Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
Hamuwezi kubadilisha na hamko kwenye nafasi hiyo sababu anayetoa fedha ni mmarekani. Yeye ndio mwenye mamlaka na hiyo pesa, na mamlaka hayo yamesainiwa tiliwa sahihi na serikali yako.Wanazuoni wetu na wanasaikolojia wetu wanaonaje juu ya hilo?
Na jee tuendelee kukubali uhuni huu?Je na sisi tunaeeza kuweka sharti juu ya andiko hili kulinda utu wetu?
Hatuwezi , why? Sababu wenye pesa ndio wameamua hivyo.kwa nini hatukubakia na mfumo wa zamani?
Na kwa nini tusirudie kwenye mfumo wa zamani?
Linalenga kuwaambia wananchi kuwa huo ni msaada na si pesa ya serikali.Ni sharti linalolenga nini haswa?
tukibadilisha itakuaje?unadhani haiwezekani kurejea hali ya awali kabla ya maandiko haya?Hamuwezi kubadilisha na hamko kwenye nafasi hiyo sababu anayetoa fedha ni mmarekani. Yeye ndio mwenye mamlaka na hiyo pesa, na mamlaka hayo yamesainiwa tiliwa sahihi na serikali yako.
Dawa ni moja tu, mpaka tutakapoweza kujitegemea ndio itawezekana.
Tatizo nini wenzetu wanapenda transparency sio kama Chadema ukiwaambia wekeni majina ya watu Na kiasi walichomchangia matibabu Lisu wanasepa.Wao wanaweka kibao kwa hisani ya watu wa Marekani alyechangia akienda aweza onyeshwa list nzima ya wachangiaji namba zao za simu walipo nk Chadema waambie waonyeshe hiyo list hata kama ulichangia hawakupi Na mwenye list ni mwenyekiti tu.Hakuna ulaya waweke tu hata wakijenga genge la kuuza nyanya la elfu nne.It is ok.Miaka kadhaa ya nyuma hilo andiko halikuwepo ...why now na linalenga kuachieve nini?
Nope. According to msaada uliotolewa, pesa zimeandikwa kuwa zilitoka america.hiyo ndege iliandikwa kwa "hisani ya watu wa marekani" ???
Serikali zetu haziaminiki...zinapenda sifa sana na kusema na pesa ya serikali... So ili kuondoa ukakasi huu inaandikwa kuwa ni msaada...kwani zamani ilikuwa haijulikani kuwa tunasaidiwa na marekani?
Narudia tena hamko kwenye position hiyo. Mtabadilishaje wakati makubaliano yametoka kwake, serikali iliyasoma ika sign.tukibadilisha itakuaje?unadhani haiwezekani kurejea hali ya awali kabla ya maandiko haya?
Habari za jioni wadau.
Naomba niweke wazi kuwa mimi napenda nchi kama nchi ijitegemee kwa asilimia mia moja lakini pia natambua jambo hili laweza kuchukua muda kutokana na historia ya Taifa na harakati za kidunia zilizokuwepo na zinazoendelea kutokea.
Naamini pia katika kufikia lengo la kimaendeleo bado ni muhimu kupata msaada kutoka kwa wenzetu ambao walitangulia kimaendeleo.
Naamini pia njia bora na ya kweli katika kufikia uhuru wa kiuchumi,kifikra na kimaamuzi ni kupitia jitihada za watanzania wenyewe.
UKAKASI
Nimekuwa nikisikia au kushuhudia matangazo mbalimbali haswa katika sekta ya afya ambayo yanapenda kusisitiza matumizi ya maneno haya...
"KWA HISANI YA WATU WA MAREKANI"
Kwa maoni yangu maneno haya ni ya kudhalilisha mno na sielewi mantiki ya kubandika maneno haya pindi mradi unapopata msaada wa kutoka marekani.
Wakati mwingine kamradi kadogo tu kama vile ujenzi wa choo cha shilingi milioni 5 uatakuta haya maneno yapo tu.
Naamini Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi mbalimbali lakini sijashuhudia sana maneno dhalili namna hii.
Je nia ya msaada wa marekani haiwezi kufikiwa hadi maneno haya yaandikwe?
Je kuna sheria nchini Marekani inayolazimisha maneno haya yaandikwe?kama ipo ni sheria ipi?
Je kuna vipengele vyovyote katika mkataba wa ushirikiano kati yetu na marekani kinachotaka maneno hayo yaandikwe?
Je wananchi wa Marekani wanapoteza nini maneno hayo yasipoandikwa?
Je Serikali haiwezi kuyapiga marufuku matumizi ya maneno haya ...mbona zamani tulipewa misaada na hakukuwa na aina hii ya maneno ya kudhalilisha?
Karibuni kwa mjadala.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!
Kwani haya anayofanya jiwe tulimuagiza?Je agizo la kuandika hivyo lilitoka kwa wananchi wa marekani au ni mbwembwe za watawala wa huko?