Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

mswahili plz tubandikie hapo ili tuweze kufika pazuri na kuangalia pengine maana kazi imebaki kubwa
 
ukurasa wa 100 ,...kweli hii ni record discussion moto kweli,mkimaliza TRA na kuingia kitengo kingine itakuwa busara.au tufanye summary au flashback ,,katika hizi kurasa 100 ,tumejifunza nini?????

tusonge mbele basi,,nchi ni kubwa hii!!!!
 
mswahili.......

halafu tupatie na data za wanafunzi wa kitanzania wanaosoma nje ya nchi kwa skolaships specially zinazotoka serikalini waislam na wakristo,vipi pale ELIMU YA JUU?mkuu hiyo issue ya mwalimu JK wee acha tu,huwa najiuliza wakati wa Mwalimu akina malima,msabaha,etc sijui walikuwepo shule au vp.

PM....mie kubwa nimejifunza kuwa ukabila tz upo tena kwa sana tu lkn hili suala limefumbiwa macho haswa huko TRA.

mkjj...wewe umejifunza nn ktk bandiko hili la TRA?
 
Mimi nimejifunza kuwa kuna Watanzania wenzetu ambao kwa sababu moja au nyingine wana chuki ya wazi dhidi ya Watanzania wenzao na kwa kutumia kisingizio cha uzalendo wanajaribu kuwanyima nafasi na ikibidi kuhakikisha kuwa baadhi ya Watanzania hawapewi nafasi ya kutumikia nchi yao!!

Zaidi ya yote nimejifunza kuwa ni rahisi zaidi kulaumu ukabila mahala pa kazi kuwa ni tatizo kubwa wakati tatizo kubwa la ajira Tanzania ni kujuana (kunatokana na sababu mbalimbali). Wale wanaotaka tuangalie ukabila wanafanya hivyo ili tufumbie macho matatizo makubwa zaidi!!

Kuhusu TRA yenyewe hadi hivi sasa nimeoneshwa majina ya wachagga wachache na kuambiwa kuwepo kwao kwenye taasisi hiyo ni kutokana na ukabila uliokithiri!! Tulipowauliza watetezi wa ukabila huu watuambie kuna makabila mangapi yanafanya kazi TRA, na ni wachagga wangapi ambao wamewahi kufukuzwa (katika mabadiliko ya 96 na mengine) au kinidhamu hakuna anayetaka kutuambia!!

Nimejifunza jambo jingine pia; nalo ni kuwa katika Tanzania yetu hii ya leo kuna watu ambao hawataki kuchunguza mapungufu yao na kuyarekebisha lakini wanafanya hima kulaumu matatizo yao kwa watu wengine!! Inanikumbusha jinsi Ulaya ilivyowalaumu Wayahudi kwa matatizo yao na hatimaye kuanza kuwaua kihalaiki!! Ni yale yale yaliyotokea Serbia, Iraq na sehemu nyingine! Kuna ndugu zetu hapa ambao wameamua kuwalaumu Wachagga kwa matatizo yao au ya sehemu zao!

Kwa ndugu zetu hao, Wachagga ni watu hatari kabisa ambao wamejazana kama mchwa na wanatafuna wasichopika, wakivuna wasipopanda, na wakijenga wasipokaribishwa! Ndugu zetu wakabila wa JF wanataka mbegu ya chuki ipandikizwe ndani ya mioyo ya watu kiasi kwamba ukiona jina la Mchagga kwenye maombi ya kazi hasa yakiwa matatu uamue kuajiri angalau mmoja tu ili usionekane kupendelea Wachagga!! Ndugu zetu hawa hawajaribu kutuonesha eneo lolote ambapo watu wamakabila mengine wanapeana nafasi za kazi au kupendeleana kwa namna moja au nyingine; of course hawawezi kuona sehemu hizo unless watu hao ni Wachagga!!!

Nimejifunza pia kuwa kuna Watanzania ambao kwa sababu zao wameamua kuamini kuwa kweli Tanzania kuna Ukabila na wao wenyewe pasipo kujua wameanza kuingiwa na hisia ya shuku dhidi ya Wachagga!! Ndugu zangu hao katika forum hii wameanza kuacha kuangalia mambo kiukweli na badala yake wanaangalia mambo kihisia!!

Tuliuliza itawezekana vipi watu wa pwani kujazana katika nafasi nyingi za ajira wakati idadi yao ni ndogo? Nikatoa mifano ya makabila ya pwani:

Wakwere = 98,000
Wandengereko = 110,000
Zaramo = 657,000
Segeju = 7000
Wadigo = 88,000
Wabondei = 80,000
Wazigua = 355,000
Wasambaa = 664,000

Jumla = 2,059,000

Idadi ya Wachagga = 2,000,000!

Sasa hata kama nina ukabila kiasi gani, ni kitu gani kitanifanya niamini kuwa kuna ka uwezekano ka watu wa pwani kujaza nafasi nyingi wakati idadi ya makabila nane makubwa ya pwani ni karibu sawa kitakwimu na kabila moja la kaskazini? Hivi kweli kuna uwezekano wowote mtu akitangaza nafasi za kazi miongoni mwa waombaji watakuwemo Wachagga?

