Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Injinia Mohammed.
Mwalimu alihakikisha Znz hawana chuo kikuu na masomo kama ya biashara aliyapiga marufuku kule kwani hayo ndiyo yanayopelekea kwenye menegement. hata vilivyopo wenyewe hawapendi wanafuata usia wa mwl.

acha ZNZ jiulize toka ametoka Nyerere Madarakani vyuo vikuu vingapi vimenzishwa? wastani wa chuo kikuu kimoja kwa kila mwaka au kwa miaka miwili toka atoke madarakani Nyerere.

Mzee yule katubana sana kielimu si kwa waswahili tu hata watu wengine.
 
KNKCU mada hii niliandika huko nyuma... kwenye ukurasa kama 17 hivi.. naona nirudie hapa...
Mwanakijiji nimeipata ktk kuperuzi peruzi na kugoogli na Kuna sehemu wanasema hata wasukuma wanaongoza kwa Ethnolinguistic kwa kuwa na 9.5%,wanafuatiwa na wahehe na wabena 4.5%,wagogo 4.4%, Haya others 5% source Britanica.
Kwa mtazamo huo makabila hayo mbali na kiswahili bado hayakupoteza matumizi ya lugha zao kwa mapana.
 
pole sana.. kijana. maumivu yakizidi muone daktari!!

Nimemwona daktari, na anasema chanzo cha uonevu....I mean maumivu, kiko TRA bila ubishi.
Katika page hizi zote, mimi nimejifunza kwamba, 'journalist' yoyote wa kibongo ni mgumu kuwa neutral. Ni lazima achague upande, which makes them lose credibility to the observant eye.
Sasa sijui kuna mtu kaambiwa wasaidizi wa Mhe. ni wachagga, basi its sucking up big time, so one can get an interview by any means neccessary.
Wachagga tunachanganyika nao kama kawa, ila dont divert the fact that there is problem pale TRA. And one should be ashamed to compare those who realise there is a problem at TRA, with Hutus and Tutsis.
 

Defunkadelic,
Ninakubaliana na wewe .Ninadhani watu wameshachukua upande wao au kwa kujua au kwa kutokujua kiundani.sasa sijui kama kila kabila likija na hizo mbinu zinazotumiwa sijui kama tutafika.
 
Unajua tatizo letu wengi hapa tumekuwa tunang'ang'ania vitu bial kutumia utashi wa kutosha.

Binafsi nadhani swala la TRA ni la kiukoo zaidi kuliko Kikabila. Kwa hiyo mnapozungumzia kabila mnatakiwa muelewe wazi kuwa Wachaga wamegawanyika kwenye KOO zaidi ya ishirini, na ndani ya hizi KOO kuna ambazo haziivani hata kidogo siyo kwenye ajira tu bali hata kwenye mambo ya kijamii kama kujenga au kuishi sehemu moja.

Ukiingia pale TRA utaona watu wa UKOO fulani wapo kwa wingi sana kuliko UKOO mwingine. Mfano unaweza kukuta UKOO wa MUSHI au MOSHI umejipanga kuanzia daraja moja hadi lingine, na hamna ukoo mwingine kutoka uchagani. Sasa hapa tutasema ni UKABILA au UKOO.

Hili swala nimeshalikuta sana TRA na sehemu nyingine kama UHAMIAJI.

Swala la Mchagga ni ligumu kuliko tunavyolichukulia hapa. Watu wengi wanachukulia kwa sababu mtu katoka Kilimanjaro ni Mchagga na hivyo wachagga wanapendeleana.

Kwenye Kabila la MCHAGGA kuna Wakibosho, Wakirua, Wamachame, Waold Moshi, Warombo, Wakilema, Wauru nk.

Na katika haya Makundi kuna KOO kama Massawe, Mushi, Masao, Kulaya, Msele, Kwai, Nkya, Kombe, Lema, Mboya, Mremi, nk.

