Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Dar si Lamu.. hivi kuna Wazaramo wangapi Tanzania? na kuna Wachagga wangapi? clue: angalia mwanzoni mwa mada hii....

mzee mkjj,

niaje mzee,sasa wewe unanifanyisha research wakati ukijua mambo haiko clear kama swali yangu ilivyokuwa! au unataka kuniambia nimelipua na namba ipo[at least approx.].

ama sijakuelewa...si unajua lugha ya kijijini na huku mjini haifanani[joking,but true!lol]

unataka kusema kuwa wazaramo ni endangered species? au una maana wachagga wako all over na sie watu wa pwani,especially wazaramo tuko pwani tu.

anyways...sijakupata fresh yaani! swali langu lilikuwa tuna wangapi tra[ukiachana na quoting yako ya mwalimu jkn]
 
JF members...asanteni sana kwa ukaribisho wenu.

mswahili and OTHERS....mie nafikiri mada ya TRA ifungwe TUKUBALIANE TUSIKUBALIANE undugunization etc upo hamna,twende ktk kitengo chengine labda mie nianze kuchokoza ukumbi ktk kitengo cha IKULU.

suala kubwa hapa labda tuliangalieni anapokuwa RAIS wa DINI FULANI jee ile chains nzima (hapa nakusudia watendaje wakuu kama idara ya usalama,jeshini,mabalozi,mawaziri sehemu idara nyeti etc)wanayomfuata wanakuwa wa dini yake au anaMIX?niliwahi sikia kuwa MUUNGWANA kuwa baada ya kupata USHINDI WA SUNAMI alipitisha jina la VP na hakupenda kufanya kazi na huyu wa sasa lkn hizo habari hazina uhakika,jee MUUNGWANA alichagua jina la MEMBE?

kipindi cha mzee RUKHSA pale ktk baraza lake la mawaziri kulikuwa na wa-znz wengi tu kama akina mar diria,amina salum,juma hamad omer,alli ameir etc,jee aliteua kutokana na USOMI wao?au issue ya MUUNGANO lazima sura za wa-znz ziwemo ktk baraza la mawaziri,au kwa sababu mzee rukhsa alikuwa anatokea znz?jee ni kweli kipindi kile sura za watendaji wakuu serikalini DINI FULANI walikuwa wengi kuliko?..............generally tuangalie kuwa UKABILA IKULU lkn hapa tuengeze kitu chengine JEE KUNA UDINI IKULU? naomba kutoa hoja,karibuni JF makini tujadiliane kwa amani.TUPE DATA za wakati wa mzee rukhsa,then akaja MKAPA na sasa tunaenda na mzee MUUNGWANA.

kwa wale wanaosherehekea PASAKA basi nawatakia PASAKA NJEMA na akina cc tuliobakia NAWATAKIA IJUMAA MUBARAK.
 
Mzee Engineer,

Heshima mbele mkuu, binafsi ninalewa kuwa rais wa nchi yoyote duniani ni lazima aijweke karibu na the royals, wale ambao watamtumika kwa utiifu na kwa imani kubwa kwake na mawazo yake,

Tanzania sina uhakika sana kama marais wetu wamejikita sana kwenye hilo, ndio marais wetu huweka watu wao lakini sio mbaya sana kama nchi zingine duniani, unless kama kuna wenye mifano hai!

Maana sasa hivi sioni Muuugwana kuwaweka watu wake Ikulu, lakini ninafikiri hii ni open debate na kuna wenye kuwa na mifaano hai, ila personal bado kila nikiangalai marais waliowahi kututawla silioni kuwa ni tatizo kubwa kwetu!
 


hata ungekuwa wewe mhandisi moh'd ungepanga timu yako!hilo li dhahiri!

sijawahi kuona kiongozi anayefanya kazi na watu asiowaelewa vizuri au ambao hajatoka nao pahala[labda kama ana mkubwa wake anayempangia timu hiyo]. kwani kufanya hivyo ni kutaka kusalitiwa,kazi kutokwenda[au kwenda,au?],kuanza kulaumu watu[kumbe ndivyo walivyo nawe huwajui] na kadhalika!

ni kazi sana kujaribu ku-balance masuala ya dini katika timu na kadhalika. kwanini?wakati mwingine mtu atakayekufaa au anayafaa kwa nafasi fulani anaweza asiwe wa dini unayoitaka[kui-balance,au?]na umebanwa kwenye kona ya utendaji[kama unavyoamini] hivyo huwezi chukua second rate!

halafu,ukiwa mtu wa watu utakuwa na wapambe na wenza wa dini tofauti,hivyo utakuwa na timu ya watu tofauti na hakutakuwa na suala la ku-balance sababu....huuoni huo udini,kwani we si mdini!

angalia background za viongozi utaona na kufahamu picha ya timu yao itakavyokuwa....hilo linatabirika kabisa! kama alizungukwa na wakristo wengi ilihali yeye ni muislam basi watu wake wengi watakuwa wakristo,na kinyume chake ni sahihi!

hata huyo mswahili....akiwa kiongozi hawezi kuwa mdini...mbwembwe zake tu humu![au fikrani kwake labda]kazungukwa na watu wa kila aina na atawahitaji wote,muda ukiwadia[sisemi mswahili atakuwa au atagombea nafasi yeyote ya uongozi,sifahamu!]
 
