Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Dua.. inafurahisha unapojaribu kujenga hoja kwa kutumia maneno mengi na hivyo kuficha ukweli kuwa hauna hoja! Nikianza kukujibu tena.. nitakuwa najirudia! Ukijitahidi kumwonesha kipofu mbalamwezi na akang'ang'ania kuwa ule si mbala mwezi ni jua wakati haoni.. utapoteza muda!! Hivi kuna mtu humu ambaye haelewi kuwa Mbunge alikuwa anazungumzia kesi ya huyo dada kwa vile ni mwanamke? Kama ni ukabila mbona hawakutaja kabila la huyo dada? Kama alikuwa anazungumzia ukabila TRA ulijuaje alikuwa anazungumzia ukabila wa "wachagga" na siyo kabila jingine? You have already made your decisions, now find the evidence to support it.. while I look at the evidence and make my decision!
 
Sawa endelea kuangalia mbalamwezi wakati jua linawaka.
 
Nimekuwa msomajii mzuri wa hii mada tuko ilipoanza. Ama kwa hakika pande zote mbili zimetoa hoja nzito na uhakika na ni vizuri mada ikaendelea for an indefinately period kwani the more we discuss the more we r unearthing valuable information.

Hili la majadiliano na Mrs Nagu halina maana kwani hawa watu wanafanya kazi ktk kile wanachoita " Collective responsibility" hatutegemei mama Nagu aje aseme kweli kuna ukabila TRA in a way atakuwa naishambulia the very government to which she took an oath. Afterall Nagu mwenyewe she is belong to the same group Mswahili anawaita Northerners!

Back to the mada, nakubali kuwa kuna tatizo la ukabila TRA. Hizo hoja za Historia ni upuuzi mtupu kwanini tunakuwa watumwa wa historia? mbona baada ya Uhuru kuna nafasi ziliendelea kushikwa na wazungu na baadae tukaja wenyewe. Haya mazingaombwe ya historia hayana mashiko.

Tatizo letu watanzania maswali magumu tunayapa majibu rahisi matokeo yake rabsha. Sisemi haya kwa kuwa natoka kanda ya ziwa lakini ukweli na sisi tuna haki ya hiyo national cake jamani
 
dua wrote: jokaKuu
Huyu mbunge aliisha anza kusakamwa kwa EMS na mengine ambayo hakuweza kusema, je unafikiri alikubali kwa hiari yake? .

....there you go again. unapotosha unapodai Mbunge alikuwa anasakamwa kwa EMS. Barua iliyotumwa kwake kwa EMS ilikuwa ni barua iliyoandikiwa huyo mama aliyeachishwa kazi. TRA wali-forward barua hiyohiyo kwa Waziri wa Fedha, na kwa mbunge wakitumia EMS.

Sababu za TRA kumtumia mbunge barua hiyo ilikuwa ni kutaka kuwa wawazi na kushirikisha pande zote zilizohusika na suala la huyo mama.

Mimi naamini Mbunge hakuwa amefanya utafiti wa kutosha ktk suala hili. Inaelekea hakulichunguza suala hili tangu mwanzo wake yeye ameingilia tu akishinikiza "hukumu" ya waziri wa kazi itekelezwe bila kuangalia implications za utekelezaji wake.

Dua wrote:
Hivi uliona wapi ulimwenguni mtu anapewa compensation wakati hakuna hatia? Tupe mfano naona wengi watajumuika kupata hizo pesa za bure

Dua, mimi nadhani umeelemewa chuki yako kwa wachaga kiasi kwamba unashindwa kuona mtiririko wa hoja ulioko ktk majibu ya Waziri wa fedha[mchaga]. Mbunge mwenyewe amekiri kwamba alikosea.

Sasa kwenye hilo suala compensation, na madai yako ya kupuuzwa kwa maelekezo ya waziri wa kazi.

Hiyo compensation naiangalia kama implication ya maagizo ya Waziri wa Kazi. TRA sasa walilazimika "kumuachisha" kazi huyo mama na kumlipa hiyo compensation, na siyo kumfukuza bila mafao yoyote.

SHERIA YA KAZI TANZANIA inaelekeza kwamba mwajiri atashindwa kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Kazi ya kumrejesha mtumishi kazini, basi anapaswa kumlipa mshahara na mafao yake ya mwaka mmoja.

Sasa "siri" ya compensation hii hapa: 1. mwibie mwajiri wake ili ufukuzwe kazi 2.tafuta mbunge na waziri akutetee 3. nenda mahakama ya kazi hakikisha kwamba inaamuliwa "uhurumiwe," mwajiri atakulipa mshahara wa mwaka mzima!!

