Hii inathibitisha kuwa hii nchi imewashinda hawa walio madarakani.
Hivi kweli ingekuwa hao ni wanaojitambulisha kuwa ni waandamanaji, je wasingekamatwa?
Huyu anayeitwa IGP nadhani ni bosheni tu. Huenda IGP halisi ni mafwele na wauaji wenzake ndomana wakina Mwaipopo wako na ujasiri wa kuvaa maguo ya kihalif na kujitambulisha na hakuna wa kuwafanya kitu.
Ila huyu Mwaipopo namhurumia sana. Namwona kama Musiba alosinzia. Unakuja wakat anatoka hadharani kutaka huruma ya watanzania.
View attachment 3627813
Mwl. Laurent Noti Joseph (Mnegro)* mwalimu kutoka shule ya Sekondari Ikungulyabashashi anayeshikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi Bariadi.
Nikafunga safari kwenda kituo cha polisi kumsalimia, nikiwa njiani rafiki yangu mmoja akawaa amenipigia simu nikamjulisha nipo njiani naelekea kituo cha polisi kumsalimia Rafiki na mwl Laurent Noti Joseph (Mnegro) ambaye nimejulishwa yupo kituoni hapo.
Basi rafiki yangu akaniambia tukutane tukamuone.
Tumefika kituoni hapo tukaambiwa haturuhusiwi kuonana naye, ila kama ni chakula tunaruhusiwa kumpelekea ila sio kuonana naye.
Kutokana na ushamba wetu wa kutokujua sheria tukauuliza vipi kwa upande wa mwanasheria akipatikana? Tukiambiwa hata mwanasheria/wakili kuna taratibu zake.
So hakuna ndugu, jamaa au rafiki anaruhusiwa kuonana naye.
Mimi sio msomi wa sheria, japokuwa nina sifa za kwenda Bungeni kutunga sheria, kwa maana najua kusoma na kuandika pia na kuhesabu.
Japokuwa mimi sio mwanasheria na sijui taratibu za kiutumishi zikoje. Ila hofu yangu ni kwamba huyu Mwl. Akikaa mda mrefu bila kuhudhuria kazini anaweza kukosa sifa za kuwa mwalimu. Kitu ambacho kitayumbisha hali za watu wanaomtegemea. Tukumbuke Mnegro ni mme, baba na mtoto wa wazazi wake macho ya wengi yanamtazama. Japo kuwa sijui kinachomsibu kwa maana hata jeshi la polisi halijatoa taarifa kwa umma nini Mnegro kinamsibu.
Sijajua kama umma una haki ya kupata taarifa juu ya kilichosababisha kukamatwa kwake. Maana mimi sio mwanasheria.
Nimekuwa na ushuhuda mwingi sana kwa chama cha walimu nchini kutokujali shida na changamoto za walimu wao. Mjumbe wao wanayemkata hela kila mwisho wa mwezi ety akipata shida wamsaidie yamekuwa ni maneno na hayana uhalisia. Hata kwa huyu mwl. CWT wamekaa kimya kama hawajui chochote. Pia nina ushuda wa mwl mwingine alitapeliwa akapeleka malalamiko kwao hakuna kilichofanyika.
Tangu enzi na enzi vyama vya wafanyakazi vilikuwa na nguvu za kutetea haki za wafanyakazi na kufanya mabadiliko panapohitajika.
Kwa kutumia nafasi hii naziomba taasisi mbalimbali za kutetea haki, mawakili mbalimbali wajitolee kumsaidia mwl huyu huduma za kisheria.
Ieleweke sio Gunini anasema Mnegro hana hatia la hasha! Kama amefanya kosa ahukumiwa kwa haki kwa mujibu wa sheria na taratibu tulizojiwekea.
Asanteni sana!
Gunini Masunga
Mkulima wa pamba kutoka mtaa wa Itongo Bunamhala.
Britanicca