Mswahili, kabla sijajibu hoja yako nikuhakikishie jambo moja nalo ni kuwa wewe kutoamini maneno yangu hakuniathiri mimi kwa namna yoyote kwani sina uwezo wa kutawala imani za watu. Pili, kama una namba nyingine zaidi ya ile ya ofisini nipitishie na jitihada zangu zitaendelea. Tatu, inasikitisha kuwa umeacha safari yako kwa kusubiri mahojiano ambayo hayakupangwa tarehe wala muda.