Injinia Mohamed.

Hatuwezi kuzichambua data za Ruksa,BWM na Muungwana huku muasisi wa UDINI Mwalimu Nyerere tukamsahau. tuanze na data za udini za nyerere. hadi ukabila wake.

hapo utakutana na kina Apiyo,Nyirabu charles,Warioba. Wassira na kundi kubwa la ukristu. wizara kama za elimu ilikuwa haramu waislam kushika.
masheikh na wazee wa mjini wakawa wanakamatwa na kutiwa jela hakuna padri au kanisa lililowahi kuitisha misa ya maombi ya kuwaondoa wakoloni kazi hizo zilikuwa zinafanywa na masheikh tu wao walikuwa na uchungu wa kujitawala. lakini baada ya uhuru kwa ubaguzi wa Mwl na chuki za kidini akawaadhibu wazee wetu waliomfundisha jinsi ya kuvaa suruali.
ilikuwa mwiko kwa mapdri kwenda kinyume na wakoloni kwani ni kuliendea kinyume kanisa.

Dar-si Lamu.

mimi sina ubaguzi na wala sitaki upendeleo ila nataka haki sawa kwa wote, mtu akiwa na uwezo apewe kwa uwezo wake, kukuthibitishia hilo wazee wangu hawakuona taabu wala kinyaa kumpa madaraka mzee makaputula (nyerere) na wakampata kila support. kama wazee wangu walikuwa fair ujue nami niko fair. ila pale wanapoona watu wajinga ndio mimi hupatwa na hasira sana.
 
mswahili, hivi ukipewe uongoze mahala ambapo kuna wachagga 10 na watanzania watatu utafanyaje?
 
sijakuelewa? unakusudia wachagga si watanzania, au una lako unalitafuta kwa mswahili?

mie simo mkjj yatayokukuta
 
sijakuelewa? unakusudia wachagga si watanzania, au una lako unalitafuta kwa mswahili?

mie simo mkjj yatayokukuta
Hii ndiyo ile hadithi ya pwagu na pwaguzi kwa wale mliokuwa mnafuatilia kipindi hicho enzi ya RTD waliposema tuna watanzania kadhaa na wamakonde kadhaa ilhali hao wanaoitwa wamakonde ni wazaliwa wa tanzania na uraia wao hauna mashaka.
 
ilimu....ustaadh wangu mswahili...ilimu!.yawezekana kabisa alikuwa na yake,lakini watoto wetu hawakupiganiwa kuifahamu ilimu dunia vizuri.

tuliwachapa bakora pale walipotega kwenda madrasa,lakini si walipoachafanya homework zao!

kama tungalifanya hayo ungalitukuta nasi tuko tumejaa kila pande....ila tupo kidogo kwenye sehemu sehemu,ila haitoshi ukilinganisha na wengine....sababu ni hiyo ustaadh!
 
Tunaomba wale ambao wanadataz za Office nyengine kama Ikulu, Ujenzi, mambo ya nje, mipango BoT na office nyengine nyeti za serikali basi watumwagie hapa ukumbini ili tuone kama kweli na huko kuna ukabila ama la, au ukabila upo TRA tu???
 
Same QN I wanted to ask. Thread imelalia upande mmoja jama! Tusiangalie TRA tu; twende ofisi nyingine kama thread inavyoonyesha kudhamiria!

Now; what about Ikulu, Wizara ya Ujenzi (Miundombinu?), Wizara ya Mambo ya nje, Wizara ya Mipango, BoT na ofisi nyinginezo...

Mswahili/wengineo hope tuna data zaidi katika ofisi hizo juu ya ukabila unaopigiwa makelele kila kukicha.

Shukrani
 
Ukabila uko kwenye taasisi za fedha.. na ukabila huo unawahusu Wachagga tu!
 
tumemaliza ya TRA. next stop Ikulu tujadili wachaga na "wakilimanjaro" wanavyomhujumu Muungwana.
 
Mzee MWANAKIJIJI NA Joka kuu.
mawazo yenu hapo juu ni makini sana. mmezungumza jambo la mbolea sana.
endeleeni hivyo kwani mmejua ubaya wa ukabila.
 
Mie nilishaanza Ujenzi na ule utaratibu wa Tanroads. na kazi za KINA LYATUU.
NILIJARIBU kutizama why ujenzi wa mabarabara ulikazania tu Kilimanjaro na nikapata jibu.
lakini nikarudishwa tena TRA.
 
Mswahili... ningefurahi ubandike kile ulichonitumia PM... nafikiri watakuelewa ni kwanini mzalendo kama wewe unavyopinga ukabila....! Au nipe rukhsa miye nibandike..!
 
msitubanie bandikeni, au ziko more confedential? pengine mkiziweka hapa zitasaidia kujua ukweli ni upi?
 
mtu mwitu namsikiliza mswahili aamue.. ameniandikia kitu kimoja very interesting...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…