Kubwa jingine nililojifunza ni kuwa watu hawataki kuangalia takwimu hata kama utawawekea a magnifying glass mbele yao!!
 
nilipoingia kwenye mjadala huu niliyasema hayo....we umeongezea zaidi.

nilichokiona ni maskhara ya watu ilhali wao wanalijua hili,hata kama haliku-click, kwa kuwakumbusha wangeliona.

nikajiuliza...tunaongea juu ya ukombozi wa maendeleo ya taifa letu...kwa mtindo huu tutaendelea?.

watu barza bwana! nikakaa barzani nika kalaga bao!

sasa,kwenye barza kuna mengi,wenye hikma wanajua watakusanya yote walosikia au kuambiwa na kuyafanyia kazi.

wengine ukiingia usiku watarudi makwao kuwasha karabai,kupata mlo na hatimae kupumzika[pwani ndivyo ilivyo]...kesho,kwenye barza tena!

tutafika tu!....ila wengine wakiwa mbele,wengine kati na wengine nyuma...safari huwa hivyo,infact wengine hawafiki...huachwa njiani!
 
Mwanakijiji Hii Idadi ya makabila imeitoa wapi?Ni sensa ya mwaka gani hiyo?
 
Idadi hiyo ni ya mwaka 2000! na rahisi kupata kwenye mtandao...KNKCU, ningekupa wapi nimepata sasa nikifanya na hivyo nitakuwa nimewarahisishia watu kazi... nitakuwa nimeng'ata, kutafuna, na kuwamezea.. wao washibe tu! So.. waache wafanye kazi kidogo ya kufanya ya kutafiti
 
Nimekuelewa,Hata hivyo ni kama vile umeshanipa kwani huo mwaka tu unanitosha kuweza kupata source.Nitaenda fuatilia ili kuona na makabila mengine hasa wasukuma kwani eneo lao kubwa na wako wangapi na ndiyo Kambi kuu ya ushindi wa CCM kwa Tanzania Bara.
 
fanya hima utuambie Wasukuma wako wangapi? halafu jumlisha na Wanyamwezi... Halafu angalia Wahaya wako wangapi, na Wanyakyusa wako wangapi...!
 
fanya hima utuambie Wasukuma wako wangapi? halafu jumlisha na Wanyamwezi... Halafu angalia Wahaya wako wangapi, na Wanyakyusa wako wangapi...!
Unajua baada ya kuweka hayo makabila hapo ubongo umeklick na kutaka kufanyia kazi eneo fulani.
Siahidi Lakini ninataka nijaribu kupata karibu makabila yote huenda nikapata kitu cha kufanya baada ya kupata hizi data.
 

Dar si Lamu.
unatuumiza roho zetu sana kwa kauli ya kujikomba hapo juu. hivi hujui wazee wetu mwaka 1964 tayari walikuwa na mpango wa uzinduzi wa chuo kikuu? na Makaptula (Nyerere) ndiye alikuwa mgeni rasmi wa kuweka jiwe la msingi.?

university hiyo ilikuwa ifundishe masomo yote na Said Tewa na Bibi Titi Mohammed wakaja kupata balaa kubwa kutokana na kuiunga mkono jumuia ya waislam. chini ya Al-Markhum sheikh Hassan Bin Amir. jiulize wakati huo waislam wanawaza kuwa na chuo kikuu sio sekondari leo wangekuwa wapi?

Tumaini university imekuja kufunguliwa 1997 wakati sisi kitu chetu kilikuwa kiwe uwanja wa Taifa 1964. hujui wizara ya elimu ilikuwa marufuku kwa waislam kushika ngazi ya juu ya uongozi na ilikuwa haramu muislam kuwa waziri wa elimu. Nyerere aliweka wakurugenzi 12 wizara ya elimu ambao ni mapadri unategemea nini?

jiulize nyerere toka katawala hadi anaondoka kuna shule yeyote iliyojengwa Dar? hujui kama Tambaza, Azania zilikuwa shule za waislam? hujui kama Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa-Asha Migiro alianza primary school mnazi mmoja -Dar ambayo ilikuwa mali ya waislam?
1964 waislam walikuwa na scholarships 36 kila mwaka walipata toka kwa rais Abdul Nassir wa Misri. Nyerere akapiga buti na kuiua jumuia yetu, Hujui kama Ruksa alijitahidi tujiunge OIC ili tupate huduma za jamii Nyerere akavuruga?
kifupi kama si kufungwa spidi gavana na Nyerere huku wenzetu wakiwa free kufanya walitakalo. basi hali tusingekuwa nayo.
Nyerere katumaliza hilo hatulisahau.
pitia wastaafu wa East -Africa ndio utajua tulikuwa vipi tunawajibika.
 