Dua wrote:Mimi sijaandika waziri na wanasiasa hayo ni maneno yako. Wanasiasa hawakusemwa kwenye kile kifungu cha sheria, ni Waziri tu ambaye anazarauliwa na Commissioner wa TRA.

wewe Dua kwasababu ya chuki zako unaona hiyo ni dharau ya Kamishna wa Kichaga dhidi ya waziri wa serikali ya Jamhuri. Chuki yao inakufumba usiangalie upande wa TRA.

Huyo mtumishi aligushi nyaraka za TRA/Serikali na kusababisha serikali ipoteze mapato. Sasa kurudhishwa kwake kazini huoni kwamba kungewavunja moyo watumishi waadilifu wa TRA?

Huyo mama hakufukuzwa kazi peke yake, bali pamoja na mtumishi mwingine waliyeshirikiana. Kama TRA ingetelekeza hukumu ya mahakama ya kazi, basi ili kutenda haki ilipaswa kumrudisha na mwenzake huyo mama.

You may not agree with TRA's decision, but you can not fail to understand why they proceeded in a manner that they did.
 
Bazee,
Sikufanikiwa kuona mahali/pahali? ambapo mbunge (kwa kumbukumbu zangu nilidhani Mhe Ibrahim Marwa (as he then was)) alitoa madai/tuhuma/shutuma za ukabila katika asasi zilizo Wizara ya Fedha. Hata hivyo, bado naamini kuwa suala la "madai" ya ukabila lishazungumzwa bungeni, si mara moja, si mara mbili.

Kwa mfano Mhe Lucas Selelii amewahi kuzungumzia kuendelea kutokuwepo kwa uwiano wa maendeleo, na huenda upendeleo wa dhahiri, kwa baadhi ya maeneo nchini, kunakofanywa na serikali kupitia bajeti yake na mipango ya maendeleo. Wakati huo huo, Mhe Selelii alionesha kukerwa kwake na wale ambao hutuhumu wale wanaoonesha shaka hii kuwa "wakabila"!

Nimeona sehemu kama mbili hivi (angalia pia sehemu zinazohusu mikataba ya madini, wanasheria "wetu", hoja ambazo hujadiliwa humu mara kwa mara):
"...Mheshimiwa Spika, lakini Nishati na Madini katika mambo ambayo ni mabaya, ni wenye Mikataba hii ya wachimbaji wakubwa wakubwa. Ni mabaya kupindukia. Nadhani kama ni dhambi kubwa ndiyo kwenye dhambi, mimi nawalaumu sana na kwa kweli nawalaumu Wanasheria wetu wa nchi hii. Kwa kweli nitaendelea kuwalaumu Wanasheria wetu wa nchi hii kwa sababu wanatuingiza kwenye Mikataba ambayo haina maslahi ya Taifa na tunapokuja kusimama kusema, wanaanza kusema tunazungumza mambo ya kisiasa. Sisi tumeanza kulalamikia Mikataba hii ya Madini mwaka 1998, Mheshimiwa Kahumbi yupo hapa ni shahidi. Serikali ilikuwa inasimama inasema kwamba ninyi mnaleta ukabila, nyinyi mnaleta ukanda, nyinyi sijui mnaleta kitu gani, lakini mbona Mheshimiwa Rais Kikwete sasa hivi anazungumza hamumwambii? Ndiyo! Ilikuwa haki yetu! Mimi wa kwanza kuwalaumu Wanasheria. Kwa kweli ifikie mahali tuwawajibishe kwa jinsi ambavyo wanalipeleka Taifa letu kubaya. Sasa hivi tuanze kurudia Mikataba hii, lakini nchi hii imeporwa raslimali yake yote bila manufaa kwa wananchi wetu. Sisi tunaotoka kwenye maeneo ya madini tunaelewa. Sisi tunaotoka maeneo yenye wachimbaji wakubwa tunaelewa..." (17 Julai 2006).
Link:http://www.parliament.go.tz/bunge/ContrLst.asp?Menu=Contr&PTerm=2005-2010&vpkey=1226&page=4

Na nyingine:

"...Mheshimiwa Spika, napenda tu kutahadharisha kwamba, mimi natoka Kanda ya Magharibi na katika hilo, sioni aibu wala sisiti kutetea Kanda ya Magharibi, hasa kwa upande huu wa miundombinu.

