Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,191
- 677
dua sijakuelewa??? nifafanulie ngoma kubwa kivp?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tumemaliza ya TRA. next stop Ikulu tujadili wachaga na "wakilimanjaro" wanavyomhujumu Muungwana.
huwa najiuliza wakati wa Mwalimu akina malima,msabaha,etc sijui walikuwepo shule au vp.
Mwanakijiji Hii Idadi ya makabila imeitoa wapi?Ni sensa ya mwaka gani hiyo?Tuliuliza itawezekana vipi watu wa pwani kujazana katika nafasi nyingi za ajira wakati idadi yao ni ndogo? Nikatoa mifano ya makabila ya pwani:
Wakwere = 98,000
Wandengereko = 110,000
Zaramo = 657,000
Segeju = 7000
Wadigo = 88,000
Wabondei = 80,000
Wazigua = 355,000
Wasambaa = 664,000
Jumla = 2,059,000
Idadi ya Wachagga = 2,000,000!
Nimekuelewa,Hata hivyo ni kama vile umeshanipa kwani huo mwaka tu unanitosha kuweza kupata source.Nitaenda fuatilia ili kuona na makabila mengine hasa wasukuma kwani eneo lao kubwa na wako wangapi na ndiyo Kambi kuu ya ushindi wa CCM kwa Tanzania Bara.Idadi hiyo ni ya mwaka 2000! na rahisi kupata kwenye mtandao...KNKCU, ningekupa wapi nimepata sasa nikifanya na hivyo nitakuwa nimewarahisishia watu kazi... nitakuwa nimeng'ata, kutafuna, na kuwamezea.. wao washibe tu! So.. waache wafanye kazi kidogo ya kufanya ya kutafiti
Unajua baada ya kuweka hayo makabila hapo ubongo umeklick na kutaka kufanyia kazi eneo fulani.fanya hima utuambie Wasukuma wako wangapi? halafu jumlisha na Wanyamwezi... Halafu angalia Wahaya wako wangapi, na Wanyakyusa wako wangapi...!
ilimu....ustaadh wangu mswahili...ilimu!.yawezekana kabisa alikuwa na yake,lakini watoto wetu hawakupiganiwa kuifahamu ilimu dunia vizuri.
tuliwachapa bakora pale walipotega kwenda madrasa,lakini si walipoachafanya homework zao!
kama tungalifanya hayo ungalitukuta nasi tuko tumejaa kila pande....ila tupo kidogo kwenye sehemu sehemu,ila haitoshi ukilinganisha na wengine....sababu ni hiyo ustaadh!
Najitahidi kweli kuona haya majibu wazi.
Very good! nimesubiri mmoja wenu alete hii point kwa sababu nimeshasema ukabila mnaozungumzia ni wa "idadi ya watu wa kabila moja mahali pa kazi" na wala si hisia ya kujiona bora, kustahili zaidi, na kukandamiza watu wa makabila mengine. Ukabila huu mnaouona nyinyi unatokana na kulinganisha na idadi ya watu wa makabila mengine? Je kuna wasomi wengi wa Kisukuma na Kinyamwezi (makabila makubwa zaidi Tanzania?) Hebu tuangalia idadi ya makabila makubwa zaidi Tanzania (unaweza kupata info hapa www.ethnologue.com) Makisio ya 2000
- Wahehe est. 750,000
- Wandengereko est. 110,000
- Wazaramo est. 656,000
- Wadigo Est. 88,000 (Tanzania, 300,000 Kenya)
- Wairaqw Est. 462,000
- Waluguru Est. 692,000
- Wazanaki est. 62,000
- Wakwere est. 98000
- Wasukuma est. 3,200,000 (kabila kubwa zaidi)
- Nyamwezi est. 2,000,000 (kabila la pili kwa ukubwa likifunganga na Wachagga) ni ndugu za wasukuma
- Wagogo Est. 1,300,000 (Wanawazidi Wanyakyusa kidogo kwa wingi)
- Wamakonde est. 1,100,000
- Wapare est. 1,000,000
Haya makabila hayo matatu
- Haya est. 1,200,000 (1991)
- Chagga est 2,000,000
- Nyakyusa est. 1,000,000
A. Sasa kwa kufuata logic ya wingi peke yake Wasukuma na Wanyamwezi ndio wangekuwa wengi zaidi katika kila kona ya nchi na katika kila ofisi. Hali siyo hivyo kwanini, wakati tumeambiwa kuwa kuanzia miaka ya 70 watu wote wamepewa nafasi sawa ya kusoma? Kwanini wasukuma hawajapata nafasi nyingi za ajira kuliko watu wengi wa pwani wakati nafasi za kusoma zipo wazi kwa wote? Hivi hawa wote wamebaguliwa na kunyimwa nafasi za kazi licha ya kuwa na elimu sawa na watu wa makabila hayo matatu? Nitafurahi kuona ushahidi wa hilo.