Chifu Makwaia wa Wasukuma afariki




na Joel Makwaia




ALIYEWAHI kuwa mjumbe wa kwanza wa Baraza la mkoloni la kutunga sheria kabla ya uhuru, Chifu David Kidaha Makwaia (86), amefariki dunia.


Taarifa iliyotolewa na Frank Makwaia, ambaye ni mdogo wa marehemu, ilisema kuwa Chifu Kidaha alifariki dunia Machi 31, mwaka huu, katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kifo chake kimetokana na ugonjwa wa moyo.


Makwaia alisema kuwa, taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa ambapo leo wananchi wa Manispaa ya Moshi watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa hayati Chifu Kidaha, nyumbani kwake maeneo ya Shanti Town.


Kesho, mwili huo utapelekwa kijijini kwake Ibadakuli, katika Manispaa ya Shinyanga, ambako siku ya Jumatatu asubuhi mazishi yatafanyika kwa heshima zote za kichifu kwa kufuata mila na desturi za kabila la Kisukuma.


Mazishi hayo yanatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa nchini.


Chifu Kidaha alizaliwa mwaka 1921 mkoani Shinyanga na kupata elimu yake ya sekondari katika Shule ya Tabora (Saint Mary's), kati ya mwaka 1936 – 1940. Baada ya hapo alijiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda na kuhitimu Diploma ya Kilimo kati ya mwaka 1941 – 1944.


Kati ya mwaka 1949 – 1950 Chifu Kidaha alijiunga na Chuo Kikuu cha Lincoln, nchini Uingereza (Lincolin College Oxford University) kwa ajili ya kusomea philosophy na siasa.


Kabla na baada ya uhuru, Chifu Kidaha amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwemo ile ya Ujumbe wa Baraza la Mkoloni la Kutunga Sheria kuanzia Mwaka 1945 – 1958. Baadaye nafasi hiyo ilichukuliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.


Mwaka 1958, aliteuliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Williamson Diamonds, wakati huo ikiwa ni kampuni iliyokuwa inajishughulisha na utafutaji wa madini ya almasi Mwadui – mkoani Shinyanga. Nafasi hiyo alidumu mpaka mwaka 1961.


Kati ya mwaka 1959 – 1961, pia alikuwa ni Ofisa wa Uhusiano katika Kampuni ya First Permanent Building Society Limited. Kampuni hii ilikuwa inafanya kazi zake katika nchi za Uganda, Kenya, Tanganyika na Zanzibar.


Mwaka 1964, hayati Chifu Kidaha aliteuliwa kuwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Bandari na Reli (East Africa Railways and Houbours) ambapo alistaafu mwaka 1975.


Kuanzia mwaka 1976 – 1998 Chifu Kidaha alikuwa wakala wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) katika Manispaa ya Moshi.

Hayati Kidaha alikabidhiwa rasmi uchifu wa Kabila la Wasukuma mwaka 1945 baada ya Chifu Makwaia Mwandu kufariki dunia. Hayati Kidaha ameacha watoto na mjane.
 
Phillimon mikael.
Huyu nae ni chifu mbona hujaweka tanzia yake? ulikuwa busy na Chief Marealle tu? huyu mzee 1949-1950 yuko Oxford anakula kitabu angekuwa mchagga tusingelala humu.
 
KNKCU mada hii niliandika huko nyuma... kwenye ukurasa kama 17 hivi.. naona nirudie hapa...

 
Mwanakjj.
mara mwisho tumekubalina kuwa kuna interview. pia uliunda tume ambayo bado hatujakabidhi ripoti, unasema tulishindwa kujibu hoja? sisi tuna hoja zetu tunazotaka kuzimwaga moja kwa moja kwenye interview au unataka kumpelekea Kittlya maswali in advance?
 
mswahili....duh umesema maneno mazito wewe kuhusu issue ya chuo kikuu na waislam enzi za mwalimu nyerere,lkn nimekuwa najiuliza sisi znz tuliwaondoa waarabu 1964 almost 42 yrs leo hii lkn tupo nyuma kweli and almost 90% waislam,wizara zote zimeshikwa na waislam ukitoa ya mawasiliano(retr brigd mwakanjuki),ndio kwanza tuna vyuo vikuu 3 tena habari nilonazo vyote hivyo havina usajili wa kudumu kutoka bodi ya usajili ya vyuo vikuu vya tz,KULIKONI hili?ama kweli safari ni ndefu,lkn mola akipenda tutafika.nafikiri unaifahamu shule ya AL-HARAMAINI,KINONDONI MUSLIM etc zimefikwa na majanga gani zile?ni shule zetu waislam,tumeshindwa kuziendesha au mambo ya u-SUNNI na u-SHAFI umeua shule zile?hebu tueleze kidogo.

mie nafikiri hilo suala la mkjj kuhusu interview tuliwache twendeni ktk angle nyengine au waonaje,UMESHINDA mkuu kwa data zako.


mkjj....sema naye mswahili na kubali kuwa ameshinda kuna issue kibao tu hapa inabidi tuongee nyengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…