Kanali Serombe alikuwa ni mkufunzi wa wanafunzi wa kijeshi wanaosoma masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT).
Alisema kulingana na cheo cha Luteni Kanali Serombe na madaraka aliyokuwa nayo alikuwa na uwezo wa kusoma baadhi ya taarifa ambazo zilimfikia kwenye ofisi yake kwa ajili ya utekelezaji au kwa taarifa.
"Katika kipindi chake cha utumishi kwa muda mrefu alikuwa mkufunzi wa masomo ya kompyuta katika kituo chetu, kwa mantiki hii taarifa nyingi alizokuwa nazo zilikuwa ni zile za wanafunzi, yaani mahudhurio, matokeo na nyingine zinazomhusu mwanafunzi," alisema Meja Komba.
Aliongeza kuwa jeshi lilipoanza uchunguzi dhidi ya makosa ya Luteni Kanali Serombe kitu cha kwanza kilichofanyika ni kuhakikisha anakabidhi vitendea kazi vyake vyote kwenye uongozi, huku akibainisha kuwa walichomwachia ni elimu aliyonayo.
"Labda sasa anaweza kuitumia elimu hiyo huko alikotorokea kufungua chuo cha kompyuta na wananchi wakapata ujuzi huo," aliongeza Meja Komba.