B. Wahaya ni mara mbili ya Wazaramo na ni mara 12 ya Wakwere. Wachagga ni mara 10 zaidi ya Wadigo na Wandengereko combined! Wanyakyusa ni mara tano ya Wadigo na Wandengereko combined! Makabila hayo matatu combined ni zaidi ya makabila hayo nane ya kwanza! Sasa mtu aniambie iweje makabila madogo moja moja yawe na watu wengi maofisini kupita makabila haya matatu moja moja? Kama kabila lako lina watu 68,000 na wote wasomee uhasibu, na wote waajiriwe na serikali bado kuna watu zaidi ya milioni moja upande wa uchagga ambao nao wanataka nafasi hizo!!!! Hivyo hata kama nafasi zote za ajira za serikali zipewe watu wa makabila hayo nane, still makabila ya Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa wanao watu wengi zaidi kuwazidi waajiriwa hao wapya!!! Unless makabila madogo madogo wazaane kwa wingi na kufikia idadi ya makabila hayo matatu, na wakati huo huo watu wa makabila hayo matatu waache kuzaana wakiwasubiri hao ndugu zao... there will never be parity!!!! Huo ndio ukabila mnaouzungumzia!!
C. Kama kuna watu katika Tanzania ambao wanaweza kudai ukabila na kuonewa ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wagogo, Wamakonde na Wapare ambao wote wana idadi zaidi ya milioni moja? Ni kwanini makabila hayo matano hayajaingia katika nafasi nyingi? Je hii yote ni njama za Wanyakyusa, Wahaya, na Wachagga?
Ndio umeniambia, ila ushahidi hukutoa na mimi si mmojawapo!
Sifikiri mimi niko kundi hilo!
Najaribu kuuona huu "uwazi" wa wachagga kupungua. Je wamepungua kwenye population kitu kilichosababisha wao kupungua mashuleni na vyuoni.
Please cite one study for me, iliyofanywa Tanzania..! general studies can be applied anywhere hata msituni.
Wala sijakimbia, huwezi kuchagua kitengo kimoja, mipaka miwili na ofisi tatu kujenga maoni ya jumla! Kwa watoto wa chekechea inaweza kuwafanya waduae, ila kwa watu wazima tunaoweza kusoma katikati ya mistari tunasema:
- Tupeni vitengo vyote vya TRA na viongozi wake
- Tupeni wakuu wa vituo vyote vya mipakani na ofisi zote za mikoa za TRA
- Tuonesheni kuwa wote walioajiriwa hawana elimu (sizungumzii walioteuliwa). Nionesheni Mhasibu TRA anayefanya kazi ambaye hajasomea uhasibu n.k
Hatubishi alimradi tunabisha tu, na haturukii treni hili la ukabila kwa vile watu fulani wanaimba nyimbo mzuri. Naomba mnishawishi kwa hoja zenye nguvu badala ya maneno ya mvuto! Narudia tena hakuna ukabila wa kibaguzi Tanzania kama jumuiya nzima, isipokuwa ule uliomo ndani ya wale wanaoutafuta. You can't conclude and then find the evidence to support your conclusions! Na pia mimi si mtoto mdogo ambaye sielewi kuwa kuna watu mmoja mmoja ambao wanasukumwa na ukabila na watu hawa hawako kwenye makabila hayo matatu tu, wapo na wa makabila mengine kama tulivyoshuhudia mumu humu!