Kwa mtu anayefahamu wachagga kwa ndani au mchagga mwenyewe atakuambia kuwa wachagga wa koo tofauti mara nyingi hawaivani. Au ukitaka mfano Mzuri nenda kwenye Maduka ya Nguo, Redio nk pale Kariakoo.

Mwsiho wa siku nadhani kila mmoja atabakia na kile anachoamini. IMANI NI KITU KISICHOFUTIKA. Mtu akiamua kuamini kitu hata ukimpa ushahidi wa kupinga anachoamini haachi kuamini anachokiamini. Kama mtu anaamini rangi anayoona ni NYEKUNDU angali watu Wengine wote wanaona ni RANGI ya BLUU bado ataendelea kuamini anaona rangi Nyekundu.
 
aljazeera, hivi kati ya tatizo la kupeana ajira kiushkaji, kwa kufahamiana, kujuana na kiundugu na tatizo la kupeana kazi kwa kuangalia kabila, ni tatizo lipi unafikiri ni kubwa zaidi Tanzania na ambalo linatishia zaidi utendaji kazi, ufanisi, na nidhamu ya kazi? Na hapa sizungumzii kitendo au idara moja..nazungumzia kiujumla
 
Mwanakijiji,
vigezo na bench marks za kuhakiki madai ya huo ukabila ni vipi? yalishaletwa majina ya watumishi wa tra na tukajionea kwamba wachaga/wakilimanjaro hawajazidi kiidadi.

wengine wakadai kuna hujuma katika miradi ya ujenzi wa barabara. personally nikaleta jedwali la ripoti ya miradi ya barabara toka tanroads. ukilichunguza jedwali hilo utakuta kwamba kilimanjaro haiongozi kwa kuwa na miradi mingi.

vilevile taarifa za tanroads zinawiana na bajeti wizara ya miundo mbinu iliyosomwa na waziri mramba. vilevile ukichunguza manegement ya tanroads utakuta hakuna wachaga wengi.

zikaletwa taarifa kwamba wizara ya elimu/mamlaka ya elimu inahujumiwa na wachaga. napo nikawaletea webpage ya mamlaka ya elimu tanzania. manegement yake haijasheheni wachaga. taarifa ya fedha ya mamlaka hiyo haioneshi kwamba kuna upendeleo wa waziwazi wa shule za uchagani/ukilimanjaroni.

yaani haya madai yamekuwa so ridiculous kiasi cha wale wanaoyatetea kuzua kabila jipya tanzania, "WAKILIMANJARO." Madai mazito kama haya shurti yatetewe na DATA, siyo ufundi wa kupiga mayowe.
 

Mkjj, nimekuwa nikijiuliza na kushangaa ni kwa vipi wengi wetu humu JF hatuupati ujumbe mahususi unaotakiwa tuuelewe. Nadhani ni sababu ya staili tu inayotumiwa katika kuwakilisha hoja ndiyo inayotuchanganya wengi.
Ukabila wa uchaga ni kisingizio tu cha kufikisha ujumbe; hoja mahsusi hasa ni DINI. Ninaelewa maswala ya udini kwa waTz wengi wanayaogopa, hata kule kuyazungumzia tu; lakini kuna baadhi ya watu (wachache?) kama akina Mswahili ambao wameyavalia njuga kikwelikweli. Inafaa sasa waache kubabaisha kwa kisingizio cha ukabila wa wachaga, ili watu waweze kuzungumzia ukweli au uongo wa hii dhana ya kuonewa kwao kwa sababu tu ya dini zao.
 


maneno yako yanavutia....kama sukari ilo na mchanga ndani yake!...utanisamehe ustaadh lakini ndio kweli.

ina maana ile shule iliyopo pale karibu na uwanja wa taifa ilikuwa iwe chuo kikuu?....bibi titi huyuhuyu tunayesikia alimfanyia hila jkn?
 

mhandisi,

ningekuwa ninatoa tenda...ningekupatia weye[sijui kama unajenga barabara au vipi]....huwa ukweli unauweka bayana!. humfichi mtu kitu....na huo ndo utu uzima!

nshamwambia,mi akinichanganyia sukari na mchanga nitabaini...hata kama napenda vitamu!
 


kwani bara vilikuwa vingapi wakati anafariki?
 

ushaangalia ...sometimes in april...?hebu tazama hiyo halafu utaona media ilivyo-play part kwenye uovu uliojengwa na uongo![ukiondoa historia ya rwanda]
 
Dar si Lamu.