"...Mheshimiwa Spika, barabara zilizopo kwa kweli hapa uzalendo umenishinda, chukua barabara ya kutoka Manyovu kwenda Mwandinga, kule kwa ndugu zetu wa Kigoma, imepangiwa kwenye vitabu vya fedha shilingi bilioni mbili. Ukichukua barabara ya kutoka Ipole kwenda Mpanda, imepangiwa shilingi milioni 600, ukichukua barabara ya kutoka Nzega kwenda Tabora, imepangiwa shilingi milioni 500, ukichukua barabara ya kutoka Sumbawanga kwenda Nyakanazi shilingi milioni 500. Kuna barabara moja, juzi jamaa zangu wale wa Mwanza walilalamika sana mpaka wakawa wanaandika kwenye magazeti, tumewapangia fedha, hazimo humu kwenye kitabu cha hotuba, hakuna na hata kwenye kitabu cha fedha, ile barabara ya Usagara kama sijasokea sana, hakuna.

Mheshimiwa Spika, lakini iko barabara ya kutoka Marangu - Tarekea imepangiwa shilingi bilioni 17. Jamani hivi nchi hii hii moja, barabara moja tu, tena barabara ile ni kama vile kutoka Urambo unakwenda Kaliua, inapangiwa shilingi bilioni 17. Barabara nyingine shilingi milioni 500, nyingine shilingi milioni 300 na nyingine zero; maana yake nini? Hapo ndipo nimenichanganyiwa, kweli uzalendo umeshinda.

Mheshimiwa Spika, ningeiomba Wizara hebu tutende haki, tunaelewa kabisa vipaumbele mnavyo vingi, tunaelewa kabisa sungura ni huyo huyo mdogo, hilo tunalijua, lakini tutende haki twende angalau kikanda. Unapozungumzia Kanda utataja Magharibi, unapozungumzia Kanda utataja Kanda ya Ziwa, unapozungumzia Kanda utataja Kanda ya Kusini ya wakulima wa korosho, ndiyo kanda hizo. Lakini unapozungumzia kutoka Tarekea kwenda Marangu, hivi jamani hiyo ndiyo haki?..." (3Julai 2006)
Link:http://www.parliament.go.tz/bunge/ContrLst.asp?Menu=Contr&PTerm=2005-2010&vpkey=1226&page=10

Hapo alikuwa "akipambana" na Mramba (wakati huo akiwa Waziri wa Mindombinu) kuhusu kutenga fedha nyingi kwenye barabara hiyo ya "kaskazini".
 
mwanagenzi... unaweza kuamini chochote kile.. kuna watu wanaamini kuwa mwezi umetengenezwa kwa cheese! kama mtu kutaja neno ukabila kunafanya mahala kuwa na ukabila basi tuna kazi! Katika maelezo aliyotoa Dua ya mbunge, huyo mbunge alikuwa anazungumzia kufukuzwa kazi yule dada kwa sababu ya ukabila au kwa sababu ni mwanamke? labda mimi ninasoma maelezo mengine.
 
Mzee Mwanakijiji

Mimi najiondoa katika hayo mahojiano nafikiri ni vizuri kwa mapendekezo yangu washirikishwe jokaKuu na Phillemon Michael ili mahojiano yawe mazuri zaidi na yenye mafanikio.
 
MWANAGENZI,
nimepitia hotuba ya bajeti ya waziri mramba na nikakuta kwamba barabara ya sumbawanga-nyakanazi iko ktk hatua ya UPEMBUZI YAKINIFU. vilevile nzega-tabora iko katika hatua ya USANIFU. barabara ya kuelekea tarakea iko ktk UJENZI tangu mwaka 2003 wakati waziri akiwa John Magufuli. naamini hiyo ndiyo sababu kuna tofauti kubwa kati ya fedha zilizoelekezwa kwa miradi hiyo mitatu inayolalamikiwa na mbunge.

hizi kauli za wabunge wakati mwingine ni za KICHONGANISHI. kauli hizo zinaichonganisha serikali na wananchi wake, na zaidi mawaziri na wananchi. swali la kujiuliza ni kwanini Mbunge ashambulie barabara ya tarakea pekee na siyo barabara nyingine zilizopewa fedha nyingi kuliko hizo za sumbawanga na tabora?

DUA,
Dua wrote:Mzee Mwanakijiji,
Mimi najiondoa katika hayo mahojiano nafikiri ni vizuri kwa mapendekezo yangu washirikishwe jokaKuu na Phillemon Michael ili mahojiano yawe mazuri zaidi na yenye mafanikio.

Dua sasa unatushangaza kidogo. unakuwa huwatendei haki wale wanaoamini kuwa wachaga wanadhulumu haki ya watanzania wenzao ktk ajira huko TRA.
mawazo yangu na ya phillemon kwa vyovyote vile yatakuwa yanawakilishwa na hao jamaa wa TRA.

Mwanakijiji,
1.Nilimuomba Dua alete majibu ya Waziri wa Fedha kwa hoja ya huyo Mbunge. Dua alikataa katakata. Sasa ukienda kusoma majibu hayo, utaelewa kinachoendelea hapa.

2.ili mahojiano yanoge labda ungemtafuta huyo Mbunge aliyekuwa anamtetea mtumishi wa TRA. probably kuna habari za ndani ya TRA ambayo anazielewa.
 
Joka Kuu,
Nashukuru...sikusudii kuingia kwenye mjadala au ubishi zaidi kuhusu hili, lakini kama maelezo yako ni rahisi hivyo nadhani Mramba asingeshindwa kusema hivyo na mambo yakaisha siku hiyo. Nasema hivyo kwa sababu bahati nzuri wakati wa kikao hicho niliweza kufuatilia mjadala. Kwa kweli, Mhe alikuwa na wakati mgumu sana kujitetea. Nakumbuka ilifika wakati Mramba akajikanyaga kupita kiasi ikawa anasoma takwimu ambazo hazipo; kila akiulizwa anabadilisha takwimu; Meghji na Magufuli wakajaribu kumsaidia lakini wapi. Nadhani kuna barabara moja ya maeneo ya Nzega au Shinyanga ama haikutengewa pesa kabisa au ilitengewa kiasi kidogo sana, chini ya milioni. Mramba mwenyewe alishindwa kusoma hizo takwimu akasema "I can't read this..." zaidi ya mara moja; bunge likacheka, na mawaziri wengi wakawa wanashangaa. Selelii alikuwa ametishia kuondoa shilingi na ilibidi hekima ya Spika itumike la sivyo hoja isingepita.

Tuendelee na mengine...
 
hata mimi hili suala la Majadiliano sidhani kama litasaidia sana kusolve hili tatizo just tutakuwa tunarudia rudia tu yale yale yaliyokwisha zungumzwa hapa.

nadhani linaloweza kusaidia ni kuishindikiza serikali kuunda tume huru kufanya uchunguzi juu ya haya malamiko. Though niliwahi kusikia kuwa serikali iliwahi kuambiwa juu ya hili suala (la kuundatume) lakini haijachukua hatua yoyote, lakini hata hivyo tusikate tamaa tutumie njia nyengine ya kuishindikiza. kwa mfano, naamini humu kwenye JF kuna watu wanainfluence na wabunge, so watumie uwezo wao kuwaconvice ili jambo hili kuzungumzwa kwa uwazi bila ya kuoneana haya.
 
#25 16th March 2007, 08:06 AM
Mtipula
Junior Member Join Date: Wed Feb 2007
Posts: 6
Rep Power: 0




--------------------------------------------------------------------------------

Mimi sina tatizo na Mchagga kuwa mkubwa wa kampuni au taasisi fulani mradi anachapa kazi zake vizuri na kwa uadilifu. Tatizo la Dr. Kimei ni mkabila wa wazi na mifano iko mingi. Ukiangalia leo CRDB, ameajiri wachagga wengi si kwa msingi wa sifa zao bali ni kwa sababu ya uchagga wao. Hata alipokuwa BoT, alikuwa akiendekeza sana uchagga na ailhakikisha kwamba anatoa upendeleo wa wazi kwa wachagga kwa kuwapa madawati amabyo anajua yako lucrative. Yeye mwenyewe amekuwa akisema wazi kwamba yeye uchagga hautamtoka, akimaanisha tabia yake ya upendeleo unaotokana na tribal inclination. lakini analo tatizo lingine la kupenda sana warembeo na kuwapendelea wale ambao ana mahusinao naoa hata kama kufanya hivyo kutaharibu kazi au sifa ya taasisi. Wale walio CRDB wanafahamu na hata wale waliokuwa wanafanya naye BoT wantakuwa mashahidi wa udhaifu wake huo. Kwangu mimi Dr. Kimei ni kielelezo cha watu wanoirudisha nyuma Tanzania kwa kudhani kwamba makabila mengine hayana watu wenye sifa za elimu na utendaji bora wenye kuleta tija na sifa.
 
Hayo majadiliano hayatoleta ufumbuzi wowote ni kupoteza wakati tu
 
Mwanakijiji.

Kittlya,Mramba umewapata? na Lauwo kumtumia mdogo wake kwenye mizigo michafu, nataka niwabane sana na maswali kwani mzizi wa ukabila aliyeuweka ni Mramba.
pia Benny Lusege(mhanga wa ukabila TRA) usimkose.
nakusikiliza mwanakjj. lete vitus.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…