KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Baada ya kusoma habari hiyo, ni wakati sasa wa kuamini kwamba UK kaingia kwenye mtego wa Urusi na inaweza kuwa ni nchi ya kwanza na ya mwisho kutupiwa bomu la Nuclear kutoka Urusi.
Kuitambua Wagner kama kikundi Cha kigaidi maana yake ni kwamba:
1) watataka kuingia mpaka ndani ya Urusi kuwasaka Wagner ambao wamewatambua kama magaidi ,je Urusi watakubali?
2) Tumesikia Wagner wapo Belarus na Belarus ni mshirika mzuri sana wa Urusi, Je, UK wakitaka kuwatafuta Wagner ndani ya Belarus,Urusi atakubali?
3) Kama kikundi hicho kina ushirika wa Kremlin kama inavyodaiwa lakini Kremlin imekuwa ikikataa Hilo, kutaka kukivamia maana yake ni kutaka kupambana na Urusi, je Urusi watakubali?
4) Kwa tafsiri rahisi ni kutaka kulibrand Taifa zima la Urusi kama magaidi, Je Urusi watakubali?
Hebu fikiria zaida, kama Urusi asipokubaliana na hayo na akaona usalama wake unahatarishwa ,unadhani ni Nini kitatokea?
Urusi atajibu na atajibu Kwa mapigo mazito na hapa ndio tutaona Urusi ikitumia silaha nzito za maangamiza kama Nuclear Kwa sababu UK ni ' formidable foe'