Ujumbe wa JWTZ kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba

Ujumbe wa JWTZ kuhusu kutoroka kwa Luteni Kanali Coelestine Seromba

Status
Not open for further replies.
...ndo maana sikuzote nasema likagame linaweza kutuchapa tu,jiulize wangapi bado wamejificha serikalini.sasa tupo uchi mbele ya wanyaruanda,ole wetu tuwaguse tunakula kichapo kikali sana,ikowapi tiss...
Umesema kweli watu tunapiga kelele ati Rwanda ka nchi kadogo hawawezi kutuvuruga sisi taifa kubwa, lakini tumesahau Congo ni kubwa kuliko tz
 
By the way.
Huyo Mwanajeshi alitoroka tokea February kama wana JF mlikuwa hamjui..sasa kutoa Tamko leo ndo nini....
 
Kuna siku tutaanza kuona matamko ya kufupisha maneno kama cna, kw mawacliano, jsh nk.
 
Wadau,

Hivi TCRA walipokuja na zoezi la usajili wa namba na kutuaminisha kuwa ni kinyume cha sheria kwa mtumiaji yeyote hapa nchini kutumia simu pasipop kusajili, walikuwa wanatutania eenh? Tena utani wa maungoni kabisa. Namba hiyo katika waraka huu, ya 0715-270136 HAIJASAJILIWA!!

Vinginevyo, tunaweza anza kuhoji the authentisity ya the whole statement. Upuuzi wa mwisho kabisa huu ikiwa maafisa wetu tu wenyewe hawawezi tii sheria zilizopo. Kumbe inawezekana?

Nimetukana bonge la tusi.

Bazobonankira
 
Haijasajiliwa kweli.Sikutegemea JWTZ i-misbehave kwa kiwango hiki.Ingekua jeshi la polisi nisingeshangaa lakini JWTZ?No no no!
 
kaazzi kwelikweli yaani kama mpaka askari wa jeshi la ulinzi anatoroka je ni wangapi wameajiriwa kwa vyeti feki na wangapi wameolewa na askari wetu.
 
Haijasajiliwa kweli.Sikutegemea JWTZ i-misbehave kwa kiwango hiki.Ingekua jeshi la polisi nisingeshangaa lakini JWTZ?No no no!

Ben,

Trust me, huu ni udhaifu mwingine dhahiri kabisa katika usimamizi wa sheria na mamlaka za nchi. Kwa hili, naomba tuungane mkono kuhakikisha tunaona TCRA inachukua hatua stahiki kwa afisa huyu wa jeshi na wengine ambao wapo. Ushahidi wa hili ni bayana. Afisa huyu, na wengine wengi wa namna yake wanaweza kutumika kuleta madhara kwa individuals kwa kutumia namba hii na bila kuacha trace marks, who knows? Mamlaka ya mawasiliano ijitokeze itueleze kama kuna exceptions kwa makund maalum ya watanzania. Isingekuwa advantaje ya usajili, nani angejua Ramadhan Inghodu ilihusika na mkasa wa Ulimboka? Tuzilazimishe mamlaka kuwajibika. Hell no on this.
 
kuna uzembe mkubwa sana ktk vyombo vya ulinzi vya nchi hii, wanachojua na kubaka mabinti wa form6 kwenye makambi ya jkt
 
Luteni Kanali > 20 yrs ya utumishi serikalini. Upo uwezekano mkubwa Mwinyi alimpa nyota ya kwanza. Mkapa na JK walimpa nyota zilizofuata, Je TISS hawakujua? Ipo siku tutapata Rais na Mwenyekiti wa CCM Taifa, TX. Wanausalama wapo busy kufuatilia CDM, wanaharakati na kuiba mali za umma. Hii ni kashfa ya mwaka, kama ningekuwa Rais, ningefukuza kazi mara moja na kuwafungulia mashitaka ya uzembe maofisa wengi wa juu wa TISS na JWTZ
 
Umesema kweli watu tunapiga kelele ati Rwanda ka nchi kadogo hawawezi kutuvuruga sisi taifa kubwa, lakini tumesahau Congo ni kubwa kuliko tz

Usifikiri Tanzania kuna Wanajeshi kama wa CONGO! DRC wana Jeshi dhaifu ndio maana Wanyarwanda wanaingia na kutoka na madini kama wapo nchini kwao kupitia jina la m23, na hii sio mara yao kwanza kupigwa na Majeshi ya Rwanda hao Wakongo. Tanzania tuna Jeshi Imara ndio maana kabla hatujaenda kule walianza na propaganda nyingi za kijinga kwa JWTZ mara ooh TPDF isije DRC, TPDF walivofika DRC wakaanza eti ooh Majeshi ya Tanzania yanabaka raia wa Congo haraf pia wanachukua malaya wanaojiuza kisha hawawalipi ela. Toka lini kwenye mapigano mazito kama Goma kuwe na Biashara ya Ngono? Inakuwaje askari na pesa? Walivyoona haitoshi wakasema eti wamemkamata askari wa JWTZ wakati wa mapambano. Mkuu Brigedia zote zilizo chini ya UN, Mtanzania Brigedia Jenerali James Mwakibolwa akaja akasema hakuna askari wa Tanzania aliekamatwa, hao m23 mpaka sasa hawajasema lolote. Wanyarwanda ni mabingwa wa propaganda. Na kamwe hawawezi kuipiga Tanzania,
 
Labda atakuwa amempelekea Kagame data. Kama Kagame aliwatandika Banyamulenge akachukua nchi kwa nini ashindwe kuitandika Tanganyika inayoongozwa kilegelege..

Labda afanye hivyo Congo lakini sio Tanzania. Tena kwa bahati mbaya hata Congo watanzania tumeshafika na tunakata wizi wa Rwanda wa kuiba madini hapa DRC.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom