Julias Vimvinyira
Senior Member
- Jun 2, 2025
- 155
- 205
Ndugu wapendwa katika Kristo,
Ni nani anayeweza kujidai kuwa na mamlaka ya pekee ya kuifahamu kweli yote ya Mungu? Ni nani anayeweza kudai kusikilizwa kwa sababu ya utakatifu wa nje, huku moyo wake ukiwa mbali na upendo wa kweli wa Kristo?
Tunasikitika na kutafakari kwa uchungu juu ya majeraha ya kihistoria ambayo yameacha doa kubwa katika dhamiri ya wanadamu. Tukio la mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, ambapo zaidi ya ndugu zetu 800,000 wengi wao wakiwa Watutsi waliuawa kwa ukatili mkubwa, linaendelea kutukumbusha wito wa Kristo wa kuwa vyombo vya amani na upendo.
Katika mazingira hayo ya giza, baadhi ya watumishi wa madhabahu hata maaskofu na mapadre walishindwa kuwa taa katika giza, wakachangia au kukaa kimya mbele ya uovu.
Wapo waliogeuza nyumba za ibada kuwa maeneo ya utekaji na maangamizi. Wapo waliokimbilia makanisani wakitarajia kupata hifadhi, wakiliomba sala ya Mtakatifu Francisko wa Assisi “Ee Bwana, nifanye kuwa chombo cha amani yako” lakini hawakupata amani hiyo, bali mauti iliwakumba mikononi mwa wale waliopaswa kuwalinda.
Ni huzuni kubwa kusema kuwa Padre Athanase Seromba, mmoja wa viongozi wa Kanisa Katoliki, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa kwa kushiriki katika dhambi hiyo ya mauaji. Hili halikuwa kosa la mtu mmoja tu, bali ishara ya mapungufu ya taasisi nzima kushindwa kuamka na kulinda utu wa mwanadamu.
Si Rwanda tu. Katika vita vya Balkan baada ya kuvunjika kwa Yugoslavia, tulishuhudia namna ambavyo makanisa, hususan Kanisa Katoliki nchini Croatia, yaliingia katika siasa za utaifa zilizochochea mgawanyiko wa kikabila na kidini. Badala ya kuwa madaraja ya maridhiano, baadhi ya makanisa yakawa ngome za itikadi kali, chuki, na maamuzi ya kikatili dhidi ya wale waliokuwa tofauti na wao.
Mwandishi na mtafiti Michael Sells alielezea haya kwa kina katika kitabu chake The Bridge Betrayed namna ambavyo tulishindwa kuwa daraja la amani, tukawa sehemu ya mfumo wa uonevu kwa kivuli cha haki, demokrasia, na uzalendo.
Ndugu wapendwa, haya ni majeraha ambayo bado yanahitaji uponyaji. Lakini pia ni onyo kwa vizazi vya sasa. Taifa letu Tanzania linapokaribia uchaguzi mkuu, yapo maneno yanayotamkwa katika majukwaa ya dini ambayo yanatoa harufu ya chuki, ya uchochezi, na ya uzushi usio wa Kristo.
Huu si wakati wa kuigiza utakatifu huku mioyo yetu ikitafuta utukufu wa dunia. Si wakati wa kutumia madhabahu kama jukwaa la kujijenga kisiasa au kijamii.
Wale wanaotumia jina la Mungu kueneza chuki, wakiwasha moto wa fitina kwa kivuli cha haki au haki za binadamu hao si sauti ya Kristo. Bwana wetu Yesu Kristo hakupigania haki kwa upanga, bali kwa msalaba. Hakuwahi kuchochea ghasia, bali alitufundisha kusamehe sabini mara saba.
Tusiwaruhusu “Athanase Seromba” wa nyakati zetu kupenyeza roho ya uharibifu katika taifa letu. Tuwapime viongozi wa dini kwa tunda la roho zao, si kwa mavazi yao au maneno yao matamu.
Kwa hivyo, Watanzania wenzangu, tumuombe Mungu atupe hekima, utuongoze katika amani, na atujalie kuwa chombo cha upatanisho si chanzo cha machafuko.
Katika Kristo tumaini letu,
Mwenye upendo na maombi