Veta Nako Wamejikita Wachagga Watupu Kama Chadema.
CHADEMA wamejikita wachagga watupu namna gani? Tupe takwimu za ngazi mbalimbali!
Nashauri uendelee kujikita katika mjadala ulioko katika thread hii badala ya kuanzisha mjadala kuhusu CHADEMA. Kama unataka kuijadili CHADEMA ifungulie thread separate. Endelea kukata issues!
JJ
Rejea tamko la CHADEMA kuhusu suala hili
http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php ambalo pamoja na mambo mengine lifafanua kwamba
"Si kweli kuwa CHADEMA ni chama cha Wachagga kilichoanzishwa toka wakati wa kudai Uhuru!
Mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa wa historia ya nchi yetu, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA. Ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Na jina la CHADEMA lilibuniwa na Simon Madete ambaye ni Msukuma. Hii inatufanya tubaki na maswali mengi kuhusu nia ya wanaosambaza uzushi huu.
Si kweli kwamba CHADEMA imejaa Wachagga!
Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.
Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na Mu-Unguja.
Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?
Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa Kamati Kuu, kati yao hakuna mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?
Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?
Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi.
Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?
Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?
Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.
Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?
Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na Watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine.
Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga?
Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?
Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa.
Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.
Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini.
Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli. "