Nyerere wakati anaondoka madarakani aliacha chuo kikuu cha Dar-es-salaam na Sokoine morogoro tu.

piga wewe hesabu sasa. Iringa kuna university karibu tatu. Morogoro kuna Tatu. Mwanza si chini ya mbili.Kilimanjaro hazipunguwi tatu. Zanzibar kuna tatu, Dar kumeongezeka Open university,CBE kama sikosei. kuna masters zinatoka IFM, Kairuki medical university,Dodoma nako unasikia,

Nadhani Mbeya nao watakuwa wako njiani. na jamaa zetu wa Bukoba walitaka kujaribu ila nina wasiwasi na standards za chuo chao usikihesabu kama IMTU nacho nina wasi wasi nacho.
Na watu tumeweza kusafiri na kutafuta elimu nje ya mipaka. kipindi cha Mwinyi, Mkapa kumetokea scholarships nyingi tu na hadi sasa kwenye Kasi mpya kinyume na Nyerere. Vijana wamekwenda Nchi Mbalimbali. kama Angekuwa bado madarakani asingeturuhusu.
 

fikra za mwenyekiti zidumu....zidumu!....hii ndio iliyosababisha baadhi na si yote ya hayo unayomtuhumu!
 
Veta Nako Wamejikita Wachagga Watupu Kama Chadema.

CHADEMA wamejikita wachagga watupu namna gani? Tupe takwimu za ngazi mbalimbali!

Nashauri uendelee kujikita katika mjadala ulioko katika thread hii badala ya kuanzisha mjadala kuhusu CHADEMA. Kama unataka kuijadili CHADEMA ifungulie thread separate. Endelea kukata issues!

JJ

Rejea tamko la CHADEMA kuhusu suala hili http://www.chadema.net/tamko/2007/mwanri.php ambalo pamoja na mambo mengine lifafanua kwamba
"Si kweli kuwa CHADEMA ni chama cha Wachagga kilichoanzishwa toka wakati wa kudai Uhuru!

Mtanzania yeyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa wa historia ya nchi yetu, atakubaliana nasi kuwa katika orodha ya vyama vya siasa vilivyokuwepo kabla ya uhuru, hakuna chama kilichoitwa CHADEMA. Ukweli ni kuwa CHADEMA ni chama kilichoanzishwa na kusajiliwa mara baada ya Tanzania kuingia katika mfumo wa vyama vingi. Na jina la CHADEMA lilibuniwa na Simon Madete ambaye ni Msukuma. Hii inatufanya tubaki na maswali mengi kuhusu nia ya wanaosambaza uzushi huu.

Si kweli kwamba CHADEMA imejaa Wachagga!

Kwa akili za kawaida, shutuma kwamba CHADEMA imejaa wachaga maana yake ni kwamba CHADEMA ina viongozi na wanachama wengi wachagga kuliko kabila lolote hapa Tanzania. Je ni kwa kiasi gani kauli hiyo ina ukweli?.

Katika safu ya juu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA yenye viongozi sita: wenyeviti na makatibu mchaga ni mmoja tu-Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe. Viongozi wengine wanatoka makabila mengine kama MuIraq, Myao, Mpemba na Mu-Unguja.

Aidha katika sekretariati ya chama taifa ambacho ndio chombo kinachosimamia utekelezaji wa kila siku wa shughuli za chama kikiwa na kurugenzi 9, kati ya wakurugenzi wake mchaga ni mmoja tu. Na wasukuma ni watatu. Kwa nini hawasemi kwamba CHADEMA ni chama cha wasukuma?

