Wewe mtoa mada usijifanye kuwa unajali uhai wetu sana wakati Ben Saanane hakuingia maandamano yoyote na mlimuua.
Anzori Gwanda hakuwepo kwenye maandamano na mlikwishamuua,masheikh wa Rufiji na wengi wengineo waliookotwa mitoni na kwenye fukwe za bahari.
Tunajua kwamba,tukiandamana mtatuua lakini hamtatuua wote na ata tukiacha kuandamana,huyu Nduli atatuua kwa njia yoyote ile.
Basi hatuna budi kuandamana kwa sababu kifo kitakuja tu vyovyote iwavyo,iwe mkituua tutakufa ama hata Mwenye Mungu akitaka tutakufa.
Hata ninyi mnaotuua hamk salama kiviile,aidha huyu muuaji atawaua ama pia mtakufa wakati wenu ukifika. Na yeye pia atakufa,ama pia atafia kifungoni.
Ushauri wangu ni huu...TENDENI HAKI,hilo tu basi mtakuwa salama,wananchi watakuwa salama,na hayo maendeleo mnayoyanadi yatakuja kwa usalama.