Ujumbe wa "Kwa hisani ya watu wa Marekani" Lengo lake ni nini haswa?

Ninachojiuliza ni kwamba hapo zamani tulikuwa tunafanyaje?Mbona fedha za Global fund inatosha tu kumention "GLOBAL FUND" Fedha za World bank,IMF na ADB hazina hizibmbwembwe za ajabu ajabu?
Na sio kwa hisani ya wananchi wa mataifa flani?

Hiki
 
Mleta thread, tambua kuwa budget yetu ni tegemezi kwa kwa karibu asilimia 60. miradi mingi nchini ni ya fedha za hao wahisani. Tena ni kwa niaka mingi ipo hivyo.
 
Hata dawa za kupunguza makali ya VVU ni kwa hisani ya watu Wa marekani....unaubavu Wa kukataa kauli?
Lakini ulitaka wasemeje labda badala ya neno hilo....'mradi huu umekamilika kwa kubadilishana na madini? Hii imekaaje?
 
Vodacom walikua wanadhamini ligi kuu ya Tanzania bara na ikawa inaitwa ligi kuu ya Vodacom vipi hapo ulilionaje hili? Voda wana ligi?
 
Ni sharti linalolenga nini haswa?
Jinga lao ebu tutafasirie ..."kwa hisani ya watu Wa marekani " kwa kiingereza kwanza kisha tujadili maana wenye kiswahili ni sisi...sijui mnalalamika nini mabazazi nyie
 
Mleta thread, tambua kuwa budget yetu ni tegemezi kwa kwa karibu asilimia 60. miradi mingi nchini ni ya fedha za hao wahisani. Tena ni kwa niaka mingi ipo hivyo.
Hilo nalitambua vyema na kama unakubaliana na mimi zamani tulipokea msaada kwa zaidi ya asilimia hizo ila sikuwahi kusikia maneno hayo ya kuudhi au kujijweza.
 
wapi papa msofe!, ndama mtoto wa ngombe! salum matelephone! hii ni pesa walikuwa wanawapa wanamusic ili utajwe papaaa! achana na kitu pesa!
 
Vodacom walikua wanadhamini ligi kuu ya Tanzania bara na ikawa inaitwa ligi kuu ya Vodacom vipi hapo ulilionaje hili? Voda wana ligi?
Walikuwa wanajitangaza kibiashara na hilo ni lengo linalokubalika na kueleweka.
 
Ninachojiuliza ni kwamba hapo zamani tulikuwa tunafanyaje?Mbona fedha za Global fund inatosha tu kumention "GLOBAL FUND" Fedha za World bank,IMF na ADB hazina hizibmbwembwe za ajabu ajabu?
Na sio kwa hisani ya wananchi wa mataifa flani?

Hiki
Niliwahi kuuliza the same question maana hawa jamaa huwa wakali sana wakati wanapokuja kutembelea miradi huko field.... Mfano wakikuta mme print T-shirt, kofia, even slides presentation without acknowledging aisee inakuwa bonge la issue. Program officer wa nchi moja (ambaye fortunately alikuwa mbongo mwenzetu) akasema ni madharti ya nchi zao na kila siku yanabadilika, eti pia ni njia ya kuhakikisha pesa inatumiwa as intended.
 
Je agizo la kuandika hivyo lilitoka kwa wananchi wa marekani au ni mbwembwe za watawala wa huko?
Sio mbwembwe bali ni halisi!
Watu wa Marekani/wananchi wa Marekani ndio walipa kodi ambazo tunapewa misaada sisi.
Nchi zenye viongozi ambao wanawajali wananchi wao hawafanyi vitu kwa kujitafutia sifa wao kana kwamba viongozi ndio watoa misaada, ndio maana viongozi wao wakifanya mambo ya kipumbavu wananchi wao huchukua maamuzi mara moja wakisaidiwa na vyombo vyao vya ulinzi

Ingekuwa tanzania ndio inapelekea misaada kule, wananchi wa Marekani wangesikia matangazo ya "hii misaada ni kwa hisani ya rais Magufuli".
 
wapi papa msofe!, ndama mtoto wa ngombe! salum matelephone! hii ni pesa walikuwa wanawapa wanamusic
mimi nahisi chanzo cha maneno haya mabaya watakuwa ni wabongo wenzetu wenye hulka ya kunyenyekea hata pasipostahili.Nimewahi kupokea misaada kadhaa kutoka kwa wamarekani nadhani wanachohitaji ni recognition kimaandishi zaidi mfano ni kuwaandikia appreciation letter ambayo atarudi nayo kuionesha huko alipochangisha fedha ili kujustfy matumizi na kuombea mchango zaidi.
Hii hoja ya kwamba usipotamka au kuweka maneno hayo wanachukia ni hoja potofu na haina ukweli wowote.Huu utumwa mbaya upo sana wizara ya afya na sijaweza kumjua aliouanzisha....
Nadhani ile nembo ya USAID inatosha sana kutoa ujumbe husika hizi mbwembwe za hayo maandiko hazina mantiki yoyote.
 
kwa nini hatukubakia na mfumo wa zamani?
Na kwa nini tusirudie kwenye mfumo wa zamani?
Wangebakia kama zamani angetokea dikteta mmoja akitoa msaada wa watu wa marekani angesema msaada katoa yeye.

Hujawahi kuona kodi za watanzania zinapelekwa sehemu kufanya maendeleo lakini vinatokea vidudumtu vinasema "jiwe katoa hela"?

Wenzetu wamepiga hatua kukwepesha ubabe kama wa "sipangiwi, sijaribiwi"
 
Ina maana haya maandiko yanatumika ndani ya udongo wa marekani?
 
zamani fedha hizo zilikuwa zinatoka wapi?mbona hakukuwa na maneno haya?
Siku zote ombaomba akizidisha kuomba, mwombaji anaanza kumkejeli hadharani

Hata wewe ukianza kuwa tegemezi kwa ndugu zako siku za mwanzo hawatoongea sana.
Ukizidi kuwa tegemezi wanaanza kukukejeli hadharani wakikuita majina inayostahili kuitwa
 
Kuna haja ya kuendelea kuwa na udhalilishaji huu ambao hapo nyuma haukuwepo?

HII NI SAWA NA KAULI ZA KEJELI ZA MH.RAIS MAGUFULI KWAMBA "SERIKALI YANGU.UONGOZI WANGU, NA KEJELI MBAYA ZAIDI NI ZA MPAMBE WAKE PAUL MAKONDA "DA ES SALAAM YANGU"!USIHOJI YA WAFADHILI WANAOTUSAIDIA KWA KODI ZAO HOJI KWANZA DHARAU,KEJELI NA UDHALILISHAJI UNAOFANYWA NA ULIOWAPA KURA NA WANAKULA KODI ZETU!
 
Hao Wamarekani wanaheshimu kodi za raia wao, na huo msaada umepatikana baada ya raia kukamuliwa kodi.Kwa hiyo lazima serikali iheshimu kodi za wananchi wao, usifafanishe na nchi yako ambapo viongozi hawaheshimu kodi wanazokamuliwa wananchi wao na badala yake hujiona fedha ni za mifukoni mwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…