Kadhalika mpaka sasa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ameteua wajumbe wanne wa Kamati Kuu, kati yao hakuna mchaga hata mmoja na kati yao wawili ni wahaya, Profesa Mwesiga Baregu na Balozi Ngaiza. Kwa nini hawakusema kwamba CHADEMA ni chama cha wahaya?

Kwa upande mwingine kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi uliopita, jimbo ambalo CHADEMA iliongoza kwa uwingi mkubwa zaidi wa kura ni Tarime ikiwa asilimia zaidi ya 64. Kama CHADEMA ni chama cha wachaga kwa nini jimbo la kwanza lisingekuwa la mkoa wa Kilimanjaro?

Kati ya majimbo kumi ambayo CHADEMA ilifanya vizuri zaidi, jimbo la Kilimanjaro ni moja tu la Moshi mjini huku mikoa kama Kigoma, Rukwa ikiwa na majimbo mawili ambayo CHADEMA imefanya vizuri zaidi.

Kama CHADEMA ingekuwa chama cha wachaga si ingefanya vizuri zaidi katika majimbo ya Kilimanjaro?

Je, wanataka kutuambia kuwa Mara, Kigoma, Rukwa na mikoa mingine ambayo CHADEMA imefanya vizuri kote kumejaa wachaga?

Kwa mantiki hiyo basi, si kweli kwamba CHADEMA ni chama kilichojaa wachaga. CHADEMA ni chama cha kitaifa. Kinachojumuisha wanachama na wapenzi wa asili na hali mbalimbali.

Lakini swali la kujiuliza ni je wachaga hawana haki ya kuwa sehemu ya viongozi katika taifa na wanachama wa CHADEMA?

Zaidi ya hayo tunawashangaa wakitoa hoja kwamba CHADEMA imejaa wachaga. Lakini tunawashangaa zaidi kwa kuwa hatukuwasikia akisema chochote pale Rais Kikwete alipoteua wachaga na Watanzania wenye asili ya Kilimanjaro wengi zaidi katika baraza la mawaziri kuliko makabila mengine.

Je, kwa mantiki ya wazushi kama hao serikali ya Kikwete ni ya wachaga? Je, kwa kuwa wachaga ndio kabila lenye wabunge wengi zaidi kati ya wabunge wa viti maalumu wa CCM na CHADEMA, je kwa kigezo hiki tu tuseme kwamba CCM na CHADEMA ni vyama vya wachaga?

Je, kwa CCM kuwa na wabunge wa viti maalum wachaga hata katika mikoa mingine ya nchi yetu zaidi ya Kilimanjaro wanapotoka wachaga je, kwa uchambuzi wa wazushi kama hao wanaweza kusema kwamba CCM ni chama cha wachaga?

Hatukupenda kujadili viongozi kwa kutazama makabila yao. Lakini tumeamua kutoa uchambuzi huu kwa sababu suala la ukabila ni nyeti sana kwa mustakabali wa nchi yetu na kwamba kwa kutoa mifano hai tutathibitisha wazi uzushi wa watu hawa.

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuasa kwamba kufanya dhambi ya ubaguzi ni kama kula nyama ya mtu, ukianza huwezi kuacha.

Sisi tunaamini kauli za wazushi kama hawa zinapandikiza mbegu ya ubaguzi miongoni mwa watanzania na kuwashawishi watu kutazamana kwa misingi ya makabila yao. Tukiwaruhusu watu kama hawa tutaweka mashakani mshikamano na amani yetu hapa nchini.

Tunatoa mwito kwa watanzania kupuuza na kukumea kauli za viongozi kama hawa. CCM inaendelea kukumbatia wazushi hawa na uzushi wao, watanzania watakuwa na kosa gani wakianza kuamini kwamba chama tawala kinapandikiza mbegu za ubaguzi? Na kwa upande mwingine, tunatoa rai kwa vyombo vya habari kuchambua kwa kina kauli za watu kama hawa kwani uwongo ukisemwa sana wananchi wanaweza kuaminishwa kwamba ni ukweli. "
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…